Ninafuatilia kwa makini mnyukano wa siasa za Tanzania, NCCR ilikuwa tishio kwa chama tawala, CUF ikawa tishio na sasa ni zama ya CHADEMA
Ninachokiona mbinu zote zilizotumiwa na CCM huko nyuma kuzorotesha upinzani zimekwama haziwezi tena kufanya kazi kwa CHADEMA, ndiyo maana kinachoendelea sasa ni siasa nyepesi kwa kifupi ni siasa za majungu zisizokuwa na tija,
Na zaidi nimetafakari sana na kufikia hitimisho kuwa humu kwenye jukwaa zaidi ya 90% ya members wake sio wanasiasa ni wapika majungu tu, labda hiyo 10% inayobakia wanaweza kuthubutu kujiita great thinkers. watu wanatumia muda mwingi kujadili maisha ya mtu binafsi badala ya kujadili chama kwa ujumla wake kama Taasisi.Kwa mtu yoyote makini hawezi kufanya biashara mbovu hiyo isiyolipa.
Ni ushauri wangu na mtazamo wangu kuwa kama kweli tuna uchungu na taifa hili tujadili fikra na mstakabali wa taifa letu kwa ujumla wake badala ya kujadili watu
Kwa wana ccm je huu ni wakati kwenu kuzungumzia uchaguzi wa CHADEMA na ku target katibu wa chama kuwa ndo tatizo "simple mind always discuss people but complex mind discuss ideas" ni msemo uliozoeleka sana, Nawauliza wanaccm je huu ni wakati wa kujadili watu wakati chama chenu kinadhoofu na wala hamna mpango wa kukijenga, Mnavizia CHADEMA kiingie haraka haraka kwenye uchaguzi mkidhani utatokea mpasuko wa kuinufaisha CCM,
CHADEMA ni chama makini, na kimtazamo viongozi wake ni makini sana wala uwezi ukalinganisha na viongozi wa CCM. Pia wanachama wake ni makini , kimsingi ni watu wanaojitambua. Kwa propaganda pamoja na matumizi mabaya ya dola ili kuiboa CHADEMA, hakika kisingekuwa chama makini na viongozi wake kuwa makini mpaka sasa ingekuwa ni historia, kingekuwa kimefutika kabisa kwenye ramani ya siasa za Tanzania . Nakifananisha CHADEMA na kisiki cha mpingo hakika hamtakiweza kwa propaganda dhaifu hizo na matusi mnayotukana humu jukwaani
Ushauri wa bure kwenu wanaccm kijengeni chama na mjaribu kurudisha imani iliyopotea, Chama chenu kwa sasa hakina mvuto kwa wananchi walio wengi