Sitachoka
JF-Expert Member
- Nov 17, 2011
- 3,030
- 1,303
NIMECHOCHEWA kuandika makala
haya kufuatia mjadala ulijitokeza
kati yangu na rfk yangu anayeishi, kusoma na
kufundisha Uingereza.
Huyu bwana ni mwalimu wa
Hisababati na Fizikia, na ndio
anavifundisha Uingereza. Mjadala
ulianza pale tulipokuwa
tunakatiza katika mitaa ya chuo
kikuu cha Birmingham hapa
Uingereza tukaona jengo moja
limeandikwa (Physics and
Astronomy). Kwa Kiswahili cha
haraka haraka maana ya haya
meneno ni Fizikia na Elimu ya
Anga za juu.
Kuona maneno ya Physics and
Astronomy ilizusha mjadala mkali
sana lakini unaorutubisha akili
kati yangu na huyu rafiki yangu.
Bwana Nkwabi alianza kwa
kusema wenzetu Waingereza
wanachokisoma wanakifanyia
kazi kwa vitendo ndio maana
wanaweza kupeleka vyombo
mwezini na katika anga nyingine
za mbali, achilia mbali mambo
mengine luluki makubwa
wanayoyafanya. Elimu ya
Waingereza inaendana na
uhalisia wa mambo. Hawaandai
mitaala ya masomo ili tu
kujiridhisha.
Nikupe mfano mwepesi, wiki
jana nilienda shuleni kwa binti
yangu anayesoma shule ya awali,
kumchukua baada ya muda wa
masomo kwisha. Kwa kawaida
kwa sheria za Uingereza watoto
wa shule za awali, na msingi
lazima wapelekwe shule na
kufuatwa kurudishwa nyumbani
na wazazi au walezi wao. Hii ni ili
kuakikisha usalama wa watoto.
Nilipofika shuleni nikakuta
mapokezi wameweka machine
mbili ndogo za kuangulia vifanga
vya kuku na wakawa
wanaanguliwa. Ukubwa wa kila
machine ni futi moja kwa futi
moja.
Kwa hiyo watoto wakawa
wanoana vifanga wa kuku
wanavyoanguliwa. Bila
kuambiwa chochote watoto
wanajifunza vitu vingi sana. Mie
mwenyewe binti yangu japo ana
miaka miwili na nusu, alianza
kuniuliza maswali mengi sana
kuhusu mayai, kuku, ndege na
kadhalika.
Bwana Nkwabi akaigeukia
Tanzania, na kusema wasomi
wetu, hasa akimaanisha
maprofesa na madakitari wa
falisafa wanachojifunia ni
papers ngapi wameandika na
kuwasilisha katika
makongamano. Nami nikachapia
kwa kusema pia wanaona sifa na
fahari kwa wingi wa kuku na
ngombe wanaofuga na bar
wanazomiliki. Naye
akachombeza, sasa kwa mtindo
huu ni saa ngapi tutaona elimu
yao ikitembea barabarani.
Kutoka hapa tukajadili je ni
kwanini wasomi wetu
wanashindwa kutafsiri elimu
walio nayo katika bongo zao
ikaonekana na jamii na
kutunufaisha kama Taifa.
Tukakimbilia jibu rahisi na labda
la kichovu kwa vile hatukupenda
kufikiri kwa kusema wasomi
wetu hatuwapi rasilimali pesa na
pia nafasi. Ila hatukujadili je
kwanini wasingepewa hizi pesa
za EPA badala ya kuwachia akina
Green na Kagoda Industrial
wazisunde wavavyotaka.
Sikuvunjika moyo maana
nilikumbuka nchi ya Ghana,
ambayo ni waafrika wenzetu.
Wao mitaala yao imeelekezwa
kumuanda Mghana kufanya kazi
pahala popote duniani. Ndio
maana katika katika kazi kubwa
na mashirika ya kimataifa
hutakosa Mghana.
Kwa jinsi hii siwezi kushangaa
Kofi Anan wa Ghana alifanikiwaje
kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, maana ni matunda ya
mikakati ya makusudi kielimu.
Katika mada hii nitajaribu kujadili
na kuchokoa kuwa licha ya
kisingizio cha kutokupewa pesa
na nafasi bado wasomi wetu
wanaweza kutoka katika vyumba
walivyojifungia na kutumia
mianya mingi iliyopo na kuweza
kutafasiri elimu yao katika
vitendo.
Ila ni lazima tuanze na msingi
nzuri na imara
Nitajaribu kujikita katika elimu ya
msingi na kiasi fulani elimu ya
awali kujadili tufanye nini. Maana
naamini tukishakuwa na msingi
na mitaala mizuri huko chini,
sekondari, vyuo vya kati na hata
nyuo vikuu haitakuwa kazi
ngumu, maana itakuwa ni jadi
yetu.
Pa kuanzia ni kuifanyia ukarabati
mkubwa mitaaala yetu ili iendane
na hali hali halisi ya kiuchumi na
dunia na zaidi izingatie
mazingira yetu. Nitatoa mifano
michache ili ichokoze kufikiri
kwetu.
Nianze na mfano wa somo la
historia, badala kungangania
kujua historia ya kila pahala
duniani. Somo la historia
lifundishwe na kuakikisha
mwanafunzi anaijua historia ya
nchi yetu barabara.
Tunawacheka Waingereza au
Wamarekani watoto wao
wanapokua hawajui historia au
mambo ya nchi nyingine, ila ya
kwao wanayafahamu kama sala
ya Bwana. Wanaona haiwasaidii
chochote watoto wao kuimba
kama kama kasuku mambo ya
kila pembe ya dunia, wakati yalio
uhani kwao wanayajua
nusunusu.
Mfano mwingne ni somo la
Jografia. Kwa jinsi
linavyofundiswa sasa hivi
halimuandai na kumfanya mtoto
aelewe mazingira ya Jografia ya
Tanzania na jinsi ya kupambana
nayo.
Mtoto atakariri wee Tanzania
kuna mito, maziwa, milima,
madini kiasi gani, bas!
Tungeenda hatua moja zaidi na
kumfanya aone je, hivi vitu
vinagusaje maisha yao
haya kufuatia mjadala ulijitokeza
kati yangu na rfk yangu anayeishi, kusoma na
kufundisha Uingereza.
Huyu bwana ni mwalimu wa
Hisababati na Fizikia, na ndio
anavifundisha Uingereza. Mjadala
ulianza pale tulipokuwa
tunakatiza katika mitaa ya chuo
kikuu cha Birmingham hapa
Uingereza tukaona jengo moja
limeandikwa (Physics and
Astronomy). Kwa Kiswahili cha
haraka haraka maana ya haya
meneno ni Fizikia na Elimu ya
Anga za juu.
Kuona maneno ya Physics and
Astronomy ilizusha mjadala mkali
sana lakini unaorutubisha akili
kati yangu na huyu rafiki yangu.
Bwana Nkwabi alianza kwa
kusema wenzetu Waingereza
wanachokisoma wanakifanyia
kazi kwa vitendo ndio maana
wanaweza kupeleka vyombo
mwezini na katika anga nyingine
za mbali, achilia mbali mambo
mengine luluki makubwa
wanayoyafanya. Elimu ya
Waingereza inaendana na
uhalisia wa mambo. Hawaandai
mitaala ya masomo ili tu
kujiridhisha.
Nikupe mfano mwepesi, wiki
jana nilienda shuleni kwa binti
yangu anayesoma shule ya awali,
kumchukua baada ya muda wa
masomo kwisha. Kwa kawaida
kwa sheria za Uingereza watoto
wa shule za awali, na msingi
lazima wapelekwe shule na
kufuatwa kurudishwa nyumbani
na wazazi au walezi wao. Hii ni ili
kuakikisha usalama wa watoto.
Nilipofika shuleni nikakuta
mapokezi wameweka machine
mbili ndogo za kuangulia vifanga
vya kuku na wakawa
wanaanguliwa. Ukubwa wa kila
machine ni futi moja kwa futi
moja.
Kwa hiyo watoto wakawa
wanoana vifanga wa kuku
wanavyoanguliwa. Bila
kuambiwa chochote watoto
wanajifunza vitu vingi sana. Mie
mwenyewe binti yangu japo ana
miaka miwili na nusu, alianza
kuniuliza maswali mengi sana
kuhusu mayai, kuku, ndege na
kadhalika.
Bwana Nkwabi akaigeukia
Tanzania, na kusema wasomi
wetu, hasa akimaanisha
maprofesa na madakitari wa
falisafa wanachojifunia ni
papers ngapi wameandika na
kuwasilisha katika
makongamano. Nami nikachapia
kwa kusema pia wanaona sifa na
fahari kwa wingi wa kuku na
ngombe wanaofuga na bar
wanazomiliki. Naye
akachombeza, sasa kwa mtindo
huu ni saa ngapi tutaona elimu
yao ikitembea barabarani.
Kutoka hapa tukajadili je ni
kwanini wasomi wetu
wanashindwa kutafsiri elimu
walio nayo katika bongo zao
ikaonekana na jamii na
kutunufaisha kama Taifa.
Tukakimbilia jibu rahisi na labda
la kichovu kwa vile hatukupenda
kufikiri kwa kusema wasomi
wetu hatuwapi rasilimali pesa na
pia nafasi. Ila hatukujadili je
kwanini wasingepewa hizi pesa
za EPA badala ya kuwachia akina
Green na Kagoda Industrial
wazisunde wavavyotaka.
Sikuvunjika moyo maana
nilikumbuka nchi ya Ghana,
ambayo ni waafrika wenzetu.
Wao mitaala yao imeelekezwa
kumuanda Mghana kufanya kazi
pahala popote duniani. Ndio
maana katika katika kazi kubwa
na mashirika ya kimataifa
hutakosa Mghana.
Kwa jinsi hii siwezi kushangaa
Kofi Anan wa Ghana alifanikiwaje
kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, maana ni matunda ya
mikakati ya makusudi kielimu.
Katika mada hii nitajaribu kujadili
na kuchokoa kuwa licha ya
kisingizio cha kutokupewa pesa
na nafasi bado wasomi wetu
wanaweza kutoka katika vyumba
walivyojifungia na kutumia
mianya mingi iliyopo na kuweza
kutafasiri elimu yao katika
vitendo.
Ila ni lazima tuanze na msingi
nzuri na imara
Nitajaribu kujikita katika elimu ya
msingi na kiasi fulani elimu ya
awali kujadili tufanye nini. Maana
naamini tukishakuwa na msingi
na mitaala mizuri huko chini,
sekondari, vyuo vya kati na hata
nyuo vikuu haitakuwa kazi
ngumu, maana itakuwa ni jadi
yetu.
Pa kuanzia ni kuifanyia ukarabati
mkubwa mitaaala yetu ili iendane
na hali hali halisi ya kiuchumi na
dunia na zaidi izingatie
mazingira yetu. Nitatoa mifano
michache ili ichokoze kufikiri
kwetu.
Nianze na mfano wa somo la
historia, badala kungangania
kujua historia ya kila pahala
duniani. Somo la historia
lifundishwe na kuakikisha
mwanafunzi anaijua historia ya
nchi yetu barabara.
Tunawacheka Waingereza au
Wamarekani watoto wao
wanapokua hawajui historia au
mambo ya nchi nyingine, ila ya
kwao wanayafahamu kama sala
ya Bwana. Wanaona haiwasaidii
chochote watoto wao kuimba
kama kama kasuku mambo ya
kila pembe ya dunia, wakati yalio
uhani kwao wanayajua
nusunusu.
Mfano mwingne ni somo la
Jografia. Kwa jinsi
linavyofundiswa sasa hivi
halimuandai na kumfanya mtoto
aelewe mazingira ya Jografia ya
Tanzania na jinsi ya kupambana
nayo.
Mtoto atakariri wee Tanzania
kuna mito, maziwa, milima,
madini kiasi gani, bas!
Tungeenda hatua moja zaidi na
kumfanya aone je, hivi vitu
vinagusaje maisha yao