Goodrich
JF-Expert Member
- Jan 29, 2012
- 2,091
- 1,179
Hali ni mbaya upande wa ccm baada ya hila zake za kuchakachua rasimu ya katiba iliyowasiliswa na Tume ya Jaji Joseph Warioba kubainika.
Kazi ya BMK ilikuwa ni kujadili namna ya kutekeleza maoni ya wananchi na sio kuyakataa na kuja na rasimu mpya.
Imebainika kwamba kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba, 2012, waliojitoa kwenye bunge maalumu la katiba ni ccm kutokana na uamuzi wao wa kuachana na rasimu iliyowasilishwa na Tume na kuamua kujadili rasimu iliyowasilishwa na kikundi fulani cha ccm kinyume cha sheria ya mabadiliko ya katiba.
Aidha kauli za baadhi ya makada wa ccm ambao wameonyesha kukerwa na hila hizi na kuweka wazi kuwa itakuwa ngumu katiba kupatikana bila UKAWA, kauli ya msajili kuwataka ccm warejee kwenye rasimu ya warioba, na ukimya wa walioandaa rasimu ya ccm vinaashiria hali ni mbaya ndani ya ccm.
Hivi sasa kuna mnyukano ndani ya ccm ambapo wakongwe wanadai hakukuwa na haja ya kuigharimu nchi kwa kuanzisha mchakato wa katiba na mwisho wa siku kuyakataa maoni ya wananchi.
Wengine wamehoji itakuwaje Rais wa Muungano akiwa Mzanzibari, maana Zanzibar itakuwa na Marais wawili, na Tanganyika itakuwa haina Rais hasa ikizingatiwa kuwa nafasi za umakamu hazina nguvu yoyote kikatiba wala kisheria.
NB
Tujadili bila kuweka ushabiki wala itikadi.
Hili ni suala la kitaifa.