Idimi
JF-Expert Member
- Mar 18, 2007
- 15,300
- 11,115
CCM Ilala kuandaa makada wake kuanzia shule za awali
2007-10-29 18:26:54
Na Mariam Mkumbaru, Ilala
Katika kujihakikishia kuwa hapo baadaye kinakuwa na wanachama imara zaidi na waliopikika kuwa makada wa kweli, Chama cha Mapinduzi, CCM wilayani Ilala kimeanzisha utaratibu wa kutoa mafunzo maalum kwa watoto wa shule ya awali kuhusiana na chama chake.
Akizungumza katika mkutano na viongozi wa chama hicho na wanachama wengine wa chama hicho katika Kata ya Kitunda, Mwenyekiti wa CCM wilayani humo Bw. Suleiman Kalanje, amesema watoto wakiandaliwa kuwa wanachama wa chama hicho tangu katika ngazi ya awali, baadaye itakuwa rahisi kuwa na makada wanaokipenda kweli chama hicho tofauti na sasa ambapo baadhi hujiegemeza katika chama chao kwa nia ya kutimiza malengo yao mbalimbali.
``Tuimarishe Jumuiya zetu kwa kujenga ofisi imara za matawi na kuanzisha shule za awali kwa ajili ya kuandaa wanachama wa kweli kwa siku za baadaye ambapo wakati huo sisi tutakuwa wazee ama hatupo duniani,`` akasema Bw. Kalanje.
Aidha, Bw. Kalanje akatoa wito kwa viongozi mbalimbali wa chama hicho wilayani Ilala kujiimarisha kwenye matawi yao na hatimaye kuwezesha chama hicho kuendelea kufanya kazi katika mazingira ambayo yatasaidia kuleta maendeleo ya chama hicho.
Aidha, akasema muda wa kuwekeana visasi kutokana na matokeo ya uchaguzi ndani ya chama hicho umekwisha na iliyobaki na kuendeleza umoja na mshikamano wa kuimarisha chama chao.
SOURCE: Alasiri
Nakumbuka kulikuwa na programu za namna hii tukiwa shule za msingi miaka kibao iliyopita, tukijulikana kama chipukizi. Sasa kama inaanzia chekechekea basi makada watakuwa kiboko!