CCM acheni kulaghai wenye nchi

ichumu lya

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
2,605
2,729
Yaani sijui nchi hii inapoelekea CCM wamepiga ngoma isiyo na mdundo Watanganyika tunaruka na kukanyagana.

Nani asiyejua ila za CCM? Wanataka Katiba Mpya kwa baada ya kupitisha budget ya 2022-202. Hivi aliyeanzisha mchakato wa Katiba Mpya mpaka tukapata Rasimu ya Warioba ni nani? Si ni hao CCM na Kikwete wao?

Leo wanawapima uelewa na ninyi mnaingia kichwa kichwa. Nataka niwambie mimi nitakuwa wa mwisho kujisalimisha CCM nitaendelea kuhamasisha na kudai Katiba Mpya mpaka Serikali itakapoonesha nia ya dhati kwa kutenga fedha ili tuvuke tulipokwama.

Hatutaki Rasimu ya CCM tunataka Rasimu ya Warioba yenye maoni yetu hasa kumpunguzia Rais mamlaka ya kumiliki ardhi kama yake na kutufanya Watanganyika kuwa wapangaji kwenye ardhi yetu.

Katiba itamke wazi "ardhi ni mali ya Watanzania (Mwananchi)" hatutaki kuendelea kuwa watumwa wa Rais bali Rais awe kiongozi na mamlaka ya mwisho yawe kwa wananchi sio mamlaka ya mwisho kuwa kwa Rais kama ilivyo kwenye katiba hii kandamizi /ya kikoloni inayoleta Utawala badala ya Uongozi.

Michezo ya CCM tumeizoea ila namuuliza Mwenyekiti wa CCM hayo maigizo mnayotufanyia Watanganyika mnajua madhara yake?

@katikabakam.
KaTiBaMaPyANiSaSa
View attachment 2269204
 
Back
Top Bottom