Kauli ya Mbunge wa Ulanga ambaye ni kijana wa Marehemu Celina Kombani (aliyepata kuwa Mbunge wa Ulanga na Waziri katika wizara mbalimbali) kudai kuwa kama angekuwa na uwezo angeng'oa sanamu ya askari wetu pale City center na kusimika sanamu ya Diamond haiwezi kupuuzwa na watu makini!
Kauli ya Mbunge huyo imeonyesha ni kwa namna gani Mbunge huyo ana upeo mdogo sana, ukilinganisha na Wabunge waliowahi kutoka katika ukanda huo kama vile Marehemu Kasapira, Ponsian Nyami na hata kina Mzee Juma Ngasongwa! Unaweza hata kujiuliza mtu huyu aliwezaje kuwashinda wana CCM wengine katika kura za maoni kufuatia kifo cha Mama yake (Celina Kombani) aliyekuwa Mbunge hapo.
Ifike mahali Wana CCM tuachane na hii tabia ya kurithisha majimbo kwa watoto kufuatia vifo vya wazazi wao! Mfano ni Sioi Solomoni Sumari (japo hakupata),Godfrey Mgimwa, Omary Kigoda na sasa hili "Teja" la Ulanga!
CCM inapaswa muda wote kusimamia misingi yake ya kupata viongozi bora! Hatuwezi kuendelea na huu utamaduni mpya wa kutotaka kuwajua watu tunaotaka kuwapa uongozi kwa undani! Angalau tujue kabla ya kuomba uongozi shughuli zao ktk jamii ni nini!?
Tusije kushangaa siku huyu Mbunge wa Ulanga akiomba Ikulu yetu ya Magogoni igawanywe ili akina Diamond wapate sehemu nzuri ya kuweka Studio yao ya kurekodia na Ukumbi wa Disko!