CCM Bukoba mjini watimuana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Bukoba mjini watimuana

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Oct 22, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Lilian Lugakingira, Bukoba

  HALMASHAURI ya CCM, Wilaya ya Bukoba mjini, imewasimamisha kushiriki katika kampeni za chama hicho, viongozi watano, akiwemo mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) wa wilaya hiyo mjini, Murungi Kichwabuta.

  Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Robert Bahati alitaja viongozi wengine wa chama hicho waliosimamishwa wasishiriki katika kampeni za chama hicho kwa madai ya kukihujumu chama kuwa ni mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM taifa, Abdalah Kichwabuta na Pius Kaijage ambaye ni katibu wa CCM , Kata Kahororo.


  Bahati aliwataja wengine waliosimamishwa kuwa ni Sylivanus Muhyoza aliyekuwa diwani wa Kata Kahororo kipindi kilichopita na Udi Miruko katibu mwenezi CCM Kata Bilele.


  Alisema wanachama hao wamezuiliwa kujihushisha na kampeni za chama hicho juzi na halmashauri ya CCM wilaya ya Bukoba mjini baada ya kubainika kukihujumu chama katika kampeni zinazoendelea kwa kupinga wagombea wa CCM.


  Mwenyekiti huyo wa CCM Bukoba mjini alisema kuwa pamoja na kusimamishwa wasihusike katika kampeni, wanachama hao wataendelea kuwa chini ya uangalizi wa chama hicho.


  Alisema pia baadhi ya wanachama hao wamejihusisha na vitendo vya kufanya kampeni ya umeya wa Manispaa ya Bukoba kabla hata ya uchaguzi wakati meya huchaguliwa na madiwani.


  Imedaiwa kuwa wanachama hao wanapita kwa wagombea udiwani ambao wanaonyesha uelekeo wa kushinda na kuwaomba wakichaguliwa wamchague tena Samwel Ruangisa ambaye alikuwa meya katika kipindi ilichopita, ili aendelee na wadhifa huo.


  Hivi karibuni uongozi wa CCM Bukoba mjini, mbele ya mke wa mgombea urais wa CCM mama Salma Kikwete, uliwatuhumu Samwel Ruangisa ambaye pia anagombea udiwani katika kata Kitendaguro na Murungi Kichwabuta mwenyekiti wa UWT Bukoba mjini kuwa wanakihujumu chama na watakikosesha kura.


  Chanzo: Mwananchi
   
 2. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  :A S-fire1:Na bado.
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280

  (Utasikia) Mwananchi wachochezi.
   
 4. minda

  minda JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  hapo lwakatare tu; kwani hata wakati wa ule 'mwenge wa vijana' alisifiwa sana.
   
 5. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  hiyo ni homa ya rwakatare...! kaazi kweli kweli...........
   
 6. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2010
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Huu ni ugomvi unaomuhusisha Mzee Ruangisa na kampeni za umeya na wala haijabadili upepo wa kampeni za ubunge, Lwakatare asijipe matumaini yasiyokuwepo.
   
 7. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #7
  Oct 22, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  ccm wamekwisha elekea Kibra, wamekaa mkao wakuliwa, hatuna wasiwasi nao, tunajielekeza kuwamaliza 31 October
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Oct 22, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Huo ugomvi wa umeya unaweza ukawasaisia wapinzani.
   
 9. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #9
  Oct 22, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  mbona hata CCm taifa watatimuana come november.
   
 10. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  kaaaz kwelikweli
   
 11. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #11
  Oct 22, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kuna mengi nyuma ya issue hii ambayo hatuyajui.
  Hata hivyo kushindwa kwa sisi m Bukoba mjini ndiko kunawapa homa viongozi wa jimbo hilo. Na sasa wanatafuta mchawi kabla mgonjwa hajafa.

  Kama mwenyekiti Robert Bahati ambaye binafsi amegombea udiwani mara nyingi na kushindwa na upinzani akiweza kutuambia mbona ushirikiano wa Kagasheki na watendaji wa chama chake ni wa kutia shaka katika kipindi hiki chote cha uchaguzi, nitakuwa wa kwanza kumpiga mawe mwizi wa ushindi wa wao sisi m.

  Imefikia mahali Kagasheki anasema wazi bila yeye sisi m Bukoba ilikuwa haipo. Na alikuja kama mwokozi wao.
   
Loading...