CCM; Chama KATILI Kuwahi kutokea.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM; Chama KATILI Kuwahi kutokea..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Eng. Y. Bihagaze, Jun 11, 2012.

 1. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #1
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Sehenleed.. *!!

  Watu wapitao jamvini, watu makini walao chakula cha maneno hapa kwenye jamvi hili makini, sehenleed!!

  Chama chetu CCM, kinaweza kuingia kwenye orodha ya vyama Katili vilivyowahi kutokea hapa kwenye DUNIA hii ya Mola.

  Ukatili Wa Chama hiki unatokana Na propaganda zake za kinazi, kizayuni zenye umauti, ambazo wamebahatika kuzishusha na kuzikandamizia kwenye Mawazo yetu watanzania Na kutulevya, propaganda zilizosheheni *uongo mzito sana Na Kwa asilimia kubwa watanzania wengi sasa tunachukiana, kutengana Na kudharauliana Kwa misingi ya Ukabila Na udini

  Propaganda hizi zina ufashisti, zinazolenga kuhakikisha kwamba watawala wanabaki madarakani Kwa gharama iwayo yoyote ile hata Kama ni Kwa kumwaga damu ya watanzania..

  Ziko propaganda nyingi Lakini Leo niongelee mbili.

  1. UDINI.. CCM wametengeneza propaganda kwamba CHADEMA ni Chama cha UDINI.. Ukristu. Na Mgombea wake wa urais ni padre.. Propaganda hii ikanenepa sana kiasi Radio Iman maskini ya mungu wakawa wanamtaja mgombea huyu kama padre Slaa. CCM iwaombe sana radhi Waislam Tanzania Kwa kuwapotosha sana Na wakakosea si Kwa hiari Yao Bali Kwa matakwa ya uroho uliopitiliza Wa kutamani kuendelea kutawala. Sasa hadanganywi *mtu tena. Chama kina Katiba, sera, na taratibu iweje kiwe na Udini mbona wametufanya sisi kuku that way jamani.. ?Propaganda ni kama kansa kwenye ubongo Wa Mwanadamu, propaganda hii walifanikiwa nayo kwenye Chama cha CUF, Chama chetu kile kikadidimia, kikadidimia Na kuzama sasa kinajitutumua ila njaa Kali sana Sijui Kama kitatoka matopeni. Professor Lipumba akaitwa pumba tu, he watu wote tukamdharau kwamba ni professor wa Pumba, kumbe kichwa cha nguvu kiasi DUNIA ya uchumi inamtamani Na sasa inamtumia.. Nakushauri Lipumba kubali walikufanyia TIMING that time, embu JIUNGE CDM, wang'olewe kwanza hawa wasio Na roho za ibinaadam. Mengine baadae

  2. UKABILA. baada ya Dola ya propaganda ya UDINI kupata matatizo mawili, moja la uchaguzi wa Igunga, ambapo mbali Na kudumbukiza propaganda hiyo Kwa nguvu sana, Na kushinikiza viongozi wetu wa Dini kutoa matamko makali sana, Lakini CCM ilishtuka sana ilipoambulia ushindi mwembamba sana kwenye kinyang'anyiro hicho, Na pigo la pili ni Uchaguzi jimbo la Uzini ambapo CDM ilikuwa ya pili badala ya kuwa ya tatu au nne. Upepo huo uliwapa ujumbe kwamba Kete ya UDINI sasa imeishiwa Charge.. Sasa wamekuja Na Gia nyingine mbaya zaidi ya Ukabila, kwamba CDM ni Chama cha wachaga, na wameiongezea nguvu kwamba ni Chama cha Ukanda.. Yaani propaganda za CCM ni za kimautimauti, watugawe watanzania kwenye ukanda, wa kaskazini, kusini, magharibi Na mashariki..manake nini Kama CCM wakipata kura nyingi kusini Na CDM kaskazini Basi wataoshika Dola upande wa pili watavutana wajitenge Na hapo ndipo tutarejea Sudan Na umwagaji Damu wa Kutisha..

  CCM akili zake sasa hazina akili tena. Kama inapumulia mpira si ikubali kufa peke yake kwani lazima ife Na damu za watu!!.. *Aah!!*
   
 2. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Kumbe kumuita slaa kwa title yake ya UPADRE ni udini? hebu jifunze kujenga hoja we mchadema!
   
 3. J

  John W. Mlacha Verified User

  #3
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  asante mama
   
 4. J

  John W. Mlacha Verified User

  #4
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  acha kuitetea ccm. unakumbuka CUF walisingiziwa kuwa wamekamatwa na silaha mapanga rungu etc. Kipindi cha mahita
   
 5. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Umeshafunguka sasa, karibu kwenye mapambano ya kumg'oa mkoloni mweusi
   
 6. m

  mzee wandimu JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 23, 2011
  Messages: 441
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  come 2015! eeh Mwenyezi MUNGU nilinde/nijalie uzima nishuudie ukombozi wa inchi yangu!
   
 7. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #7
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Mkuu wangu mimi sijapinga/wala kukataa na wala sijaitetea CCM kama ulivyonituhumu, Nimeshangaa iweje kumuita slaa kwa title yake iwe udini? Na ndio maana nimemuomba mtoa mada ajenge hoja!
   
 8. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Nilikuona pale Jangwani ulikuwa ukiyaongoza mafuso kushusha wenzako wenye upeo kama wa kwako
   
 9. J

  John W. Mlacha Verified User

  #9
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  yule alikuwa padri akaacha ..sasa iweje radio imaam waanze kuwatangazia waislamu kuwa slaa bado ni padri. angalia wameichagua ccm na wote tunataabika sasa hivi. wangeichagua hata CUF basi
   
 10. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #10
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Tume ya katiba, usiwe sisimizi wa fikra, kwenye umbo la Hoja yote mwenzetu umeambulia Hilo tu? . Mbona Na wewe unakuwa na Mawazo Kama Kamasi?

  Nasema TITLE za viongozi wetu Wa kiimani ni vema tukaziheshimu tu hata Kama hatuzipendi..

  Sheikh, padre, Askof, imam nadhani sio za kuchezea.. Kama huamini Dini ya mwenzio hekima ni kukaa kimya.. Wanasema wao padre ni kiongozi wa kanisa, Mtu asiye Na mke Wala watoto. Sasa huyu Slaa openly ana Mke Na watoto, alishaacha upadre Mie nadhani si heshima kumdhalilisha kupitia redio inayoheshimika.. Ni msingi wa udini. Ashkhum Kama namkosea Mtu jamani..
   
 11. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #11
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Mkuu nisamehe kama nitakuuzi, MKE padri slaa kaoa lini? huenda nipo mbali na matukio!

  Pili, title haiondoki kwa kuacha ile shughuli, nafikili umesahau tu naomba nikukumbushe! msigwa na natse wanaendelea kuitwa wachungaji hata baada ya kuwa wanasiasa.

  Ndio maana nikasema umeshindwa kujenga hoja, na jibu lako limedhihirisha!

  Umeelewa?
   
 12. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #12
  Jun 11, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  U're very right sister! Right answer to the right person!
   
 13. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #13
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Njaa mbaya sana, hasa ukiwa unatumiwa unakuwa kama zombe, hujitambui. Lakini siku utayojitambua ndio mwanzo wa kuwaona wakina Nape ni maadui zako.
   
 14. M

  Msendekwa JF-Expert Member

  #14
  Jun 11, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 440
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Slaa kwa sasa si Padre, ht km aliwahi kuwa.
  Unaposisitiza kumtambua km Padre wkt alishaacha kwa ruhusa ya Vatican, na kutaka wengne wamuone kwa upadri wake na sio km mtanzania, huo ndo udini ktk hilo.
   
 15. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #15
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  mkuu wewe juzi ulisema ni ADC,mbona unakua mjibu hoja wa CCM?angalia nawe usije anza kuvaa cheni shingoni na mkorogo usoni kama katibu mwenezi
   
 16. J

  John W. Mlacha Verified User

  #16
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  kuna tofauti kubwa sana kati ya padri na mchungaji. wewe mpemba una matatizo kweli kweli ndio maana mnahangaika kuvunja muungao huku hamtaki kuuvunja.
  kuan tofauti kuwa sana kati ya katoliki , analikana , letheran etc kwa hiyo usiropoke ropoke kama hujui..na inawezekama wewe ni mtangazaji wa redio imam
   
 17. B

  Bob G JF Bronze Member

  #17
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Athali ya kauli hizi za ccm ni kubwa mno zinawagawa watanzania, na ccm wako radhi watu wagawike wao waendelee kutawala
   
 18. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #18
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  ..
  Sidhani Kama marumbano ni fani yangu.. Nijibu ka swali kadogo sana tafadhali.. Je ni SAHIHI redio hii inayoheshimika kuendelea kumuita Dr. Slaa Kama Padre Slaa.. TAFADHALI NAOMBA JIBU..
   
 19. Iselamagazi

  Iselamagazi JF-Expert Member

  #19
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 2,221
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Splendido!
   
 20. F

  Froida JF-Expert Member

  #20
  Jun 11, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Unashangaa nini Hii ni sera aliianzisha Mh Jakaya KIkwete,Ridhiwani,Miraji ,Halfani na Mkewe Salma Kikwete katika kampeni zake za mwaka 2010.
  Haitoshi alipokuwa anatangazwa kuwa mshindi bado alisisitiza kwamba nchi immeingia kwenye udini
  Haitoshi alipokuwa akizinduwa Bunge alisisitiza kwa mkazo wa ajabu akisema kwamba nchi ina udini na kuna vyama vyenye udini ambavyo wagombea wake walisimamiwa na Kanisa ambao hawakujali hata kuingia IKULU kwa kupanda Maiti za ajabu

  Mpaka na kufa nitamchukia kikwete,viongozi waliopo usalama wa Taifa sasa ambao ni waroho wa madaraka wanaoigawa nchi vipande vipande kwa manufaa yao na vizazi vyao
  Natusipo simama watanzania kuwakemea leo kiama chake kitatumaliza wote
   
Loading...