Jamco,
Hii inajulikana wapi??
tusipende kujumisha mambo,yaani kama ukiw ana mwenyekiti Mhuni na baadhi ya watu wanaomzunguka wakiwa ni walevi sana na wanopenda sana totoz kw muda mrefu,mathalani miaka kama 20 iliyopita na wanaendeleza libeneke hili mpaka sasa,unaweza kukiita vipi cham hicho..
i said first and narudia tena,ahc kukejeli chama cha mapinzuzi,tushindane kwa hoja
Ndugu Gembe hebu tulia kidogo usihamaki. Sikiliza wanachokisema kisha pembua unayoweza kuyafanyia kazi. Yawezekana usemayo yakawa ni kweli academically lakini kihalisia yasiwe hivyo kwa sababu:
Kiongozi fisadi huchaguliwa na wanachama mafisadi.
Asipochaguliwa na mafisadi, hupigiwa debe na mafisadi.
Kwa mfumo wa uchaguzi wa ccm ulivyo, haiepukiki kuchagua viongozi mafisadi kwa sababu ndani ya ccm, ufisadi ulipewa majina kama MWENZETU n.k. Kw hiyo usitegemee vinginevyo.
CCM, kihistoria, nadhani kinaweza kuwa chama tofauti na vyama vingine duniani kwa sababu ya majukumu kilchopewa na watz. ccm ni chama pekee kilichopewa dhima za kuweka misingi ya taifa, kikashindwa. Kimepewa jukumu la kujenga demokrasia kikashindwa hata ndani yake chenyewe. Uchumi kilishindwa hata kabla hakijaanza kwa kuuwa SUKITA.
Ndani ya ccm tukajengewa dhana kuwa ujanja ndio deal. Kila mtu akawa hataki kazi tena,bali hela. Nenda white house au Lumumba uone kinachofanyika. Ni kelele kana kwamba sio ofisi iliyopewa dhamana ya kusimamia na kuendeleza mustakabali wa taifa.
Ccm wameshindwa kujenga classes based on thoughts bali wamejenga based on ujanjaujanja tu.
Trace cv za viongozi na wafanyakazi wa chama kuanzia ngazi ya matawi, unaweza kuona tatizo liko wapi. Hakuna anayehubiri imani ya chama hata mmoja. Hakuna anayechaguliwa kwa ukulima wala ufanyakazi wake hodari. Ni ujanja kwa kwenda mbele huku KUSHUGHULIKIANA ikiwa ndiyo silaha kuu ya kujenga na kulinda chama.
Nadhani wakati umefika kwa hasa wanachama wasafi unaowatetea kuamua kujipembua wakasimamia na kutetea wanachokiamini ambacho sio kingine zaidi imani ya chama na WAKAJITAMBULIASHA kuwa wanaamini hivyo na wakatetea msimamo wao bila ya uoga kama alivyofanya Nyerere.
Naamini mkifanya hivyo mtarudisha ccm iliyokusudiwa na Nyerere.[/SIZE]