CCM: Harambee ya kukiendeleza Chama 2015

CCM: Harambee ya kukiendeleza Chama 2015

Akiwa ziarani Iringa katika mkakati wa kueneza chama kwa kutembeza picha ya Mwenyekiti wa Chama Jk pamoja na Bendera

Ametumia mkutano kutoa tamko alilolitangaza kwa hisia kali kwa Wapinzani kutoka bungeni wakati ni kodi zetu zinawaweka pale akadai inauma sana.

Katika mkutano huo vijana wa Green guard wameonekana wakiwa wamevaa mavazi ya chama yenye naksi kama ya jeshi viongozi wa ngazi za juu mabegani, kofia na mikanda ya mfukoni. Kama yale aliyoonekana mhe. Mwingulu amevalia akikagua. Wakati wa mjadala wa Red vs Green Guard or CCM vs CHADEMA Ulinzi wakati Tendwa ana masaa kama si week au mwenzi astaafu akitishia kufuta CHAMA. Jamani tumetoka mbali nirudi kwenye hoja.
AMEELAANI WAPINZANI KUTOKA BUNGENI sasa chama chake IRINGA kinatembeza picha ya JK na Bendera kwa watu wa Iringa hii program ikoje imenishangaza Iringa hawaijui na kweli watu walijitokeza. Jamani Tanzania!!!

Naomba kutoa Hoja Mheshimiwa ili Jamvi lijadili tamko hilo na mengineyo tuelimishane kama walistahili laana pia tushauriane,nk.
 
yetu macho,hzo mbio zitaisha,watahangaika sana hao,
 
Akiwa ziarani Iringa katika mkakati wa kueneza chama kwa kutembeza picha ya Mwenyekiti wa Chama Jk pamoja na Bendera

Ametumia mkutano kutoa tamko alilolitangaza kwa hisia kali kwa Wapinzani kutoka bungeni wakati ni kodi zetu zinawaweka pale akadai inauma sana.

Katika mkutano huo vijana wa Green guard wameonekana wakiwa wamevaa mavazi yenye ngazi za juu za kijeshi mabegani, kofia na mikanda ya mfukoni. Kama ile aliyoonekana Mwingulu amevalia akikagua

Source pia ITV

Naomba kutoa Hoja Mheshimiwa Spika ili Jamvi lijadili tamko hilo na mengineyo tuelimishane kama walistahili laana pia tushauriane,nk.

Ukitoa tu kile kipengele cha kinafiki cha Nape kudai CCM wana uchungu sana na kodi zetu na kuwa wapinzani wanzitumia vibaya kwa kususia vikao vya bunge, mimi nadhani ni halali kwao kuanzisha mbio zozote wanazotaka. Naamini watkimbiza kila kitu mwaka huu na ujao. Ila wazingatie kuwa Watanzania wamechoshwa sana na unafiki, wamechoshwa na maisha duni, wamechoshwa na ufisadi na wanataka MABADILIKO!

Vinginevyo sitaki kusikia CCM inadai uchungu na kodi wakati mpaka sasa inalea watuhumiwa ambao imeshindwa kuwa na ujasiri wa kuwawajibisha. Otherwise wao wakimbize kila wanachojisikia kukimbiza.
 
Hivi hiki chama kina mwenyekiti..mbona kinafanya mambo ya kizoba zoba sana
 
Mlizowaibia wananchi hazijawatosha?naona waitaliano wamekamata meli yenu yenye mzigo wa billioni 123.wameshawashtukia na lazima sasa nape,kinana,mwigulu mpige magoti muombe michango.pambafu kabisa!!
 
sasa hivi ccm mkoa wa iringa wameanzisha kitu kinachoitwa upepelushaji bendera ya ccm mkoa mzima wa iringa. Wanasema kuwa lengo hasa la kupepelusha bendera(1)kuwaeleza wananchi utekelezaji wa ilani ya chama(2)kueneza chama(3)kupata wanachama wapya na ufuatiliaji wa maendeleo ya chama. Sasa mimi najiuliza!!! kuwa kama wao ni chama tawala kwani maendeleo hadi watu uwambie. maendeo siyanaoneka yenyewe? Kama ni kupata wanachama wapya. Wao sihuwa wa nasema ccm ipo imala, kila kona ya tanzania? Kama ni kukimbiza bendera kwani mwenge unaozunguka nchi zima hautoshi?.
 
Labda mafisadi, wengine hawa wanangojea kanga, kofia, fulana na mshiko. Si mlishawafundisha.
 
huu ndo muda wao wa kutakatisha fedha za unga,na tangu lini watanzania wakakichangia chama kilichodumaza maisha yao kwa zaidi ya miaka 50? watanzania wanasubiri kanga,vitenge,kofia, bendera zile kubwa wazifanye mashuka,tshirt na vilemba vya kijani maana hiyo ndo chenji ya kodi zao.me binafsi nawashauri wasiwapotezee watz muda wao maana hata mwenge tu ni janga kwa taifa hili.HADI KUFIKIA 2015 TUTAONA MENGI KABLA MAREHEMU HAJAKATA ROHO.R.I.P CCM
 
walianza na ngonjera za KUVUANA MAGAMBA, zimepita sasa wamekuja na maigizo ya bendera,magamba mtaacha lini sanaa za maonesho? nawashauri mtekeleze tu ahadi yenu ya maisha bora kwa kila mtanzania otherwise mnapoteza muda na 2015 tutawagonga tu
 
Ndugu wanajamvi naomba maoni yenu kuhusu kulazimishwa kuchangia gharama za kuendesha moja ya jumuia ya CCM. Nimefikia hatua hii baada ya kuona matukio ya uhalifu yanaongezeka, lakini Policcm wamejikita sana na wapinzani. Kuna umuhimu gani kukatwa kodi kuchangia hawa wachovu, badala ya Lumumba kuingia gharama?
 
Hata ningeambiwa nitalipwa nipige picha na kiongozi wa CCM, sitaki maana nikujitia unajisi.
Tehe tehe teheee umeniua mtu wangu.Huo Nchango angepewa kwanza huyu mwandishi wa barua akasome aboreshe kingereza yake mbofu mbofu ili akitoa andiko lingine liweze kuwa na mwonekano mwingine.Mie na inglishi yangu mbaya ya Uhandisi namzidi lol!
Kutembeza bakuli kuubwa na wizi wote wanaoufanya serikalini,kwen ye mashirika ya uma ,watu binafsi,wauza unga,wafanya biashara haramu kama kktb wao aka DENTIST wa tembo nia aibu ya milele!
 
Ukiona wanafanya harambee kaa ukijua kuna peza zimechotwa mahali wanasema ili wapate njia ya kuhalalisha matumizi yake.
 
Chama chetu hakikuwa na haja.Haja ya kuzunguka nchi nzima na 'kukitangaza' chama sasa. Haikuwa na haja ya hadi kumkodi Balozi wa China kunogeshga mikutano ya chama inayoongozwa na Katibu Mkuu Kanali Mstaafu Abdurahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye. Haja haikuwepo.Tulikuwa wapi miaka yote ya utawala wetu wa miaka 52 sasa?

CCM yetu haikuwa na haja ya kushangilia kupokea makada toka vyama vingine.Watanzania walioongozwa na CCM tangu 1977 (ikichukua mikoba ya TANU-Tanganyika na ASP-Zanzibar) hawawezi kuielewa CCM sasa. Hawadanganyiki na mikutano ya sasa ya CCM,iwe ya hadhara au ya siri. CCM imechezea bahati yake.Bahati ya kuaminiwa.Ya kuonwa kama chama kisicho na mbadala. Bahati ya kuganda mioyoni mwa watanzania maskini wengi wakiwa wakulima na wafanyakazi.

CCM haikuwahi kuwa na upinzani wa maana kwa miaka mingi.Kama chama kikabweteka.Sasa kinatapatapa.Hakukuwa na haja hiyo sasa kama chama kingejiandaa kabla. Watanzania wa sasa hawafuatilii mikutano ya CCM na kuiona kama sehemu ya maisha yao-kama zamani. Mambo yamebadilika. CCM haina haja ya kujaa hasira,visa na hujuma. Ni muda wa kufunzwa na watanzania.Kufunzwa siasa za ushindani.

Watanzania sasa wanazidi kuungana juu ya uandikaji wa Katiba mpya.CCM haikuwa na haja ya kuwapinga.Ilipaswa au inapaswa kuungana nao na kuyaishi maamuzi ya watanzania. Suala hili la Katiba mpya halina haja ya kulipuuza na kuliletea propaganda. Hakuna haja kung'ang'ania hoja zinazosadifu 'u-conservative' wa chama.Mazoea. Kunoga kwa madaraka. Uandikaji wa Katiba mpya Tanzania ni upepo mkali wa kisiasa usiozuilika na CCM. Kuuzuia ni kupeperushwa nao. Hakuna haja ya kutafuta makuu.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Last edited by a moderator:

Ni kweli bwana tupa tupa wambie hawa wanaofanya chama dume kama walishindwa kutengeza chama kabla nyerere hajafa wataweza saiz wakati chama kimeshaoza jumla?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom