CCM, CUF Pemba kimeeleweka vitambulisho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM, CUF Pemba kimeeleweka vitambulisho

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Aug 17, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF), Ofisi ya Usajili wa Vitambulisho vya Mzanzibari Mkazi, zimekubaliana kubadili utaratibu wa uandikishaji wa vitambulisho na sasa utafanyika shehia kwa shehia na kwa tarehe maalumu kuanzia Jumatatu ijayo.

  Hatua hiyo inatokana na utaratibu wa awali ambao uliwalazimu wananchi baada ya kuchukua fomu katika shehia zao kufika ofisi ya Mkuu wa Wilaya, ambako walikuwa wakipata vitambulisho hivyo.

  Akizungumza jana mjini hapa, Ofisa Tawala wa Wilaya ya Wete, Khamis Juma Silima, alisema makubaliano hayo yalifikiwa juzi kwenye kikao kilichofanyika ofisini kwa Mkuu wa Wilaya na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa CUF, Khalifa Mohammed Issa na Kaimu Katibu wa CUF wa Wilaya, Haidary Ali Abdallah.

  Wengine waliohudhuria ni Katibu wa CCM wa Wilaya, Said Abdallah Suluhu na Mhazini wa CCM, Ramadhan Issa Kipaya na Mkuu wa Idara ya Vitambulisho Pemba, Hamad Shamata Hamad.

  Watakaohusika kujiandikisha ni wenye vyeti vya kuzaliwa, na wakishapata vitambulisho hivyo watajiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, ambalo uandikishaji wake umesitishwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutokana na vurugu zilizojitokeza wakati wa uandikishaji.

  Kulingana na ratiba hiyo, inaonesha kuwa Jumatano na Jumanne wiki ijayo uandikishaji utafanyika shehia za Kambini na Kiuyu Minungwini, wakati siku mbili zinazofuata itakuwa Kiuyu Kigongoni na Ole. Agosti 21 na 22 itakuwa Mjini Ole na Kangani, wakati siku mbili baadaye itakuwa Piki na Mzambarauni Takao, huku Agosti 26 na 27 itakuwa Mtambwe Kusini na Kaskazini.

  Agosti 28 na 29 itakuwa Kisiwani na Limbani na Agosti 31 na Septemba mosi itakuwa Jadida na Kipangani, wakati Septemba 2 na 3, itakuwa Pandani na Selemu na siku mbili zitakazofuata itakuwa Utaani na Bopwe. Kwa mujibu wa ratiba, Septemba 7 na 8 itakuwa Kizimbani na Fundo, siku mbili zitakazofuata, itakuwa Gando na Ukunjwi, huku Junguni na Mchangamdogo ikiwa ni Septemba 11 na 12.

  Kulingana na ratiba hiyo, Maziwani na Kojani A itakuwa Septemba 14 na 15, ambapo siku mbili zitakazofuata, itakuwa Kiungoni na Pembeni, ambapo Shengejuu na Mpambani itakuwa Septemba 18 na 19 na shughuli hiyo itahitimishwa Septemba 25 na 26 kwa shehia za Chwale na Kinyikani.

  Hata hivyo licha ya ratiba hiyo, bado jana kulionekana baadhi ya wananchi wakiwa katika makundi wengine waking'ang'ania kutaka wapewe vitambulisho hivyo kwenye ofisi hiyo hiyo ya Mkuu wa Wilaya.

  Utaratibu wa awali ingawa ulikuwa mzuri, lakini ulipata upinzani kutoka kwa baadhi ya viongozi wa CUF waliodai una usumbufu mkubwa na kuzua zogo, kwamba baadhi ya wananchi wananyimwa fomu za kuandikishwa hasa wasiokuwa na vyeti vya kuzaliwa.

  Hata hivyo Jumanne wiki hii, akizungumza katika mkutano na viongozi wa kisiasa, masheha na baadhi ya watendaji wa Serikali, Mkurugenzi wa Idara ya Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi, Mohammed Juma Ame, aliwataka wasio na vyeti vya kuzaliwa waende mahakamani waape na kupewa fomu za kuandikishwa.

  Uandikishaji wa vitambulisho vya Mzanzibari Mkazi ulianza mwaka 2005, lakini baadhi ya wananchi walikuwa hawajitokezi kuchukua fomu kwa vile masuala ya Serikali yamekuwa hayapewi kipaumbele kisiwani hapa na hayaungwi mkono.

  Pemba asilimia kubwa ni wafuasi wa CUF. Lakini baada ya kutolewa tamko kwamba wasio na vitambulisho hawataingia kwenye Daftari, sasa mwamko umekuwa mkubwa, kila mtu akitaka kujiandikisha na kusababisha vurugu katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya, ambazo ndizo zinatoa vitambulisho, wakati shehia zinatoa fomu za kupata vitambulisho hivyo.

  http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=3192
   
 2. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  I note in the above story that, the requirement of getting ID'S was to produce Birth Certificate, ikimaanisha that is the only proof of citizenship inayotakiwa, to the contrary, viongozi wengine wenye uCUF wameshaanza kuwapa ushauri wanachi wasio na vyeti vya kuzaliwa waende Mahakamani to swear and get affidavit of authenticity, that huyu undocumented alien apewe haki ya kupiga kura kwa kupewa ID. Hapo ndipo utajuwa kuwa CUF kunamambo.

  If the agreement is already entered between CCM and Cuf, that, the only way for someone to obtain ID is to produce Birth Certificate, why then is it so hard for CUF-nites to understand that?

  Kaazi kweli kweli
   
 3. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  We unayezungumza tukifuatilia tutakuta kuwa baba yako mzazi hana cheti cha kuzaliwa. Iwapo atahitaji kujiandikisha, anyimwe haki hiyo kisa wakati anazaliwa vyeti vya kuzaliwa vilikuwa havitolewi? how many people in TZ bara hawana vyeti vya kuzaliwa? wote hao wanyimwe haki kwa vile hawakuandikishwa wakati wanazaliwa? Ndio maana kuna viapo vya mahakama kwa vile muda wa kutolewa vyeti ulishapita hivyo mhusika ni lazima aape mahakamani kuwa yeye ni mzaliwa wa mahali fulani na ikithibitika kuwa amedanganya mahakama, sheria kari zinachukuliwa juu yake. Kama kuna mtu anatilia shaka kiapo cha mtu fulani basi na apeleke ushahidi kuwa huyo mtu amedanganya na achukuliwe hatua kali. Kwa nini mnataka kufanya maisha ya wanachi kuwa machungu kwa ulevi wa ufisadi na madaraka?
   
 4. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Unajuwa yakhe kule kwetu mtu akifika kukwambia kwamba unazungumza (unaongea )kama vile mwanamume aliyepakatwa hapo ujuwe tayari umeshatolewa manani,sasa wewe kwa aliki zako ulizonazo nchi kama hii yaani Tanzania ingenerali na kama wewe kweli mtanzania hujuwi kuwa kuna wazazi wengi wanazalia majumbani na hata mambo ya kwenda hospitalini hayamo akili mwao ,sasa wanaposema mtu aende mahakamani ni sehemu ambayo kama ukithibitika umedanganya basi hapo tena wewe na sheria utakumbana nao kauli uliyotowa hapo juu umekuwa kama vile mtapta asiejuwa nini anakitafsiri.
   
 5. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160

  The above paragraph is very clear that those who are allowed to register and receive IDS are the only ones who have birth certificates.

  It is shame for such a simple sentence in bold becomes ambiguous to some people, while infact there is no any ambiguity in it, rather than deciding not to follow the mutual agreement entered between CCM and CUF, that 'ONLY THOSE WHO HAVE BIRTH CIRTIFICATE' are allowed to receive IDS.

  It is customerily and ethical for any one who don't have a birth cirtificate to use judical conduit in order to verify his/her citizenship, not only in Tanzania but it is a worldwide thing, and there are merits to support that. As such, CCM and CUF representative while knowingly and consciosuly decided not to allow and/or practice such tradition of verification of citizenship/birth for undisclosed reasons.

  It will be fair and it will reduce unnecessary war words if the tangible stipulation entered between CCM and CUF be disclosed to the public so that the pioneers can understand the reasons, and why did both parties refused to used traditional verification of birth, if someone does not have a birth certificate.

  .
   
  Last edited: Aug 17, 2009
 6. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mimi naomba tu amani.
   
 7. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #7
  Aug 17, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  umeeleweka!kwanin hii sheria ianzie tz visiwani?
   
 8. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Hawaaminiki. The laws comes when there are obstraction of justice.
   
 9. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #9
  Aug 18, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  CUF hawaachi visingizio. lakini naona safari hii Zan ID imewasakama wenyewe. Na tangalie game uwanjani.
   
 10. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #10
  Aug 18, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  CUF CUF CUF, hawa watu ni taaabu kweli kuishi nao. Wao kila kitu lazima walete shari.
   
 11. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #11
  Aug 19, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Si ni chama cha kidini na dini yao inaruhusu shari?
  Kama nasema uongo angalia jinsi wanavyolalamikia kila kitu.
   
 12. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #12
  Aug 19, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  naona unawatafuta watu kina Mwiba, Ngekewa, Junius, na wale wengine, haya bwana -sebu shari-lako pekeyo hilo.
   
 13. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #13
  Aug 19, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  We bana, acha kuniita kisebusebu. Mimi naitwa mchukia mafisadi.
  Mi nilishazoea shari hivyo siogopi tena shari hasa nisemapo ukweli.
  Kutosema ukweli ni jadi ya sisi m sasa akina mwiba, junius, ngekewa,na wewe, kama si sisim bila shaka mtanielewa:D

  Nimekoswa majambia toka kwa ndugu zangu leo nitaogopa nani?
   
 14. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #14
  Aug 19, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  Mchukia Fisadi hicho chama cha CUF Sio chama cha kidini la hasha Chama cha CUF ni chama cha wananchi wote na wapendao haki na Maendeleo sio Ufisadi jaribu kuelewa Vizuri Sera za Cuf na Mwenendo wake mimi sio mwanacha wa cuf wala CCM najaribu kukujuulisha kuwa sina chama chochote ninachokifuata na sio mbaguzi wa Dini yoyote ile iwe ya kiislam au ya Kikristo ninachotaka Haki na haki haiwezi kupatiakana mpaka kuwepo uongozi bora jaribu kuelewa Mkuu Mchukia Fisadi usilete chuki zako kama wewe ni Mwanachama wa CCm Au Wa Chama kingine jaribu kuwa Mvumilivu usilete uchochezi nchi yetu Tanzania ni nchi ya amani na yenye kuwa na uhuru wa kufuata au kupendelea Dini yoyote au chama chochote jaribu kuwa Mvumilivu ngojea wakati wa Uchaguzi umchague kiongozi mzuri sio kwa jina bali Anaefuata Uadilifu sio Ufisaadi upo na mimi Mkuu Mchukia Fisadi?
   
 15. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #15
  Aug 19, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Haki-Sawa- Kwa Nani?- Kwa wote!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 16. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #16
  Aug 19, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Samahani wakuu naomba mnisamehe. msinikasilikie tupo vitani. Mimi sio sisiM ni Chadema.
  Na kafu si kwamba nakichukia nakipenda ndio sababu pamoja na kutokuwa mwanachama wala mpenzi kura yangu alipewa mbunge wa kafu.
  Narudia tena nisameheni na tuendelee kupambana na adui yetu 'nambari wani'
   
 17. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #17
  Aug 20, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  Mchukia Fisadi Umesamehewa Tunachotaka sisi sio CCM,CUF,Chadema na vyama vingine kuleta mambo ya vurugu na kulumbana kusikokuwa na Maendeleo yoyote.Tunachotaka sisi ni Haki,usawa, umoja na Maendeleo yetu hata kama CCM au CUF itashinda au Chadema au chama chochote kile je tutakiangalia kinafanya nini katika kuikuza nchi yetu changa kimaendeleo na tumejawa sana na Umasikini njaa na Maradhi tunachotaka sisi wanachi ni kuondowa Umasikini njaa na Maradhi je hicho chama kitakachotawala kama kitaondowa hayo Matatizo sugu tuliyokuwa nayo Tangu tupate Uhuru kutoka kwa hao Waingereza?Je tutaweza kuyaondowa hayo Maradhi sugu kwetu? itabidi tuwaulize viongozi wetu wa Taifa hilo suala litaishia wapi?Sio ikifika wakati wa Kampeni ya uchaguzi utakuta kiongozi anayepigania kushinda katika Uchaguzi wa Chama ana ahidi mambo mengi tu lakini mkipa kura yeye ndio anakuwa Mfisadi mkuu je tutaendelea sisi Watanzania?Au tutakuwa kila siku tunawategemea Wafadhili watuletee misaada. Na hiyo misaada itakuwa mpaka lini tunaisubiri kutoka kwa Wafadhili?Je tutafika kule tulikokusudia kufika? au tutaishia njiani katika hiyo Safari yetu ndefu?tujiulize Watanzania tutakuwa Masikini mpaka lini?Ukiangalia nchi yetu ina neema sana tuna mito mikubwa,Maziwa tunayo lakini maji mazuri hatuna? hatuna Umeme ukiangalia hapo DSM kuna sehemu zingine umeme hakuna au hata ukiwepo basi utakuwa umeme wa muda au wa mgawo?tuna ardhi nzuri lakini ukiangalia sehemu kubwa ya watu hukimbilia mijini kutafuta kazi na kijijini watu wanakuacha utakuta watu wengi wanaishi mijini na kwenye Maendeleo yetu ni Vijijini kwa sababu kubwa uchumi wa nchi yetu unategemea sana mambo ya kilimo sasa watu wakienda kuishi mijini je huko vijijini wanawaacha wazee je kutakuwa na Maendeleo kweli?ndio utakuta vijana wanaishi mijini kazi yao kubwa kuiba unyan'ganyi uzururaji au uuzaji madawa ya kulevya na mambo ya ulevi tu sasa kweli nchi yetu itakuwa na Maendeleo ya kweli matokeo yake tunaishia kuomba omba tu kwa Wafadhili na hata kama hao wafadhili wakitusaidia pesa utakuata hizo pesa zinakwisha na hakuna kitu chochote kilichofanyika cha Maendeleo je tutafika kule tunakokwenda ndugu zangu Watanzania hilo tujiulize kila wakati na kila saa tuache mambo ya uvivu, chuki,tuwe kitu kimoja tushikamane kuijenga nchi yetu asanteni sana.
   
 18. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #18
  Aug 20, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Makafu, hata wenyewe hawajiamini.
   
 19. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #19
  Aug 22, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  funika kombe .....
   
 20. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #20
  Aug 24, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  SMZ yatoa msimamo uandikishaji Pemba NAIBU Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Ali Juma Shamuhuna, amesema siasa za Zanzibar ‘zinatiwa chumvi’ na hawezi kuvunja sheria kwa sababu ya hofu ya kutokea machafuko visiwani humo.

  Shamhuna amesema, kusikia na kuona ni vitu viwili tofauti hivyo si lazima yanayotangazwa au kuandikwa kuhusu uandikishwaji wapiga kura Zanzibar yawe sahihi.

  Aliyasema hayo jana asubuhi jijini Dar es Salaam wakati anahojiwa katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na televisheni ya TBC1 ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

  Shamuhuna alisema kuona ni kuamini akimaanisha kwamba kuna tofauti kati ya taarifa za vyombo vya habari na hali halisi ya uandikishwaji wazanzibari katika daftari la kudumu la wapiga kura.

  Hata hivyo Shamuhuna amesema, hapendi hali ilivyo Pemba na hata kama hali hiyo inamtisha hawezi kuvunja sheria.

  Kwa mujibu wa Shamuhuna, jambo la msingi ni kuzingatiwa kwa sheria katika mchakato huo na si hofu ya hali ilivyo Zanzibar.

  Alisema, uandikishaji wapiga kura lazima uzingatie Katiba na sheria za uchaguzi na si vinginevyo kwa sababu utawala bora ni kufuata sheria na Katiba.

  Kiongozi huyo wa SMZ amesema, wanaoruhusiwa kujiandikisha kupiga kura Zanzibar ni walioishi visiwani humo si chini ya miaka mitatu. Amehoji kwa nini hivi sasa kuna watu wengi wasioshi Pemba wanakwenda kisiwani humo kujiandikisha kwenye daftari hilo.

  Alisema, kuna wananchi wengi wanaishi Tanzania bara lakini hivi sasa wanakwenda kujiandikisha Pemba hivyo ameuliza, kwa nini wasijiandikishe wanapoishi wanakwenda kufanya hivyo kisiwani humo?

  Kumekuwa na mvutano kuhusu uandikishwaji huo kwa kuwa wananchi wa Pemba wanapinga sharti la kuwa na kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi (Zan ID) ili waandikishwe.

  Mapema wiki hii Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume alisema, taratibu za kuwepo kitambulisho cha ukaazi pamoja na matumizi yake zimewekwa kisheria na kukubaliwa na pande zote mbili katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

  Aliwaeleza mabalozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU), Marekani, Canada, kuwa, mabalozi na washirika wa maendeleo hao watafute ukweli na uhakika kuhusu uandikishaji wa vitambulisho vya ukaazi pamoja na Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na wawasiliane na vyombo husika kabla ya kutoa taarifa zao.

  Rais Karume aliwaeleza mabalozi hao katika Ikulu ya Zanzibar kuwa, SMZ imekuwa ikifanya juhudi za makusudi za kuhakikisha kila Mzanzibari Mkaazi mwenye sifa za kujiandikisha katika Daftari la Kudumu anapatiwa haki yake hiyo.
  http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=3321
   
Loading...