CCM and UDASA, this is shameful

CCM and UDASA, this is shameful

Tumaini Makene

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2012
Posts
2,650
Reaction score
6,085
Si kwa taasisi hizo pekee, bali pia watu wenye majina na hadhi katika jamii walioshiriki au kuingizwa kwenye mkakati ulioandaliwa kwenye mdahalo wa leo Chuo Kikuu Dar es Salaam, wakiwemo baadhi ya wachangizaji maada!

Hatuwezi kukaa kimya iwapo inafikia mahali CCM wanatumia kidhalili taasisi za elimu tena zinazohusiana na kiwango cha chuo kikuu kwa kiwango kinachotaka kufanyika leo.

Ilianza kama tetesi. Lakini sasa ni dhahiri with facts, kuwa mmoja wa viongozi wa juu wa UDASA mwenye uhusiano wa kikazi na CCM, ameshirikiana na chama hicho kukodi vijana kwenda Ukumbi wa Nkrumah, UDSM kwenye mdahalo unaorushwa live na Star TV.

Ingelikuwa jambo la heri na labda kujivunia iwapo UDASA ingeingizwa Kwenye mchezo huo mchafu na aibu kwa wasomi, wanataaluma na wanazuoni, endapo tu vijana hao wangekodiwa kwenda kujifunza au kutoa mchango wao kama Watanzania.

The shameful condition is...vijana hao wengi kutokea maeneo ya Buguruni, Dar ea Salaam, waliokodiwa kwa kulipwa hela na kubebwa kwa kutumia mabasi ya ile kampuni ya umma iliyouzwa kifisadi, wamechukuliwa kwa kazi moja tu, kwenda kuzomea! That is shameful...could have been a last thing to be done by an institution like UDASA to its breathing the last!

This is how you honour people like Prof. Chachage or Prof. Haroub or Walter?

This is how you guys at UDASA in collabo with the regime of the day now are transforming the Walters', Chachage's or Haroub's dreams for this country through serious discussion and debates at the Hill?

Mkakati huo wa CCM na ki-CCM umelenga kutaka kuweka precedence (bad of course) na kulazimisha hoja za CCM za kuchakachua Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya wakati BMK linakwenda kuanza Agosti 5, mwaka huu!

Umepangwa kwa namna ile ile ulivyopangwa mkakati ule uliofanywa na Serikali ya CCM kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kukodi vijana waliokwenda kutukana matusi ya ajabu hadi kuwatakia kifo akin a Mzee Warioba na wenzake kwenye Tume ya Mabadiliko!

It becomes even more shameful when it involves those whom, we, the people of this noble nation, could trust them as intellectuals of our times!

Wangelikuwa wamefanya CCM kama ambavyo wananchi wamewazoea (kuhonga na kubeba watu kwenda kwenye shughuli yoyote ikiwemo mikutano yao tusingehangaika. Maana ni sawa na kumtoa samaki majini kisha ukategemea aishi!

Kuhusisha taasisi ya wanataaluma na wanazuoni, tena chuo kikuu ni aibu ambayo hakuna Mtanzania makini atainyamazia.

Waacheni watu watoe maoni yao naturally na automatically! Yawe ni ya kuunga mkono UKAWA au CCM au kutounga upande wowote! Kwanini kupanga au kuleta mercenaries kwenye midahalo au majadiliano! Kwanini CCM haioni aibu kujianika wazi kila siku kuwa imeporomoka na haina kabisa ushawishi wa kisiasa tena kwa Watanzania!


Tutaweka facts zaidi...

Wasalaam

Makene
 
Makene...

Ni kwa nini Tundu Lissu asingekataa mwaliko?...

Ilishaelezwa hapa nini CCM wanafanya kuhusiana na Kongamano hilo...Nimeshangaa sana kuwaona Lissu, Machali , Kafulila na wajumbe wengine wa UKAWA kama sehemu ya Kongamano hilo...
 
Aibu kubwa kuliko zote ni kuiba wake za watu,unaleta porojo zako ambazo hazina kichwa wala miguu.
 
Makene...

Ni kwa nini Tundu Lissu asingekataa mwaliko?...

Ilishaelezwa hapa nini CCM wanafanya kuhusiana na Kongamano hilo...Nimeshangaa sana kuwaona Lissu, Machali , Kafulila na wajumbe wengine wa UKAWA kama sehemu ya Kongamano hilo...
Wakikataa wataenda kuuza sura wapi wakati unajua kuwa wao ni wazee wa kuuza sura kwenye vyombo vya habari.
 
attachment.php



Haya maandalizi aliyakataa Kitila Mkumbo jana

Hapo CCM inawashusha watu wake
 
Makene...

Ni kwa nini Tundu Lissu asingekataa mwaliko?...

Ilishaelezwa hapa nini CCM wanafanya kuhusiana na Kongamano hilo...Nimeshangaa sana kuwaona Lissu, Machali , Kafulila na wajumbe wengine wa UKAWA kama sehemu ya Kongamano hilo...
Balantanda

Ukweli huwa unajitenga...let them do Mkuu. Hila au uovu haujawahi kupambana na haki au dhamira njema ukashinda.

Ndiyo maana mambo kama haya yanajulikana!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Makene lalamiko lake limesikika na wengi walishakuwa na wasiwasi na hili kongamano tangu lilipotangazwa kuwa litafanyika,ushauri Wangu waacheni waandae Hayo makongamano kwa jinsi wawezavyo maana si uhaini,ninachojua ni kuwa Mtanzania wa leo si yule wa enzi zile,atasikiliza,atachambua kisha ataamua....... Nawapongeza Wapinzani walioshiriki kwenye hilo kongamano maana wamepata jukwaa la kuzidi kumuelimisha Mtanzania.
 
Mkuu Tumaini Makene

UDASA ya leo ni Mashambembenga ebu jikumbushe Mwanyekiti wake alichofanya katika Bunge la Katiba

Ndugu yetu, Daktari wa Filosofia uliyetumainiwa na wenazako hata ukasimamia Chama cha Magwiji wasomi UDSM (UDASA), yaani ndani ya viatu vya kina Prof Chachage, Leo hii bila hiana, unakacha misimamo wako Wote, unakumbatia misimamo wa watu wengine na kutumia hoja dhaifu kuutetea! Umenishtua sana!

Inakuwaje licha ya kushiriki kikamilifu mijadala yote rasimu ya kwanza na rasimu ya pili, kushiriki na kuandika mawazo ya kitaaluma, yaliyowakilishwa kwenye Tume, Leo hii unayakimbia! Wewe na wenzako mmedanaganya Tume, mlijenga hoja nzito mkaziweka kwenye kijarida na kuwakabidhi Tume, sio Mara moja Bali Mara mbili, Tume ikazikubali, Leo unawajeuka? Leo unahoji dhana iliyotumika katika utafiti, eti 'sampling'? Mbona hata Mara Mmoja hukusita wala kuhoji Tume ilitumia dhana gain katika utafiti wake? Kweli Michael, umepewa nini Hadi ukubali kuonyesha na kujidhihirisha mbele y kadamnasi yote kuwa unaweza ukawa msaliti kiasi hicho?

Wana Jamvi namhoji Huyu Ndugu yangu maana yeye huko nyuma wakati wa kukusanya Maoni Alikuwa mbele sana na hata kuonekana Kama shabiki wa Tume, na hoja nyingi zilizoko kwenye rasimu zinatokan na mawazo ya Wanataaluma wa Vyuo Vikuu vya Umma, Michael akiwa mojawapo wa viongozi Hao! Je tuwavumilie wakahaba wa hoja/taaluma? Je Kwa nini tusiamini kunmekuwepo na rushwa kubwa iliyoweza kuwashawishi wasomi wa aina ya Dr Francis na kina Prof Malymkono hata wasione Aibu mbele ya jamii Kwa kushabikia hoja wasioiweza kuiwekea mishiko?

kwa nini tusiibue hoja kuna rushwa inatembezwa ili kupata katiba? Je katiba itokanayo na rushwa sio rushwa Mara Mia zaidi. Ni nani atamjibia Dr Francis? Hivi atuthubutu kurudi na kusimama darasani anafundisha? Nchi yangu Tanzania inakwenda wapi?

Du, hata mimi nimesikitika sana kuona mwalimu anabwabwaja pumba yaani ccm inaweza kugeuza maji kuwa tope,

siamini na sijui ni nini kimemkuta mwalimu huyu, mwombeeni kwa mungu maana akiendelea hivi sifa ya wasomi inaharibika

Tatizo la Dr Francis Michael ni kuendekeza njaa. Huyu jamaa kwa sisi tunaomjua ana njaa ile mbaya. Anafundisha tuition hadi kwenye shule za kata.
 
Last edited by a moderator:
Chadema kuweni na akili...fuatilieni mdahalo...wachangiaji siyo CCM pekee.mbona ni watu wenye fikra tofauti?

Mmezoea fujo na kelele leo ni hoja tu.....Ninyi hamna fikra pana mnategemea ufuasi wa fikra za viongozi wenu ndo maana mnashindwa
 
Back
Top Bottom