CCM akili zenu finyu sana. Sasa tatizo hapo liko wapi?Malisa alitumia takwimu kuonesha kwamba Lowasa

PRODA LTD

JF-Expert Member
Oct 20, 2016
1,005
1,333
CCM akili zenu finyu sana. Sasa tatizo hapo liko wapi? Malisa alitumia takwimu kuonesha kwamba Lowassa anakubalika kiasi kidogo ndani ya CCM kuliko Dr.Slaa alivyokua anakubalika ndani ua CHADEMA.

Hoja ya Malisa ni kwamba Lowassa ndani ya CCM alikua anakubalika kwa chini ya 20% jambo ambalo lingempa ugumu sana kuongoza nchi hata kama angeshinda Urais kupitia CCM.

Maana ni kwamba 80% ya watu ndani ya CCM ambao walikua hawamuungi mkono wangemhujumu.

Huu ni ukweli ambao Lowassa mwenyewe aliujua. Sasa leo mnashangaa nini kwa hoja hii?

Naamini Malisa bado anayaamini haya aliyoandika na hajabadilisha msimamo. Hata Lowassa naamini anakubaliana na Malisa kwamba angeshinda Urais ndani ya CCM angepata wakati mgumu sana kuongoza nchi.

Lowassa alikua anakibalika sana na wananchi lakini alipata upinzani mkubwa sana ndani ya chama chake. Na hili lilidhihirika wakati wa uteuzi wa mgombea urais. Maamuzi ya CCM kumkata hayakufurahisha wananchi wengi.

Hii ina maana wananchi walikua wanamkubali lakini CCM walikua hawamtaki. Takwimu zinaonesha zaidi ya 80% ndani ya CCM walikua hawamtaki. Hiki ni kielelezo kwamba angefanikiwa kushinda Urais kupitia CCM angeshindwa kuongoza nchi maana kundi lisilomkubali (ambalo ni kubwa) lingemhujumu.

Hivi inahitaji degree kujua hiki alichokimaanisha Malisa? Acheni ujinga. Malisa alikua sahihi, yupo sahihi na atanaki kuwa sahihi kwa kauli yake hiyo.

Namna pekee ambayo ingeweza kumprove wrong Malisa ni kama Lowassa angeshinda urais kupitia CCM halafu aongoze nchi vizuri. Hapo ndipo hoja ya Malisa ingekuwa invalid (b'se alisema akishinda urais kupitia CCM atashindwa kuongoza nchi).

Lakini kwa hadi sasa kauli ya Malisa inaendelea kuwa sahihi. Na indicator mojawapo ni baada ya Lowassa kuamua kuhama CCM. It means Lowassa mwenyewe alijua anakubalika na wananchi isipokua chama chake hakimtaki. Ndio yaleyale aliyoongea Malisa kuwa CCM hawamtaki na wangempitisha agombee urais, wangeishia kumhujumu ili ashindwe kuongoza.

Nadhani vilaza mliofufua uzi huu mtakua mmenielewa.
Lowassa atashindwa kuongoza nchi ikiwa atashinda urais kupitia CCM!.
 
Back
Top Bottom