CCM haiwezi kuanguka katika uchaguzi mkuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM haiwezi kuanguka katika uchaguzi mkuu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, Jun 6, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Pius Msekwa amesema chama hicho hakiwezi kushindwa katika uchaguzi mkuu ujao kwa kuwa ni sawa na mto Rufiji ambao hauwezi kukauka.

  Alifafanua mto Rufiji, hauwezi kukauka kutokana na mtu au watu wachache kuchota maji yake kwa lengo la kuukausha.

  Msekwa alitoa kauli hiyo, kutokana na kuwepo taarifa za baadhi ya wabunge wachache wanaotishia kukihama chama hicho baada ya bunge kuvunjwa.

  Msekwa alisema hayo jana akijibu swali aliloulizwa na waandishi wa habari katika mkutano wake na waandishi uliofanyika ofisi ndogo za chama hicho kwa lengo la kutangaza rasmi tarehe ya kuchukua fomu kwa wanachama wa chama hicho wanaotaka kugombea kuteuliwa katika nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar na kwamba shughuli hiyo, inatarajiwa kufanyika Juni 21 hadi Julai 1 mwaka huu.

  Msekwa alisema chama hicho, hakihofii vitisho hivyo na mbunge yeyote mwenye nia ya kukikimbia chama hicho baada ya bunge kuvunjwa hawezi kusababisha madhara yoyote kwa sababu CCM ina wanachama wa kutosha kukipa ushindi katika chaguzi ujao.

  “Chama chetu hakitetereki, kama kuna hayo mliyouliza ya kukimbiwa na viongozi wetu, hii ni kwa sababu mwaka 2005 waliondoka watu muhimu kama Njelu Kasaka, lakini hatukutetereka na alirudi kundini na chama kinaendelea kama kawaida,’’ alifafanua Msekwa.

  Alisema watu wengi maarufu waliondoka katika chama hicho akiwemo aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu, Agustino Mrema na kujipatia maarufu na wanachama wengi, lakini chama hicho hakikuyumba.

  Akizungumzia kuhusu wagombea wa nafasi hiyo, Msekwa aliwataka kuwa na busara ya kujichunguza wenyewe kama wanakubalika ndipo waende kuchukua fomu za kugombea kuteuliwa nafasi hizo.

  Alisema gharama za fomu hizo ni Sh 1milioni kwa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano na kwamba zitatolewa na kurudishwa kwa katibu mkuu wa chama hicho makao makuu ya chama yaliyopo Dodoma na wale watakaochukua fomu kwa ajili ya nafasi ya Rais kwa Zanzibar wanatakiwa kuchukua na kuzirejesha fomu hizo kwa Naibu Katibu Mkuu, ofisi ya chama hicho zilizopo Kisiwa Ndui Zanzibar.

  Alisema baada ya kukamilika kwa kurejeshwa fomu hizo kuanzia Julai 2 hadi 8, mwaka huu, wagombea wa nafasi hiyo, wataanza kazi ya kutafuta wadhamini na upande wa muungano anatakiwa kuwa na wadhamini katika mikoa isiyopungua 10 na miwili kati ya hiyo inatakiwa iwe kutoka Unguja na mwingine Pemba.

  Msekwa alisema kwa mgombea wa Zanzibar atatakiwa kuwa na wadhamini katika mikoa isiyopungua mitatu, angalau mkoa mmoja kutoka Pemba, lakini hakuna kizuizi kwa wagombea hao, Bara na Visiwani katika kutafuta wagombea katika mikoa yote 26 ya Tanzania.

  Msekwa alisema shughuli hiyo ya kuteua jina la kukiwakilisha chama hicho kwa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itafanyika Julai 10 katika mkutano mkuu wa chama hicho na kwa upande wa Rais wa Zanzibar itatangazwa Julai 9, mwaka huu na Halmashauri Kuu yaTaifa.

  Alisema watakaogombea udiwani katika kata mpya zaidi ya 700 watachukua fomu kwa makatibu wakuu wa kata za zamani.

  CCM haiwezi kuanguka katika uchaguzi mkuu
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,649
  Likes Received: 82,382
  Trophy Points: 280
  They know that there are so many illegal activities they could do during the coming genaral election under the watchful eyes of `vyombo vya dola` in order to stay in power for another term. Kigumu chama cha mafisadi! Kigumu.
   
 3. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  BAK........Kwa jinsi nionavyo mimi kwa aina ya opposition tuliyonayo Tanzania ni vigumu kwa CCM kuanguka katika uchaguzi hata kama hawatatumia hizo unazoziita mbinu chafu....Tanzania upinzani ni dhaifu mnoooo,na hakuna umoja miongoni mwa wapinzani....kuna upinzani ndani ya upinzani kitu ambacho kitaifanya CCM iendelee kupeta tu kileleni.......

  Kwa mfano ukiangalia haraka haraka utaona kufuatia kuibuka kwa CCJ baadhi ya vyama vya upinzani vimeanza kuangalia namna ya kupambana na CCJ na kupunguza mapambano dhidi ya CCM kitu ambacho ni faida kwa CCM.........So tusitegemee eti CCM itaanguka kirahisi kwa aina ya upinzani iliyopo...CCM ni wajanja na wanajitahidi sana katika kupanga mikakati ya ushindi(kampeni) na ndo maana wameanza mapema kwa kuanzia na kampeni ya uchangiaji wa fedha za kampeni wakiwatumia wasanii na watu maarufu Tanzania(Celebrities) kuwhamasisha wananchi kuichangia,uhamasishaji huu unafanyika kwa njia ya TV,Radio,magazeti,Tovuti na Blogs mbalimbali na mabango ya mitaani.......Hii si tu itawasaidia kulamba fedha bali pia ni mtaji tosha wa kura katika uchaguzi mkuu maana inawafanya wajulikane na kujipeleka karibu kwa wananchi.......Wakati CCM wanafanya hivi wengi wa wapinzani wao wamelala(sijui wanawaza na kusubiri nini)........Ifikie kipindi nao wabadilike na kuanza kupambana na CCM kwa kila hali(ng'adu kwa ng'adu style)......

  CCM ni wazuri sana kwenye kufanya kampeni kitu ambacho kinawasaidia kuvuna kura kutoka kwa wananchi...........


  Ni hayo tu...........
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,649
  Likes Received: 82,382
  Trophy Points: 280
  Bala, CCM yenyewe haiko imara kuna makundi ndani ya chama hicho ambapo kundi lingine linafanya juu chini kuwaangusha wale wa kundi pinzani.... na hata katika baadhi ya majimbo kuna chuki za kutisha na mapesa chungu nzima yamemwaga na kundi moja ili kumshinda mgombea wa kundi adui. Hali hii inaonyesha dhahiri kwamba hata CCM si imara kabisa.

  Utendaji wa CCM katika awamu inayoisha umekuwa ni mbovu sana hawakuweza kutimiza hata ahadi yao moja waliyoitoa. Kumbuka ahadi za "Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana" "Ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya" sasa hivi hata kuzitaja hawathubutu kuzitaja. Ingekuwa nchi nyingine basi uchaguzi unaokuja CCM ingepoteza viti vingi bungeni kutokana na Wananchi kutoridhika na utendaji wa CCM katika awamu inayokwisha, lakini si Tanzania.

  Wao wenyewe CCM hawajiamini ndiyo maana itabidi watumie mbinu chafu mbali mbali zikiwemo za kuwahonga wapiga kura kwa matandiko, vyakula na mafulana yao ya njano na kijani, kutumia vyombo vya dola kuwanyanyasa viongozi wa upinzani na wanachama wao na hata kuwapiga na hili limeshatokea katika chaguzi za siku za nyuma.

  Nakubaliana nawe kwamba vyama vya upinzani ni dhaifu na wao pia wanastahili kulaumiwa kwa kuweka ubinafsi mbele na kukataa kata kata kuungana ili kuunda chama kimoja chenye nguvu, lakini hili pia ni gumu maana katika vyama hivyo CCM imepandikiza mamluki ambao inawatumia katika kuvidhhofisha vyama vya upinzani. Mfano ni Mrema wa TLP. Huyu bwana sasa hivi alitakiwa awe mstari wa mbele kuandaa chama chake katika uchaguzi ujao na kutafuta wagombea wa ubunge katika majimbo mbali mbali nchini, lakini yuko busy kumpigia debe Kikwete na kumtetea kila kunapokuwa na habari ambazo si nzuri kwa Kikwete ninaamini kabisa si ajabu hata ndani ya CHADEMA, NCCR nako kuna mamluki waliopandikizwa na CCM ili kuhakikisha vyama hivyo vinaendelea kuwa dhaifu miaka nenda miaka rudi.

  Pia sikubaliani nawe unaposema kwamba CCM ni wazuri sana katika kufanya kampeni. Nasema hivi kwa sababu CCM inatumia mbinu chafu nilizozitaja hapo juu ili kufanikisha kampeni zao. Kama wangekuwa wazuri katika kufanya kampeni badala ya kutumia mbinu chafu basi kwanza wangeanza kuwaeleza Watanzania mafanikio yao katika ahadi walizotoa katika kampeni za 2005 zikiwemo ahadi za "Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana", "Ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya" n.k. lakini kwa kuwa wanajua wamevurunda katika ahadi zao basi itabidi watumie mbinu chafu ili kuhakikisha ushindi mwingine wa kishindo. Na kutokana na wapiga kura wengi kutokuwa na uwezo wa kuona mbali basi wakinunuliwa kwa tonge chache za pilau, kilo chache za mchele na unga, matandiko, Baiskeli, fulana za njano na kijani na vijisenti vichache basi watawapigia kura CCM kwa idadi kubwa sana. Kwangu mimi hali hii huwezi kabisa ukawaita CCM ni wazuri sana kwenye kufanya kampeni.

  NB: Only few days to go before the start of World Cup....:A S soccer:

  Jumapili njema
   
 5. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Wapinzani inaelekea wapo wapo tu ili kupata RUZUKU basi halafu watu kama Zitto eti wanaota kuwa baada ya November kutakuwa na new polical dispensation Tanzania!! What a joke ; huyo huyo Zitto anawapiga vita wenzie Chadema huko Kigoma kwasababu tu ya personal relationship yake na Kafulila halafu ndio utegee kuingusha CCM?
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,649
  Likes Received: 82,382
  Trophy Points: 280
  Kwa lipi ambalo CCM imefanya inastahili kuchaguliwa? Kwa maoni yangu hakuna.... ni upumbavu tu wa wapiga kura waliokuwa wengi kuendelea kuwapigia kura CCM miaka nenda miaka rudi na mbinu chafu zinazotumiwa na CCM, ubinafsi wa vyama vya upinzani na mamluki waliopandikizwa katika vyama hivyo. Kama Wananchi wangekuwa wanatafakari mambo kwa kina basi CCM inastahili kabisa kupoteza viti vingi bungeni...lakini Wapiga kuwa wa Tanzania NDIVYO WALIVYO! CCM hata ivurunde vipi bado watawapiguia kura, CCM wenyewe watatumia mbinu chafu zote na huku NEC imeangalia pembeni na hatimaye kushinda tena kwa ushindi wa kishindo na kujiona wao ni nambari one.
   
 7. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Mwaka huundiyo ingekuwa rahisi kuiondoa CCM kwani kiongozi wake bwana "Mrisho Mpoto" ni kiongozi dhaifu mno, na ni rahisi sana kumshinda kwa hoja mkijipanga...huko baadae huwezi jua labda CCM wasirudie tena kumpa nafasi kiongozi mbovu kama huyu bwana "Mpoto"
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Jun 6, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,649
  Likes Received: 82,382
  Trophy Points: 280
  Hata bunge la CCM ni dhaifu mno limeshindwa kabisa kuwajibika katika mambo mengi ambayo yana maslahi makubwa kwa Watanzania.
   
Loading...