CCM haitakufa na itaongoza milele: Nape Nnauye

acheni kutafsiri hoja hii kinyume na fikra za Nape, yeye kaongelea chama na wewe unaleta habari zako za kilokole na kumuhusisha mungu moja kwa moja na siasa, maana ya Nape ni hakuna Tanzania bila ya CCM na ndio umilele wenyewe. Pia swala la kilio cha watanzania hilo labda bado unalo wewe sisi wengine tunatumia mfumo huu wa maneno "SEE -JUDGE -ACT" na hatuna muda wa kulia eeh mungu tusaidie bali tuna muda wa kueneza sera na kushawishi wananchi juu ya mabadiliko wanayohitaji yanaweza kupatikana kupitia kwa viongozi machachali wasiojali kingine ila maslahi ya umma.


Neno milele huwezi kulitenganisha na dini, na katika vitabu vyote vitakatifu limeongelewa sana hilo.
Nape kalitoa huko huko kwa walokole.
Nape, zilikuwepo dola imara sana kama ya warumi, leo hata chembe ya nguvu yake haipo.
Ushauri kwako kama mkristo mwenzio, unapofanya hizi propaganda za kidunia, usihusishe utani wako na Mungu!
Yeye si mwanadamu hata aweze kutaniwa!!
 
Sina hakika na statement hii kama kweli nape kajanayo, lakini ninaamini dogo dishi limeyumba kiasi cha kukosa uhuru, na finally kashindwa kuwa objective, na wajibu wake kama k/tibu mwenezi siyo huo, wa mara kamjibu lowasa, mala hili nadhani issue kwake sasa ni kusutwa moyoni kwa ufisadi alionao

Nape anahitaji mshauri, hajajua majukumu yake kama katibu wa uenezi, nilitegemea awe ana jenga daraja kati ya Chama chake na wasio wa chama chake, anachofanya yeye ni kurusha vijembe na kuzidi kuwafanya watu waichukie CCM , jaribu kusoma post zake face book, ziko so annoying and irritating, sijui publicity aliisomea wapi? Lini uliwahi kuona mtu wa publicity wa kiwanda cha bia akiwatukana wanywa soda? anachofanya ni kuwavuta nao wanywe bia, ukweli CCM waliingia chaka.
 
Sample ya vijana kama Nape na Zitto ndio wanaotuaibisha ktk jamii sisi vijana wenzao, kwani wana akili kama kuku.
NI VIJANA MBUMBUMBU.
Kumchanganya Zitto na Nape hapo natilia shaka uwezo wako yawezekana huo 'ukuku' unaouzungumzia unakuhusu wewe binafsi.
 
Nappe amesema CCM haitakuja kufa na itaongoza milele.

Ameitoa kauli hiyo kufuatia kauli zilizotamkwa na wazee 3 ambao ni Butiku, Kitine na mzee Kaduma waliosema kuwa CCM inakaribia kufa bin kutokomea.

Source: ITV taarifa ya habari saa mbili jioni ya leo
Hilo ndio tatizo la viongozi wa ccm kuamini kwamba wako imara na watatawala maisha yote, lakini ukweli ni kwamba chama kiko hoi kinaelekea kuzimu kwa tuhuma za ufisadi, uchu wa madaraka na mitandao.
 
haijawahi mahututi akaambiwa kuwa atakufa.
nape angeingia kwenye kitabu cha jinesi kuwa binadamu wa kwanza kumtakia marehemu kuwa ni lazima afe.
 
Nape kuna wtu wa kujibiwa lakini kuna watu wakati wa kuwjibu inabidi ufanye tathmini sana kwa kuwa kuna watu kauri zao ni Genuine na kuna watu kauri zao ni pumba.

Ninavyojua binafsi kama majibu yake ni dhidi ya Wazee hao ukweli ni kuwa atakuwa amejibu kama kujikosha na si ukweli kama dhamira ya wazee hao wanavyoiona CCM kwa kuwa wazee hao wameijenga CCM wakishirikiana na baba yake hivyo wanaijua ilikotoka kuliko Nape na mwenyekiti wake wanvyoijua leo hiii.

Nape punguza kukulupuka na majibu mwangalie mtoa kauri anadhamana gani katika umma wa kawaida kabisa.

Brother Nape usitukane mamba kabla hujavuka mto. CCM ina wenyewe angalia yaliyokukuta 2010 yanaweza kukuta 2015 usijivunie jino bovu halitakusaidia kula nyama. Watakutumia halafu wakutupe kama.......
 
Milele manaake hakuna mwanzo wala mwisho, yaani CCM ni Mungu wake! Uarabuni angepigwa mawe mpaka afe, kufuru kubwa saana hiyo!

Huyu kijana ana laana ya baba yake na ndio maana anazungumza hovyo!! Mwisho wake utakuwa mbaya na atakuja juta kwani hata hao wafadhili wake hatawaona!
 
Sample ya vijana kama Nape na Zitto ndio wanaotuaibisha ktk jamii sisi vijana wenzao, kwani wana akili kama kuku.
NI VIJANA MBUMBUMBU.

Ni wanafiki wa kutupwa. Wanatetea wasichokiamini. Ogopa watu wa design hii
 
Sidhani kama alimaanisha kukisema kilicho moyoni mwake,na nafikiri aliongea domo lake likiwa linatetemeka na pasipokujiamini.
 
Nape, usikubali kurubuniwa akili zako, ujana wako na malengo yako ya baadae kwa kuficha ukweli na kukumbatia uongo kuficha ukweli kwa kusema kile usichokiamini. Nachotaka kukuambia hapa ni kwamba hao wazee ni wakongwe na wameona mbali sana zaidi yako wewe na mimi. Walikuwa na mapenzi mema sana na CCM, hivyo leo kutamka maneno kama hayo si kwamba wanapiga zogo au kampeni, lahasha wameona kwa miaka hii ya hivi karibuni CCM imepoteza dira na weledi kama chama kongwe hapa Nchini.

Yale malengo na misingi yake inayotokana na Ilani ya chama zimekiukwa kabisa,na wale waliotegemewa kuiongoza ndiyo hao wa kwanza kusimama majukwaani na kuwakashfu watu, viongozi wamekiuka maadili yaliyoachwa na wasisi na viongozi waanzilishi. Mfano mdogo tu, Kuna haja gani leo ccm itumie nguvu nyingi, hila, uongo, oenevu, matusi, nguvu ya dola na pesa nyingi za walala hoi walipa kodi katika kujibizana na kutunishiana misuli katika kushindania kile kigoda/kiti cha ubunge kule Arumeru? Yale tuliyoahidiwa kule Igunga yametimizwa?

Yale yaliyoahidiwa katika uchaguzi mkuu 2010 uliokuwa uwe mwisho wa CCM yametimizwa? Maisha bora yako wapi? Nguvu zaidi, kasi zaidi na hari zaidi tuliyoahidiwa katika uchaguzi wa 2010 ndiyo hizi za kutumia rasilimali zetu kujinufaisha wachache? Hivi ni CCM hii hii ambayo imeongoza nchi kwa miaka 50 leo inapigana na Chadema ambacho ni kama mjukuu???

Ukiachia hayo; wapo watu wengi sana wenye busara wanaoipenda, na waliopenda CCM lakini hali ya maisha ya watanzania ilivyo sasa, nao wameshapoteza mapezi na chama kabisa, CCM hihi imekuwa ya kuwafumbia macho watu waovu wanaotumia fedha walizozipata humuhumu kuhujumu, kudhoofisha hata kuua nafsi za wenzao kwa ajili ya uchu wa madaraka? Mnawajua, mnawaogopa na mmeshindwa kuwaondoa chamani kwa ajili ya nguvu ya pesa walizochuma.

Nakushauri sana ndugu yangu.. Elimu, malezi na busara ulizozipata kutoka kwa wazazi, waanzilishi na waasisi wa CCM zitumie vizuri ili zikufanye uheshimike na pia sisi vijana tusikuone kama mpiga kelele yaani vuvuzela. Kuwa makini na mpole kama nyoka, mwenye busara kama njiwa wakati unachambua mambo haya niliyokueleza. Mengi unayajua lakini umejengewa misingi ya kuficha uongo kwa katika kuwadhoofisha wanyonge.

Kumbuka CCM wanakutumia kama rubber stamp tu kuwavuta vijana lakini hawako tayari kuachia nafasi hizo kwa vijana. Ukweli unaujua kuwa kila chenye mwanzo huwa na mwisho, swali ni huo mwisho ambao mimi au wewe hatuujui utafikaje. Jua pia CCM ina mwisho, na haya yote unayoyaona kutoka Nchi jirani za Mali, syria, Libya Misri na kwingineko hayakuanza tu mara moja. Hali ya kuchoka, kukata tamaa ndyo hiyo inamfanya ni mtu anafika mahali anasema NA IWE MWISHO....

Na sisi vijana wapenda mabadiliko na maendeleo tutafika mahali tuseme TUMEFIKA MWISHO NA CCM. Huku kuchelewa kwetu si kwamba ni uoga ila tunapenda hii hali ambayo ccm imetufanya kama mbuzi wa shunghuli isiilete damu wala ushaha pale inabidi iwe ya machozi na majeruhi ambao tutakumbukwa kama mashujaa wa mapinduzi ya kweli kwa karne zijazo.Mtabakia na Aibu kwa kauli zenu zinazowafurahisha wachache mafisadi.

Labda nikukumbushe tu vitu vichache.
1. Ni kwanini leo Tanzania hamna umeme wa kuaminika angalau kama Kenya? utasema ni Mabwawa hayana maji, hatuna gasi asiliay, au makaay mawe, wataalamu au kitu gani kwa miaka50?

2.Ni kwa nini Vijana wengi uliomaliza nao vyuo vikuu, waliomaliza nyuma na wanaomaliza leo hawana uhakika wa kazi na wengine hawana kazi kabisa? Utasema ajira hamna au viwanda hamna, mashirika ya umma hayapo na ofisi za serikali zimejaa wenye sifa za kuongoza?

3. Kwa nini kila profesor wa chuo kikuu, madoctor na wakufunzi wengi wanapenda kuacha kazi zao za kufundisha wadogo zao au wanafunzi na wanakimbilia bungeni? Hapa nakuachia mwanya wa kutafakari.

4.Ni kwa nini rasilimali za kitanzania hazinufaishi watanzania ili hali ukijua kwamba kama ni watalaamu tunao? Yaani hadi watu kutoka UN wanashangaa lakini wewe na mimi tunashangilia kuvaa nguo za kijani na kofia tu.

Namalizia kwa kukuomba kwamba katika yote ufanyayo utaulizwa tu siku ya mwisho matumizi ya dhamana uliyopewa ulitumia kwa kuwafanyia nini hao waliokupa?? Angalia tusije kupita barabarani kuelekea kwenye shunghuli zetu tukapigwa mawe na watanzania ambao walituamini kuwa tungeweza kuwatumikia..

The changes in the economic foundation lead sooner or later to the transformation of the whole immense superstructure by Marxist
 
Siku moja Abunuwasi alinunua sufuria ndogo, halafu akaenda kuazima sufuria kubwa kwa jirani yake. Alipomrudishia akarudisha sufuria kubwa na ndogo. Jirani alipouliza kulikoni? Abunuwas akajibu sufuria yako imezaa.Siku nyingine akaazima tena. Safari hii hakurudisha Jirani alipohoji, Abunuwas akasema sufuria imekufa!!! Kwa sababu kila kinachozaliwa hufa!
 
Nampongeza Nape, kwani anajua ndani ya moyo wake kuwa yeye mwenyewe ana mchango mkubwa wa kuiua CCM, shauri zenu kama hamuelewi anachomaanisha!
Kesho ikifa na akasema mi nilishawaambia kuwa CCM ingekufa mtashangaa? Kijana ni mzuri sana wa kujigeuza katika maneno, mmesahau suala la kujivua gamba?
 
Nape anapoongelea c c m muangalie usoni huwa haamini yale anayosema kuhusu hiyo c c m huwa ni kinyume chake :flock:
 
Mwanamke aliyeachwa anaweza kurejewa, tena anaweza kujerewa kwa mapenzi makubwa sana, lakini titi la mama halirejewi, LO! hata ukizaliwa mara ya pili huwezi kulitamani tena asilani.

Ndivyo kilivyo chama cha Mapinduzi, kimekuwa kama titi la mama kwa watanzania,wamekikataa kabisa, hata kinapolazimisha kuwanyonyesha wanakikimbia.

Nikikumbuka zamani tulipokuwa bado wachanga, tulivyokipenda na kukitumikia, tukiimba kwa furaha na kukifurahia, Duniani kote sifa zake tukizielezea, kwa mapenzi makubwa CCM mama yetu tukimkumbatia, machozi ya hasira yananinyemelea kwa umasikini mkubwa kiliotuachia.

Nikufananishe na nini Chama cha Mapinduzi?
 
MMH mmh kweli watanzania tumekikoma CCM kama tulivyokoma kunyonya maziwa ya mama zetu
 
mtaji wa Nape huu hapa

[h=3]Kampeni Za CCM Arumeru Jana[/h]

[h=3]
[/h]
Msafara wa mgombea ubunge wa CCM jimbo la Arumeru MNashariki Sioi Sumariukitoka kwenye kambi ya CCM kwenda vijijini kwenye mikutano ya kampeni jana
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Arusha, Nameloki Sokoine akimuombea kura
mgombea wa CCM Sioi Sumari kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika
Kijiji cha Sing'isi,jana
Aliyekuwa mratibu na mhamasishaji wa kampeni za CHADEMA katika uchaguzi
mdogo Arumeru Mashariki, katika kijiji cha Singisi, Anna Silas akikabidhi
kadi ya chama hicho kwa Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka baada
ya kutangaza kujiunga na CCM katika mkutano wa kampeni ulofanyika jana
katika kijiji hicho. Wengine kutoka kulia ni Mwigulu Nchemba na Sioi
Mwigulu akionyesha kadi za TLP na ya CHADEMA alizokabidhiwa baada ya
aliyekuwa Katibu Mwenezi wa TLP Kata ya Seela Sing'isi, Augustine Kyungani
na aliyekuwa mratibu wa kampeni za CHADEMA Anna Silas kumkabidhi baada ya
kuhamia CCM kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha
Sing'isi jana
 
Nape anajigamba kwa sababu hii.

[h=3]Taswira Za Kampeni Za CCM Usa River[/h]

[h=1][/h]


7xx.JPG
Wazee wa Kijiji cha Lekitatu, Usa River wakifuatilia kwa makini mkutnao wa kampeni za CCM uliofanyika jana kwenye kijiji hicho
3.+Mwigulu+akisoma+waraka+aliodai+ni+wa+CHADEMA.jpg
Mratibu wa kampeni za CCM, Mwigulu Nchemba akisoma waraka kwenye mkutano wa kampeni Usa River, waraka huo inadaiwa ni wa CHADEMA wakikiri watashindwa uchaguzi wa Arumeru Mashariki

4.+Kibajaji+%2527akiichana+CHADEMA%2527+jukwaani.jpg

Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde akihutubia mkutano wa kampeni za CCM jana Uwanja wa Ngarasero, Usa River
1.Sioi+Ngarasero%252C+Usa+River.jpg

Mgombea wa CCM jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari akisalimia maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni uliofanyika jioni hii kwenye Uwanja wa Ngarosero, kata ya Usa River jimboni humo. Kushoto ni Mratibu wa kampeni za CCM, Katibu wa NEC Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba.
2.Sioi+Ngarasero%252C+Usa+River.jpg

Mgombea wa CCM, jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari akipungia mikono maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano huo. Mbele yake (kushoto) ni Mbunge wa Mtera Joseph Lusinde
2.+Umati+wa+watu+waliohudhuria+mkutano+wa+CCM%252C+Usa+River+jana.jpg

Umati wa watu waliofurika mkutano wa kampeni za CCM, Uwanja wa Ngarasero, Usa River,janaPicha na Bashir Nkromo-Arumeru
 
Back
Top Bottom