Mchambuzi,
Mkuu wangu hata Hitler alikuwa na wafuasi na alijenga kwanza wanachama wa NAZI na jeshi kubwa kisha ndio akaingia vitani. Kwa hiyo CCM kuwa na wanachama hilo ni given lazima wawepo na sisi sote tumetoka humo.. Lakini waliobakia bado wana mtazamo ule ule na ndio maana nimekwambia wewe unatazama ukiwa ndani ya chama huwezi yaona ya nje mkuu wangu.
Watu wote wanaotetea CCM wanafaidika kwa njia moja ama nyingine na wengine hawana jinsi kama utawala wa Julius Kaizali..Lakini kuwa ndani ya CCM halafu unazungumzia Uanaharakati hapo ndipo napowapinga kwa sababu huwezi ku serve two masters..Tuyaache haya na nakuomba tena samahani - Kuwepo kwako CCM pengine kunaweza wabadilisha chama au nchi lakini navyoamini mimi haiwezekani na ndio maana mnaona kwamba Ufisadi is not an issue!..
Nimeandika mengi sana hapo juu kama ushauri tu sema lugha yangu ndio huwa nzito kiasi kwamba hata mwenyewe naporudia kusoma wakati mwingine husema Duh mkandara punguza Jazba.. lakini ndio hivyo nina uchungu sana na nchi yangu na sioni mabadiliko wala ukombozi..
Kuwepo kwako CCM pengine kunaweza wabadilisha chama au nchi lakini navyoamini mimi haiwezekani na ndio maana mnaona kwamba Ufisadi is not an issue!..
Mbona heading ya uzi wako haiendani na body?? nilidhani wamefanya mkutano mkubwa na kuzoa wanachama wengi kumbe ni maneno tu??Baada ya kukamilisha safu ya uongozi wa mkoa wa Arusha,CCK inatangaza rasmi kuwa tunaingia katika uchaguzi mdogo wa Arumeru kwa ajili ya kuchukua jimbo.
Akitanda ntakuanika ukiendelea kutudis humu....
Nataka kuwa mwanachama wa CCK, wapi niende niko Dar maeneo ya mbezi
@mkandara
Embu Tuache wananchi tupate burudani na mawazo mapya na CCK..
Unajua Chadema tumeshaanza kuchoka na wengine hata mtufanyeje hatuwaamini tena chadema??
Renatus muhabi anatumiwa tu kwenye hiyo cck
Mkubwa mwenzao lakini wa huku mkoani Arusha, nawachukia watu wanaojaribu kina cha maji kwa kidole! watu wanaojiingiza kwenye siasa kwa madhumuni ya tumbo kwanza kabla ya kuangalia maslahi ya Taifa. :A S-confused1:
Hivi hii cck ndo zao la ccj ile ya nape,sitta na mpendazoe?
Huu ni unafiki mkubwa, maneno yako hayana msingi, wewe kama uliwasaidia hao waliokuwa viongozi wa ccj so what? CCK has nothing to do with CCJ, unaonekana hata ukilala na mwanamke ukagundua anakasoro au hukumpenda ndiyo lazima kesho ukamtangaze? tumia akili hao waliokubomu pesa unajuana nao wewe usitutishie!
Mchambuzi,
Nakubaliana nawe lakini mahala pamoja tu uliposema "Ubepari ni zao la Uliberali unaweza kunifafanulia hapo?"
Sasa kuwa mkweli,kama alifanya kazi nzuri,mbona chama kilifia wodini?Bwana mkubwa hawa watu kama kiongozi wao ni huyo Akitanda Constantine namfahamu sana na ni mtu makini sana labda kama kwa hizi siku chache kabadilika , nampenda ni kijana mpambanaji na mwadilifu sana, mgogoro wangu na wao uko kwa huko nyuma tulipotoka CCj tulikuwa na viongozi wa kitaifa matapeli ila yeye wakati huo alikuwa katibu mwenezi, alifanya kazi nzuri sana ila kuna uzembe mkubwa ulikuwepo awali, kama atakuwa na safu nzuri ya uongozi naamini baadaye chama chake baada ya Chadema kitafuatia. maana ccm,tlp,tadea,nccr,udp cuf aka KAFU na majina mengine yafananayo na hayo tutavisahau soon. ilmradi tu wasiwe ccmB. au wakawa wametumwa kuharibu, ila kama wako serious nina imani na Akitanda baada ya kukuta yupo. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, Akitanda ni mtu makini sana iwapo ataungana na wapambanaji wenzake akina Willbrod Slaa,Mbowe,Lema ,Mdee,Mnyika,Kabwe, Ndessa na wengine kama hao ambao hupatikana Chadema.:welcome:
Constantine Akitanda na Mafie PM,
Sasa wakuu zangu mkianza nyie wenyewe kugombana hata chama hajifika mahala kweli kuna usalama. Kwa nini msikae mkayazungumzia yale yaliyopita, mkajifunza makosa kisha mkaendelea mbele maana navyomsoma mimi Mafie anaonyesha hana imani na baadhi ya watu na pengine hao watu wamo pia CCK..kutoka Chama cha Jamii kwenda chama cha Kijamii hakuna tofauti kwa mwenye kusoma alama za wakati.
La muhimu wekeni majina ya viongozi wenu wanachama ambao mnataka kuwanadi kwa wananchi baadaye. Kujificha ya nini kama kweli mnayo nia njema maana uchaguzi Tanzania jamani sii lelemama ni mchakato unaoanza na Wahusika hizi sera na Itikadi ni kachumbari tu kukoleza pilau. Tupeni list ya uongozi watu wengine wabebe ndizi wakijua kuna pilau la nguvu..
Soma hapa nadhani umekosea tu ulitaka kusema Ubepari au sio? Lakini maadam unasisitiza kuwa ufisadi umetokana na Uliberali naomba somo hapo kidogo..Sikumbuki kusema kwamba ubepari ni zao la uliberali kwani hii sio sahihi. Ili uliberali utekelezeke, ni lazima pawe na ubepari. Nilimaanisha ufisadi ni zao la uliberali. Je ulimaanisha kuuliza ufafanuzi kuhusu uhusiano wa uliberali na ufisadi?
Ufisadi is an issue lakini utatuzi wake sio wa kukata matawi bali kuitoa mizizi. Sio Chadema, wala CCM wanaojitambulisha kama wapiganaji, wana mikakati ya kweli ya kutoa mizizi hii kwani wanasahau kwamba itikadi wanazotekeleza - uliberali ndio chanzo kikuu cha ufisadi. Utang'ang'aniaje kupigana na ufisadi wakati hata wewe kama chama unajiendesha kifisadi? Ruzuku za vyama vya siasa ni ufisadi mtupu, na wanaotoa hizo fedha ni hao hao wanao hubiri faida za ulibepari na upanuzi wa demokrasia. Hivi unajua kwamba vyama vikubwa vya siasa vinavyopata ruzuku havitaki kabisa habari ya CAG kwenda kukagua mahesabu yao kwani watagundulika kumbe na wao ni vinara wa ufisadi? Ufisadi ni tatizo kubwa lakini ni la kimfumo, sio la kulipinga majukwaani with a wrong diagnosis.
Vinginevyo uchungu wako kwa nchi yako huwa nauona siku zote, na nina amini kabisa una uzalendo mkubwa sana kwa nchi yako. Nadhani inapotokeaga kwamba tuna tofautiana, ni juu ya njia ya kufikia ukombozi.