CCM, CHADEMA, NCCR, CUF n.k vilaumiwe kwa wasomi wetu kugeuka kuwa wafagiaji mabanda ya kuku?

Mbaga Michael

Verified Member
Nov 17, 2011
2,907
1,250
NIMECHOCHEWA kuandika makala
haya kufuatia mjadala ulijitokeza
kati yangu na rfk yangu anayeishi, kusoma na
kufundisha Uingereza.
Huyu bwana ni mwalimu wa
Hisababati na Fizikia, na ndio
anavifundisha Uingereza. Mjadala
ulianza pale tulipokuwa
tunakatiza katika mitaa ya chuo
kikuu cha Birmingham hapa
Uingereza tukaona jengo moja
limeandikwa (Physics and
Astronomy). Kwa Kiswahili cha
haraka haraka maana ya haya
meneno ni Fizikia na Elimu ya
Anga za juu.
Kuona maneno ya Physics and
Astronomy ilizusha mjadala mkali
sana lakini unaorutubisha akili
kati yangu na huyu rafiki yangu.
Bwana Nkwabi alianza kwa
kusema wenzetu Waingereza
wanachokisoma wanakifanyia
kazi kwa vitendo ndio maana
wanaweza kupeleka vyombo
mwezini na katika anga nyingine
za mbali, achilia mbali mambo
mengine luluki makubwa
wanayoyafanya. Elimu ya
Waingereza inaendana na
uhalisia wa mambo. Hawaandai
mitaala ya masomo ili tu
kujiridhisha.
Nikupe mfano mwepesi, wiki
jana nilienda shuleni kwa binti
yangu anayesoma shule ya awali,
kumchukua baada ya muda wa
masomo kwisha. Kwa kawaida
kwa sheria za Uingereza watoto
wa shule za awali, na msingi
lazima wapelekwe shule na
kufuatwa kurudishwa nyumbani
na wazazi au walezi wao. Hii ni ili
kuakikisha usalama wa watoto.
Nilipofika shuleni nikakuta
mapokezi wameweka machine
mbili ndogo za kuangulia vifanga
vya kuku na wakawa
wanaanguliwa. Ukubwa wa kila
machine ni futi moja kwa futi
moja.
Kwa hiyo watoto wakawa
wanoana vifanga wa kuku
wanavyoanguliwa. Bila
kuambiwa chochote watoto
wanajifunza vitu vingi sana. Mie
mwenyewe binti yangu japo ana
miaka miwili na nusu, alianza
kuniuliza maswali mengi sana
kuhusu mayai, kuku, ndege na
kadhalika.
Bwana Nkwabi akaigeukia
Tanzania, na kusema wasomi
wetu, hasa akimaanisha
maprofesa na madakitari wa
falisafa wanachojifunia ni
‘papers’ ngapi wameandika na
kuwasilisha katika
makongamano. Nami nikachapia
kwa kusema pia wanaona sifa na
fahari kwa wingi wa kuku na
ngombe wanaofuga na bar
wanazomiliki. Naye
akachombeza, sasa kwa mtindo
huu ni saa ngapi tutaona elimu
yao ikitembea barabarani.
Kutoka hapa tukajadili je ni
kwanini wasomi wetu
wanashindwa kutafsiri elimu
walio nayo katika bongo zao
ikaonekana na jamii na
kutunufaisha kama Taifa.
Tukakimbilia jibu rahisi na labda
la kichovu kwa vile hatukupenda
kufikiri kwa kusema wasomi
wetu hatuwapi rasilimali pesa na
pia nafasi. Ila hatukujadili je
kwanini wasingepewa hizi pesa
za EPA badala ya kuwachia akina
Green na Kagoda Industrial
wazisunde wavavyotaka.
Sikuvunjika moyo maana
nilikumbuka nchi ya Ghana,
ambayo ni waafrika wenzetu.
Wao mitaala yao imeelekezwa
kumuanda Mghana kufanya kazi
pahala popote duniani. Ndio
maana katika katika kazi kubwa
na mashirika ya kimataifa
hutakosa Mghana.
Kwa jinsi hii siwezi kushangaa
Kofi Anan wa Ghana alifanikiwaje
kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, maana ni matunda ya
mikakati ya makusudi kielimu.
Katika mada hii nitajaribu kujadili
na kuchokoa kuwa licha ya
kisingizio cha kutokupewa pesa
na nafasi bado wasomi wetu
wanaweza kutoka katika vyumba
walivyojifungia na kutumia
mianya mingi iliyopo na kuweza
kutafasiri elimu yao katika
vitendo.
Ila ni lazima tuanze na msingi
nzuri na imara
Nitajaribu kujikita katika elimu ya
msingi na kiasi fulani elimu ya
awali kujadili tufanye nini. Maana
naamini tukishakuwa na msingi
na mitaala mizuri huko chini,
sekondari, vyuo vya kati na hata
nyuo vikuu haitakuwa kazi
ngumu, maana itakuwa ni jadi
yetu.
Pa kuanzia ni kuifanyia ukarabati
mkubwa mitaaala yetu ili iendane
na hali hali halisi ya kiuchumi na
dunia na zaidi izingatie
mazingira yetu. Nitatoa mifano
michache ili ichokoze kufikiri
kwetu.
Nianze na mfano wa somo la
historia, badala kungangania
kujua historia ya kila pahala
duniani. Somo la historia
lifundishwe na kuakikisha
mwanafunzi anaijua historia ya
nchi yetu barabara.
Tunawacheka Waingereza au
Wamarekani watoto wao
wanapokua hawajui historia au
mambo ya nchi nyingine, ila ya
kwao wanayafahamu kama sala
ya Bwana. Wanaona haiwasaidii
chochote watoto wao kuimba
kama kama kasuku mambo ya
kila pembe ya dunia, wakati yalio
uhani kwao wanayajua
nusunusu.
Mfano mwingne ni somo la
Jografia. Kwa jinsi
linavyofundiswa sasa hivi
halimuandai na kumfanya mtoto
aelewe mazingira ya Jografia ya
Tanzania na jinsi ya kupambana
nayo.
Mtoto atakariri wee Tanzania
kuna mito, maziwa, milima,
madini kiasi gani, bas!
Tungeenda hatua moja zaidi na
kumfanya aone je, hivi vitu
vinagusaje maisha yao
 

kanga

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
1,020
1,225
Elimu na matokeo yake ni pamoja na sera mbalimbali na bajeti. Kwa bahati mbaya Tz wanasiasa na vyama vya siasa vinaandaa sera na usimamizi na utekelezaji wa sera wote wamekuwa mafisadi. Hayo matunda na matokeo unayotaka yatatoka wapi kama ccm ni ufisadi kwenda mbele.?R& D hakuna bajeti ahyo mazuri yatatoka wapi?.CCM NI JANGA LA TAIFA.bajeti ya jk kutalii dunia sasa inazidi bajeti ya serikali kwa safari zote alizofanya tangu aingie madarakani 2005.ccm iache tupmue wandungu zangu
 

CHASHA FARMING

Verified Member
Jun 4, 2011
6,836
2,000
Mkuu wewe ni muongo sana uingereza haijawahi kupeleka mtu anga za juu. Hata mwezini sidhani kama walisha peleka. Anga za juu ni USA,URUSI, na juzijuzi CHINA,hasa wamepeleka kwa kutumia vyombo vyao wenyewe, CHINA akisaidiwa na URUSI
 

MR. ABLE

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,474
2,000
Mbona kama naona umbeep Jk uone kama hatakupa uwaziri.
No.tigo ya 12 ikifuatiwa na pinda ya 34 pamoja na Napenya ya mwisho.
Uwasilianaji mwema.
 

Mbaga Michael

Verified Member
Nov 17, 2011
2,907
1,250
Nimesoma makala na michango
yenu kwa masikitiko makubwa
sana. Tanzania ni nchi yenye
uwezo wa kuondokana na huu
ubutu wa kufikiria lakini kama
alivyosema mmoja hapo juu
tatizo ni muda wa kufikiria
mambo kwa mapana kila mtu
mwenyewe katika eneo lake.
kumekuwepo na fikra tegemezi
katika maisha ya watanzania
wengi wasomi na hakuna mahali
imeonekana hao wasomi
walioko ndani na nje ya Tz
wanaweza kukutana pamoja
wakaweka mawazo yao sawa
nakufanya jambo ila wanaishia
kulaumu tu.
Hapa chuoni kwangu UK katika
idara moja maarufu sana kwa
mazingira wanakutana kila
wakati kupeana changamoto za
ufanisi na wanatafuta sources of
funds kutatua shida
wanazokutana nazo. kule kwetu
kuna kitu kinaitwa divide and
rule kuanzia mashuleni, vyuoni
na maofisini, ni mara chache
sana uone vikao vya kujadili
challenges and the way foward
yamambo mbalimbali. mikutano
mingi imeishia kwenye kuonyana
kuwa usiguse vitu vya
wazee,matumizi ya agrarian
leadeship na mambo
yanayofanana na hayo. Kuna
viongozi walipanda cheo kwa
sababu ya heshima ya uoga ya
NDIO MZEE/BOSI KATIKA KILA
KITU, JE WATU KAMA HAO NI LINI
WATAKAA CHNI NA KUGUNDUA
MAMBO WAKATI ANASUBIRI
KUSSEMA NDIO KILA SIKU IITWAPO
LEO ILI MWISHO WA MWAKA
AITWE MFANYAKAZI BORA.
Huku kwenye hizi nchi mambo
hayaendi bila kuonesha
competencies and efficient,
unaachishwa kazi kwa tabasamu
murua ukiwa hopeless, kule
kwetu ukichallenge system ndio
unashushwa cheo au
unahamishiwa namtumbo ili tu
UFIKE MAHALI PA Kuseme hutaki
kazi au wakati mwngine
unaachishwa kwa maslahi ya
taifa ambayo mimi natafsiri kwa
kusema kwa maslahi ya wazee
wa nchi. Hivi tunaelewa chanzo
cha kuhamishwa wizara moja
kwenda nyingine hata kama
huna huo ujuzi? Basi watanzania
wanafurahia hiyo bila kujiuliza
sababu nini hasa! Kulikuwa na
chama cha wasomi kama
mnakumbuka lakini kiliuawa
ghafla kwani ilikuwa imeundwa
na vichwa vilivyojaa ugunduzi na
mzee mmoja kule top used a
divide and rule kwa kuwapa
wale top leaders vyeo serikalini
na chama kikafa.
Hebu sisi basi tuform mtandao
wetu na kutumia mbinu ya
infiltration badala ya
confrontation kuleta mabadiliko
Tz na sio kuongea tu bila kufanya
jambo

Nawasilisha wapendwa wangu
 

Ngagarupalu

Senior Member
Oct 13, 2012
156
0
hapo, hajua kitu!!
1. wale wa nje yanayaona mambo kwenye macho mawili, sisi wa tanzania tunaya ona kwa macho matatu!! kummpa mtoto wa miaka 2.5 mayai na vifaranga ni nje, siyo hapa. sababu gharama za elimu na vitu vyote hapa ni "hypered". FEZA ni moja ya best sec school, ila pale kama huna DIV on, pt 7-10 huwezi jiunga, ila kuna mtoto wa kike alipata "zero" ukiondoa gharama zake.
2. shule za kata hapo ambazo ni mafanikio ya serikali ya CCM zina walimu 2- 8, masomo ni saba, je watafundishwa nini na nani? ( kumbuka hapo kuna administrator)
3. Bajet ya shule za europe hazitegemei, misaada, hivyo na private school zitzkuwa bora zaidi!!
mwisho, nakupa ukweli huu, Jamaa yangu alikuwa anasoma PhD ( natumai ndo wasomi wajuu) hawezi kumwona supervisor kwa miezi 3, alipo uliza akaambiwa "Supervisor" akasema ninahitaji fedha hivyo naanza na kitu kinalipa kwanza, ili niweze kushi na famili yangu, kabla sija maliza na haya ya business as usual... jamaa akasema hivi wewe ukiwa PhD utapanda daladla, watoto wako watasoma "Kayumba"? au unataka unione napanda bodaboda? jamaa akanywea....
Hivyo imefikia kipindi ukiwa msomi hapa tanzania ni kama unatafuta kashfa, maswali na matani, dharau, n.k, maana kun watuu wanapeza hata kutia saini ukumwambia arudie hazitafanana. hao ndo wajanja wa "mujini" wanahela mbaya, wewe na degree zako unaendesha pick up, wao wana "hammer" ...... nahisi inatosha kujua sasa hakuna mtu kukaa na kuvumbua, ila cut, process paste, life come, days go on.... Siasa imeharibu wananchi kuanzia matonya hadi Kingunge aka Kigogo, msomi na asiye msomi wanaishi kwa SURVIVAL... Jamani njooni njooni hapa Tanzania mfanye kazi japo miezi6, mpate jicho la tatu.
Wakatabahu
 

Ngagarupalu

Senior Member
Oct 13, 2012
156
0
hapo, hajua kitu!!
1. wale wa nje yanayaona mambo kwenye macho mawili, sisi wa tanzania tunaya ona kwa macho matatu!! kumpa mtoto wa miaka 2.5 mayai na vifaranga ni nje, siyo hapa. sababu gharama za elimu na vitu vyote hapa ni "hypered". FEZA is on of best sec school, ila pale kama huna DIV, pt 7-10 huwezi jiunga, ila kuna mtoto wa kike alipata "zero" ukiondoa gharama zake. kama ni huko uropa ingekuwa je?
2. shule za kata hapo ambazo ni mafanikio ya serikali ya CCM zina walimu 2- 8, masomo ni saba, je watafundishwa nini na nani? ( kumbuka hapo kuna administrator)
3. Bajet ya shule za europe hazitegemei, misaada, hivyo na private school zitzkuwa bora zaidi!!
mwisho, nakupa ukweli huu, Jamaa yangu alikuwa anasoma PhD chuo cha hapa Tanzania ( natumai ndo wasomi wajuu) hajaweza kumwona supervisor kwa miezi zaidi ya 3 siku alipo mwona akauliza "Supervisor" akasema ninahitaji fedha hivyo naanza na kitu kinalipa kwanza, ili niweze kushi na famili yangu, kabla sija maliza na haya ya business as usual... jamaa akaulizw hivi wewe ukiwa PhD utapanda daladala, watoto wako watasoma "Kayumba"? au unataka unione napanda bodaboda? jamaa akanywea....
Hivyo imefikia kipindi ukiwa msomi hapa tanzania ni kama unatafuta kashfa, maswali na matani, dharau, n.k, maana kuna watu wanapeza hata kutia saini ukumwambia arudie hazitafanana. hao ndo wajanja wa "mujini" wanahela mbaya, wewe na degree zako unaendesha pick up, wao wana "hammer" ...... nahisi inatosha kujua sasa hakuna mtu kukaa na kuvumbua, ila cut, process paste, life come, days go on.... Siasa imeharibu wananchi kuanzia matonya hadi Kingunge aka Kigogo, msomi na asiye msomi wanaishi kwa SURVIVAL... Jamani njooni!! njooni hapa Tanzania mfanye kazi japo miezi6, mpate jicho la tatu.
Wakatabahu
 

Capital

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
1,326
2,000
Hii kitu inafikirisha kiasi. Tanzania haina tofauti na nchi nyingi za kiafrika katika nyanja za kiuchumi, elimu ikiwemo. ni vema tukaangalia historia. elimu yetu ni ile tuliyorithi toka kwa wakoloni, elimu imejaa fitna tokea juu hadi chini, elimu isiyolenga kumfanya mtu afikirie kwa nini anasoma au nini mchango wake kwa jamii yake. watu wanasoma ili mradi tuu. athari zake mojawapo ni kuwa wote tuna fikra sawa, kama katibu kata. raisi anafikiria kama katibu kata, profesa, daktari wa falsafa, mwanafunzi, wote 'mazi ga nyanza'. binafsi naona tunahitaji mapinduzi makubwa katika kila sekta, tatizo ninaloliona ni uoga, hata kwa wasomi wenyewe kuhusu nafasi zao mara baada ya mabadiliko. na kwa mambo ya kulindana yalivyo, tusitegemee jipya. mizee ikihisi mtu anataka kuleta mabadiliko, basi huyo mtu atafanyiwa hila mpaka basi. inauma sana, wacha wasomi tuendelee kufagia mabanda ya kuku kwa sababu ya woga wetu na kudhani kwetu kuwa mambo mengi hayatuhusu tumeruhusu watu wap.uzi na wehu kutuongoza.
 
Top Bottom