CCM, CCHADEMA jino kwa jino Bungeni

SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,955
2,125
CCM, Chadema ‘kubanana’ bungeni Jumatano
Send to a friend
Saturday, 11 June 2011 20:37


Ally Mkoreha, Dodoma
WAKATI mjadala kuhusu bajeti ya serikali katika mwaka wa fedha wa 2011/12, ukitarajiwa kuwa mkali ndani ya Bunge, kufuatia hatua ya awali ya Kambi Rasmi ya Upinzani, kupinga bajeti hiyo kwa maelezo kuwa haikutoa unafuu wa maisha ya wananchi wa kawaida, wabunge wa CCM wamesema wamejipanga kuitetea kikamilifu.

Habari zilisema wabunge wa chama hicho kinachoongoza serikali, walikutana juzi katika kikao cha kamati yao ambayo Mwenyekiti wake ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.Katika mkutano huo wabunge hao waliweka mikakati jinsi ya kutetea bajeti hiyo, iliyowasilishwa bungeni Jumatano iliyopita na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo.

Katika hotuba yake, Mkulo alisema bajeti hiyo imelenga kuwapunguzia wananchi, makali ya maisha na kwamba, ndiyo maana serikali imeondoa tozo mbalimbali za mafuta na kufuta kodi kwenye pembejeo za kilimo.
Alisema kupanda kwa bei ya mafuta, ni moja ya mambo yaliyosababisha ugumu wa maisha miongoni mwa wananchi.

Hata hivyo siku moja baada ya kuwasilishwa kwa bajeti hiyo, kambi ya upinzani kupitia kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, iliibuka na kuiponda kuwa ni bajeti hewa haikulenga kuwasaidia walalahoi kama ilivyoelezwa na serikali.

Hatua hiyo ilisababisha Waziri Mkulo kuibuka mjini hapa na kuwaeleza waandishi wa habari kuwa, Zitto amepotosha umma kujitafutia umaarufu wa kisiasa.

Hali hiyo inaashiria kuwapo kwa mvutano kati ya wabunge wa CCM na wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inayoongozwa na Chadema katika mjadala kuhusu bajeti itakayojadiliwa kuanzia Juni 1 5 hadi 21, mwaka huu.

Wakizungumza na Mwananchi jana kwa masharti ya kutotajwa, baadhi ya wabunge wa CCM walithibitisha habari kuhusu kuwapo kwa kikao cha kamati yao na kwamba, kilikuwa na lengo la kuweka msimamo wa pamoja kuhusu kutetea bajeti.

"Ni kweli jana (juzi) tulikuwa na kikao cha Kamati ya Wabunge wote wa CCM, kuweka msimamo wa pamoja kutetea bajeti yetu. Tumejipanga vilivyo kuwakabili wapinzani wetu na tuna uhakika kwa kuwashinda katika mjadala huo kwa sababu bajeti yetu ni safi na wao wanaikubali ingawa kwa tabia yao, wanaipinga,” alisema mmoja wa wabunge hao.

Lakini akizungumzia majigambo hayo ya wabunge wa CCM, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, alisema: Wabunge wa CCM watashinda kwa kupiga meza na kuzomea, ni mabingwa katika hayo lakini siyo hoja, kila mtu anajua hilo.
Source: Mwananchi
Hivi wabunge wetu wana mpango gani na sisi wananchi? Kwao vyama ni muhimu kuliko maisha bora kwa wapiga kura? Ndio maana nasema alaaniwe aliyepindisha hukumu ya Mgombea binafsi
 
Jino kwa jino vipi wakati msemaji wa kambi ya upinzani bungeni na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kasema bajeti safi
 
Jino kwa jino vipi wakati msemaji wa kambi ya upinzani bungeni na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kasema bajeti safi

una uhakika ndugu yangu kuwa ameikubali?mimi sina uhakika kwa hilo,tatizo la wanadamu tumeathiriwa na ubinafsi hivyo kila anayeangalia bajeti anaongelea mstari mmoja unaomhusu lakini anashindwa kuelewa kuwa maisha ya mwanadamu ni muunganiko na mwenzako (network),hivyo anapoumia mwenzako wewe kwako inaweza kuwa haikuhusu au mwenzako anapopata unafuu wewe unaumia hivyo ni bora kuiangalia bajeti kiujumla wake,kwa upande wangu ni bajeti ya kisiasa badala ya kiuchumi na kijamii.
 
Jino kwa jino vipi wakati msemaji wa kambi ya upinzani bungeni na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kasema bajeti safi
kama alinena hivyo amekosea kwa ujumla hamna kitu hiyo bajeti usanii mtupu,kama wanania kwel na maisha ya wanyonge isipitishwe sababu hamna sehemu yeyote ya kubana matumizi mfano mafuta kodi imepunguzwa kias gan?den la taifa linazid kuongezeka,hawapo makin watungao bajet mfano fain barabaran inatengeneza mianya ya rushwa.tuachana ushabiki usio na tija.
 
Jino kwa jino vipi wakati msemaji wa kambi ya upinzani bungeni na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kasema bajeti safi

Bajeti ni kipimo tosha kwa uwezo wa wabunge wa CCM, tumejiandaa kusikia maneno ya naunga bajeti kwa 100% na malalamiko kidogo.

CCM haina wenye akili ya kufikiri. Wanafikiri pamoja kama kondoo.
 
Nina hamu ya kusikia zomeazomea,tena wengi watakaozomea ni wale wa viti maalum,na wale waliopita kimagumash kama vile KIGWANGALA.......na vilaza wengine wenye NIDHAM YA UWOGA
 
Jino kwa jino vipi wakati msemaji wa kambi ya upinzani bungeni na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kasema bajeti safi

Mkuu si unajua Mbowe si msomaji mzuri bana, mwanzoni alidhani bajeti ilikuwa nzuri sana lakini baada ya kupewa madesa na vijana, sasa nae ameona bajeti ni mbovu kabisa, haa ha ha ha....
 
Back
Top Bottom