Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,353
- 26,194
Kumdharau mtu si lazima kumwambia maneno au kumfanyia matendo ya kejeli. Hata kumlaghai kwa utapeli,propaganda na uongo ni kumdharau. CCM,acheni kutudharau,kwani mnatuonaje?
Wakati ule mlitutangazia kuwavua gamba Lowassa,Chenge na Rostam. Lakini,hakukuwa na jambo hilo kwao wala kwa wanachama wengine. Kimsingi,hakukuwa na kuvuana gamba ndani ya CCM hadi Lowassa alipohamia CHADEMA. Kwani mnatuonaje?
CCM imekuwa madarakani,kwa kuunda Serikali,kwa miaka yote tangu Tanzania ipate uhuru. Kama ni sheria na mikataba mibovu imesababishwa na CCM na mfumo wake. Wakosoaji wa tangu mwanzo sasa wanasemwa ni wasaliti. Hakika,mngekubali kukosolewa tangu wakati huo mambo yasingekuwa yalivyo sasa. Kwani mnatuonaje?
Rais Magufuli na Serikali yake wanafanya mapinduzi makubwa katika utawala wa nchi. Katika uchumi,siasa na utamaduni anafanya awezalo katika kuboresha na kuendeleza nchi yetu. Kwakuwa CCM ndiyo mzazi wa matatizo yote 'yanayoshughulikiwa' sasa na Serikali,mnapata wapi ujasiri wa kujivunia yanayotendwa sasa?
Siasa za ulaghai,utapeli na propaganda zimepitwa na wakati. Tanzania yahitaji maendeleo. Kutuambia na kututendea mazingaombwe si vyema. Kwani mnatuonaje? Acheni dhereu!