Mheshimiwa Edward Lowassa, watu wanakutaja sana kuwa una nia ya kugombea urais.
Wakati huo huo unasikika ukihaha kila kona ya Tanzania ukitembelea makanisa mbalimbali na kutoa misaada mikubwa mikubwa kwa mahitaji mbali mbali ya makanisa hayo kama ambavyo umeripotiwa na vyombo vya habari hapa chini:
Kanisa lamuandalia tuzo Lowassa
Filikunjombe, Ligola wajitosa kambi ya Lowassa, wamnadi kanisani Iringa. | Dullonet Tanzania
Mzee wa Mshitu: Lowassa ashiriki harambee ya kanisa Akyeri Meru
Mbeya Yetu: LOWASSA ACHANGIA MILIONI 10 KANISA LA EAGT TUNDUMA MBEYA
Lowassa ajiweka mbali na kampeni Arumeru,ajikita kanisani..
Msamaa.
LOWASSA AMWAGIA FEDHA KANISANI ~ Mwanafasihi Mahiri
Lowassa kuongoza Harambee ya Kanisa Nyakato Mwanza | Fikra Pevu | Kisima cha busara!
MH. LOWASSA AONGOZA HARAMBEE YA KUNUNUA BASI LA KWAYA LA KANISA LA KKKT,MSASANI JIJINI DAR ~ Father Kidevu
WAZIRI MKUU AWAMU YA NNE ACHANGISHA SH100 KANISANI DAR ES SALAAM. ~ JUMA MTANDA
habarimpya.com - Kanisa lazidi kumtumia Lowassa katika harambee
Lowassa aendesha harambee Kanisa la Moravian Mbezi Beach Dar | Blog ya habari Tanzania | Online Newspaper | Thehabari.com
Kutokana na haya ninapata maswali yafuatayo:
1. Je Mh. Lowassa, unatarajia kulipwa kura na WAKRISTO hao ambao unawasaidia kwa vihela hivyo?
2. Je huu si udini kwa kiongozi anayetarajia kugombea urais kutumia nyumba za ibada kupata umaarufu wa kisiasa?
3. Je haya yangefanywa na mwanasiasa asiye wa chama tawala ingezua mjadala gani?
Let us call a spade a spade. Kama ni UDINI tuuite UDINI bila kujali mtu huyo ni wa chama gani.
Hivi hakuna msikiti aliyochangia kweli? tukumbushane