CCM bado ina ndoto ya kuwaletea Watanzania maendeleo?

Tikerra

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
1,702
146
Tulipata uhuru mwaka 1961.Sina hakika kama ulikuwa uhuru wa bendera au uhuru wa kweli kwa sababu kwa jinsi mambo yalivyo kwenda :Julius kuruhusiwa kuendesha harakati za kutafuta uhuru almost freely, kuruhusiwa kiulaini kwenda UN kuhutubia manyan'gau yale,na hatimaye eti akaya-convince yaipe Tanganyika (wakati ule)uhuru inatia shaka.Ni kama kitu kilichopangwa hivi na kukubaliwa mapema.Baada ya kupata uhuru jamii ya Kitanzania iliahidiwa maendeleo,lakini mambo mengi hasi yalitokea, ambayo badala ya kuleta maendeleo kwa Watanzania, jamii yetu ilizidi kudidimizwa katika umaskini ambao hata wakati wa mkoloni haukuwahi kuonekana.Mwaka 1967,Azimio la Arusha lilitangwazwa.Kinadharia Azimio la Arusha lilitazamiwa kuleta neema kwa watanzania.Lakini it was too Utopian kiasi kwamba tafakuri kidogo tu ingetosha kukuambia kwamba ile haikuwa njia sahihi ya kumletea Mtanzania maendeleo.Hiki nacho kikawa kama kitu kilichopangwa kiwarudishe Watanzania nyuma.Chini ya Azimio la Arusha,Watanzania tukaingia katika shida zisizo tamkika.Mali za watu ikiwa ni pamoja na makazi na mashamba vikaharibiwa.Watu wakaingia kwenye umaskini wa kutisha.Vitu visivyo sustainable vikaanzishwa kama viwanda,mashamba ya serikali nk.Mambo hayo hayakuwa na misingi sahihi ya kiuchumi,na at the end of the day kama wengi tulivyotegemea, mbio hizo zikaishia sakafuni.Kama hiyo haikutosha,Tanzania ikaingia kati vita iliyoitwa vita ya Kagera.Kama vita hii ilikuwa lazima sijui,lakini kwa maoni yangu haikuwa lazima.Nadiriki kusema kwamba siasa zetu za kijinga ndizo zilizotuingiza katika vita hii. Baada ya vita, Watanzania wakaingia katika mtikisiko mkubwa wa kiuchumi na kwa mara nyingine tena Watanzania wakaingia katika umaskini mbaya usiosimulika,hata kuliko ule wa mwanzo,wale wazee watakumbuka.Tukaambiwa tufunge mikande kwa miezi kumi na nane,matatizo yetu yatakwisha,lakini baada ya miezi kumi na nane ya kufunga mikanda,shida za Watanzania zikazidi, tena mara hii maradufu.CCM iliyoahidi mwaka 1961 kwamba itawaletea Watanzania maendeleo, kwetu sisi tulio wengi mpaka wakati huu ilionekana wazi kwamba imeshindwa.Aibu na kunyooshewa vidole Julius kulimfanya aachie ngazi.Lakini kwa mara nyingine tena mkakati ukawa ule ule kuzidi kuwarudisha nyuma Watanzania katika maendeleo yao.Sote ni mashahidi kwamba baada ya Julius mazungumzo na vitendo vimekuwa tofauti kabisa.Mipango mingi imebuniwa, eg.Maendeleo ya miaka mitano,MKUKUTA,MKURABITA,Kilimo Kwanza nk. huku wahusika wakijua fika kwamba mipango hiyo ni hewa na haiwezi kuwaletea Watanzania maendeleo.Matokeo yake yako wazi kwa mwenye akili timamu ,Watanzania wamezidi kuwa maskini.Ushirikiano wa awamu mbalimbali hasa ya pili, ya tatu na ya nne na mashirika ya kimataifa na nchi za magharibi kama USAID,IMF,World Bank nk. ambayo kwa mtu mwenye akili timamu nia yao iko wazi,ie.kurudisha nyuma nchi yetu na nchi zote zinazo endelea kimaendeleo unatia shaka.Huwa najiuliza hivi serikali ya TANU/CCM haijui nia halisi ya mashirika haya kwa nchi zinazoendelea,au ni washirika wao katika nia yao chafu ya ku-underdevelop Watanzania?Naamini ni wadau na washirika wa mashirika hayo.Kwa vile kama wasingekuwa wadau wangestuka na kusitisha mahusiano yote na nchi hizo na mashirika hayo.Tanzania ni nchi tajiri mno,hatuhitaji msaada katika maendeleo yetu.Nina ujasiri wa kusema kwamba ukoloni tulio nao leo ni mbaya zaidi kuliko ukoloni wa Mjerumani.Watanzania wenzetu wametufanya watumwa wao,sisi tunafanya kazi,wao wanakula.Watanzania ni lazima sasa tuseme enough is enough.Watanzania leo hii maisha yao ni magumu,ni maskini wa kutupwa, hawana matumaini tena,wamekata tamaa kabisa.Katika hali hii CCM inapata wapi ujariri wa kuomba tena ridhaa ya wananchi kuiongoza Tanzania?Ni vema CCM kwa nia njema kabisa, ikabuni mikakati ya kuachia ngazi 2015.Viongozi wake wataheshimika zaidi katika jamii ya Watanzania.
 
Back
Top Bottom