CCM bila rushwa hakuna ushindi' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM bila rushwa hakuna ushindi'

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 19, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280

  [​IMG] Ndesamburo alisema hayo alipotakiwa na gazeti hili kutolea maoni kauli ya Rais Kikwete kuwa wanasiasa wanaokusudia kutoa, kuomba au kushawishi rushwa katika uchaguzi ujao, watakiona.

  "Hakuna kitu kipya. Hayo ni maneno ya kisiasa. Rushwa zimekuwepo siku zote. Takukuru wamekuwepo wakati wote. Hakuna hata siku moja tumewaona wamekamata mtu kwenye chaguzi," alisema Ndesamburo.

  Mbunge huyo ambaye ni mfanyabiashara, alienda mbali zaidi akisema "Bila rushwa CCM haiwezi kushinda kwenye uchaguzi. Hii kupambana na rushwa ni kiinimacho."

  Alipotakiwa kueleza mbinu anazozitumia yeye kushinda uchaguzi mwaka 2005 licha ya CCM kugawa rushwa alisema "Nilishinda kwa kura za chuki. Wale wanaopewa rushwa wanawaeleza wenzao hivyo wale ambao hawakupata mgawo, walikasirika na kunipigia mimi."

  Alisisitiza kwamba CCM haiwezi kuwahonga wapigakura wote, hivyo anaamini hata akipata mpinzani mwenye fedha kiasi gani kupitia chama hicho tawala, atagonga ukuta tu maana wengi wanampenda yeye kutokana na uchapa kazi wake na isitoshe wapo waadilifu wasiopokea hongo.

  Kitendo hicho cha Rais Kikwete kutangaza vita na wanasiasa wanaokusudia kutoa, kuomba au kushawishi rushwa katika uchaguzi ujao, kimeonekana kuwa ni mtihani kwa CCM ambayo sasa imepanga kuendesha semina nchini nzima kwa wanachama wake kuwanusuru.

  Juzi Rais Kikwete alisema atasaini kwa mbwembwe sheria ya matumizi ya fedha katika uchaguzi na kuwaonya watakaojihusisha na rushwa katika Uchaguzi Mkuu ujao kwamba, watakumbana na mkono wa dola.

  Jana Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya CCM, Itikadi na Uenezi, John Chiligati alisema kwamba wana-CCM hawana haja ya kuwa na wasiwasi kwa sababu chama kitawaelimisha kupitia semina mbalimbali.

  Chiligati ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema mchakato wa semina hizo utaanza kufanywa baada ya Rais Kikwete kusaini sheria hiyo.

  Alisema CCM ndiyo iliyofanikisha mpango wa kupitishwa kwa sheria hiyo ya matumizi ya fedha katika uchaguzi na imekusudia kuwaelimisha wanachama wake ili kuepuka lawama kwani, atakayekwenda kinyume na sheria hiyo, asitegemee msaada wa chama.

  Chiligati alipuuza madai ya baadhi ya makada wa CCM walioeleza kuwa sheria hiyo itakosa nguvu kwa kuwa ni kawaida kuwa na makambi katika chaguzi akisema, "Kambi huwezi kuzikwepa kwani kila anayetaka kuteuliwa huwa na watu wa kumsaidia, lakini, kinachotakiwa ni pande zote za makambi hayo kuheshimu maadili."

  Alisema sheria hiyo pia haiwezi kukosa nguvu kwa sababu ya uwezekano wa kambi hizo kusingiziana kwani dola ipo na ndiyo itakayopaswa kuchunguza kwa ajili ya kujua ukweli.

  Chiligati ambaye pia ni Mbunge wa Manyoni Mashariki, alisisitiza kwamba sheria hiyo haiwezi kulea vurugu wakati wa uchaguzi ndani ya CCM bali itakiimarisha umoja na kukikifanya chama hicho kizidi kuwa na nguvu.

  Naye Mbunge wa Maswa John Shibuda alisema kwamba sheria hiyo itaisaidia CCM kupata viongozi bora baada ya kuwazuia matajiri wanaotaka kutumia fedha zao kujipatia madaraka ila akaonya kwamba CCM inapaswa kuwa makini na kambi zinazoanzishwa kwa ajili ya uchaguzi huo

  Mbunge wa Vinjo, Aloyce Kimaro alisema kwamba sheria hiyo itaisaidia sana CCM kwa sababu kuna baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM ambao wamekuwa wakizifanya kura za maoni kama mradi wa kuvuna pesa kutoka kwa wanaowania uongozi.

  Mbunge wa Urambo Magharibi, Lucas Selelii amemtaka Rais Kikwete kuchukua hatua za mfano ili kuwakomesha wanaojihusisha na ununuzi wa kura katika chaguzi.

  "..Rais asiishie tu kutangaza vita, aonyeshe vitendo kwa kuchukua hatua za mfano na hapo wenye tabia hizo chafu watakoma. Wakiona mwenzao fulani katupwa jela wataogopa, lakini si kwa maneno tu," alisema Selelii na kuongeza:

  ∜ Wakati sasa umefika kwa rais kuwa mkali zaidi kuhusu masuala hayo. Tazama kwa mfano sasa watu wanagombania majimbo utazani yao, wanamwaga fedha hata kabla ya kampeni. Wanatoa wapi fedha hizo, kama kusaidia kwa nini wasisaidie miradi ya maendeleo ya jimbo. Rais aongeze ukali kwa hili achukue hatua.

  Mwanasiasa mkongwe nchini, Peter Kisumo alipongeza hatua ya Rais Kikwete kusimama kidete kuhusu kuhakikisha matumizi ya rushwa na hongo yanakomeshwa kuanzia Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba.

  Hata hivyo, Kisumo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa CCM alitahadharisha kuwa itakuwa ni makosa makubwa utekelezaji wa suala hilo kuachiwa Takukuru wenyewe.

  Kisumo alitoa kauli hiyo jana katika mahojiano maalumu na Mwananchi, huku akisisitiza kuwa itakuwa ni kosa kubwa kama Watanzania, vyama vya siasa na vile vya kiraia vitaibebesha mzigo Takukuru yenyewe.

  "Vita hii aliyoitangaza Rais wetu isiachiwe Takukuru na asasi za kiraia pekee kwamba ndizo zipambane na rushwa hapana∦CCM nacho kinatakiwa kuonyesha mfano wa kivitendo kuanzia chaguzi zake za ndani,"alisema.

  Kisumo alisema suala la baadhi ya Watanzania kuwaomba rushwa wagombea au wagombea wenyewe kutoa takrima kwa wapiga kura ni jambo linalotaka sasa kuwa utamaduni wa Mtanzania jambo alilosema ni la hatari.

  Mwanasiasa huyo alisema ipo mifano nchi nzima hivi sasa ya wanasiasa wanaotaka kuwania ubunge hususan kupitia CCM kuwaita viongozi mbalimbali kuanzia ngazi ya mashina na kata na kuwakirimu ili wawafanyia kampeni.

  "CCM kina wafuasi wengi na ndicho kinachosikilizwa na Watanzania wengi sasa tukionyesha mfano wa kumuunga mkono Rais nina hakika anachokisimamia Rais kitatekelezeka na katika hili, tuache unafiki,"alisisitiza Kisumo.

  Kisumo alitolea mfano wa tukio la mwaka jana huko Mwanga la baadhi ya wanawake kutaka mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Anne Kilango Malecela awalipe nauli na posho ni dalili kuna tatizo ndani ya CCM.

  Mwanasiasa huyo alisema kama sheria hiyo mpya itapokelewa kikweli kweli na Watanzania na viongozi wa kisiasa ana imani kuwa Taifa la Tanzania litapata viongozi waadilifu na hata suala la ufisadi litatoweka.

  Alisema kuwa Tanzania inakosa viongozi waadilifu kutokana na mfumo wenyewe wa kupata viongozi hao kuwa na matatizo kutokana na kuruhusu kuwepo kwa mianya ya wagombea wanaonunua uongozi kwa fedha.

  "Tukiruhusu tupate viongozi wanaonunua uongozi tutakuwa ni taifa la hovyo ∦.tusiruhusu kuwa na viongozi ambao ni criminal minded (wenye mawazo ya uhalifu) na kwa kweli kwa hili namuunga mkono rais,"alisema Kisumo.

  Mwenyekiti wa Taifa wa TLP ambaye tayari ametangaza kugombea ubunge katika jimbo la Vunjo, Augustine Mrema alisema kama mgombea wa CCM atakayesimamishwa hatajihusisha na rushwa, anaamini atashinda.

  "Mimi naunga mkono mkakati wa Rais Kikwete na naomba Takukuru wakafungue kitua chao kule Vunjo, naamini watasaidia wananchi wengi wanaonipenda niwe mbunge wao wasirubuniwe," alisema Mrema.

  Alielezea kufurahishwa na mkakati wa Kikwete, akisema atakapokuwa kwenye kampeni za kuwania jimbo hilo atawataka wapigakura waelekeze kura zao Rais kwa Kikwete.

  Kwa mujibu wa Rais Kikwete juzi kupitishwa kwa sheria hiyo mpya ni jambo la kihistoria na ni hatua ya kimapinduzi kwa kuwa itasaidia kudhibiti rushwa na kuzuia taifa lisifike mahali pabaya.

  Alibainisha kwamba, hali inaonyesha kuwa mbaya zaidi sasa kutokana na rushwa katika uchaguzi kuanza kuwa tatizo kubwa, hususani katika mchakato wa kuchagua wagombea wa chama wakati wa kura za maoni.

  Kikwete ambaye alikuwa akizungumza kwa furaha aliwaagiza makamanda wa Takukuru kuanza kujipanga kufanya kazi ya kudhibiti wanunua uongozi na kubainisha kuwa tayari kuna wagombea wameshaanza kupita mitaani wakigawa mipira na wengine kukarabati ofisi za CCM.

  "Anzeni sasa kujipanga kuifanya kazi hiyo kwani naambiwa wanunuaji wa uongozi wameshaanza, wengine wanapita na kugawa mipira na wengine wanakarabati majengo ya ofisi za CCM.

  Sheria inaruhusu kudhibiti rushwa kabla na wakati wa kura za maoni ndani ya vyama vya siasa na wakati wa uchaguzi, nawaomba muanze kufuatilia na kuchukua hatua zipasazo," aliongeza.

  Akielezea kuhusu na sakata la rushwa katika uchaguzi, Rais Kikwete alisema: "Rushwa kubwa kwenye uchaguzi ipo wakati wa kura za maoni katika vyama pengine hata kuliko wakati wa uchaguzi wenyewe na kuahidi kuwa yeye kama rais yuko tayari kufanya kila linalowezekana ili kuiwezesha Takukuru kufanikisha kazi ya kudhibiti vitendo hivyo na kuwataka waanze kazi hiyo sasa.

  Aliasa kuwa rushwa katika uchaguzi imeanza kukomaa na iwapo hatua hazitachukuliwa, una hatari itageuza uongozi kuwa bidhaa ya kununuliwa kama shati, au njugu jambo ambalo alisema ni hatari kwa vile hata mwendawazimu akiwa na fedha anaweza kuununua.

  Habari hii imeandaliwa na Leon Bahati, Exuper Kachenje na Daniel Mjema, Moshi

  CHANZO: MWANANCHI
   
 2. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hizi ndo siasa za TZ
   
 3. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,850
  Trophy Points: 280
  Musawada wenyewe ni kama umeshinikizwa toka nje ndio maana umesainiwa kwa publicity kubwa.Iko miswada mizito zaidi amabayo rais ameshawahi kusaini lakini haikuwa na media frenzy and hype kama huu.
   
 4. M

  Mkereme JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wewe Safari ni Safari!
  Kwani mpaka leo hii hujamshtukia mkulu kwamba ni msanii? Unakumbuka alivyokua akimwapisha Hosea Edward kwa mbwembe and after a few months the PCCB boss sexed the Richmond report akaibadilisha na Jakaya alipelekewa two copies the original and the sexed one na Kamati ya Bunge ikamtuhumu na hadi leo anapeta and you fools believe that hako kasheria kalikopitishwa feki katafanya kazi? Even the Chief Justice, His exellency Agustino Ramadhani is very unsure how the law can be interpreted in the courts and you cheer your president with mdundiko?? Tatizo ni kwamba ukimkataza mtu asipite sehemu fulani you must show him the way out vinginevyo ni sawa na kufukuza upepo. Hata kule mlikodesa hiyo sheria I mean the USA wagombea urais wanapewa public funds and you must not exceed the ceiling or you raise your own tatizo the option haina limit ya funds so changanyeni akili hapa CCM chini ya Jakaya wanawachezea shere tu shauri yenu Watz!!!! Fumbo mfumbie mjinga mwerevu hungamua nyie endeleeni kujiandikisha kupiga hiyo kura feki as you have been doing for the past 45years. For sure itakula kwenu. Niwachekeshe huko nyuma enzi za Mkapa ilipitishwa sheria ya kutokuvuta sigareti hadharani its over 6 years plus nasikia kanuni za utekelezaji wa sheria hiyo hazijatolewa na Waziri husika and todate sijasikia mtu amekamatwa na kufikishwa kwa pilato therefore you can have a law in the statutes books but kama haitekelezeki then ni bora isingekuwepo kwa sababu it doesn't make any difference
   
Loading...