Nono, asante kumpa Romos abc za kujenga hoja, kwa vile ni mgeni humu, kwanza Romos karibu JS. pili lengo la mada zote humu, ni ama kuhabarisha, kuelimisha, au kuburudisha. Tofauti na vyombo vingine vya habari, humu pia tunaibua mijadala. Ili hoja yako hii iweze kujadilika kwa afya na mashika, wewe usingetoa conclusion 'CCJ ni mradi wa CCM', ungeitoa kama swali au hojaji kama Je CCJ ni mradi wa CCM?. ungetoa hoja zako zilizopelekea kufiki hivyo na ungejibiwa kwa hoja kwa nini udhaniavyo ndivyo, sivyo, na kuna udhaniavyo sivyo, kumbe ndivyo.Ndugu, mara nyingi hoja haijengwi kwa kuanza na hitimisho. Kwa kawaida tunaanza na utangulizi (intro/background) ambayo hueleza hali halisi, halafu hufuatiwa na smukumo , kwa nini unaamini yale unayotaka kuyaandika (rationale) n.k. Sasa unaporukia tu conclusion, inakuwa vigumu kuona kuwa huna lako jambo.
Siamini kwamba CCj ni mradi wa CCM wala siamini kwamba CCJ ni tishio kwa CCM! Naweza kubashiri kuwa CCJ si CCJ!
Ndio maana mimi kuwa nawashauri watu kutokurupuka...Maana kuna jamaa zangu mara sasa mkombozi kaja mara tumepata chama hasa.. mara hiki ndo kitakuwa cha upinzani wa kweli nakadhalika..Hivi watu hawaoni CHADEMA??
....ni kweli kuna watu wengi sana wana mawazo hayo, lakini jiulize ni wapi vyama vya upinzani vilivyopo vilipojikwaa?na kwanini havijirekebishi ili kubeba matarajio ya watu hawa?...labda ndio sikio la kufa.
....ni kweli kuna watu wengi sana wana mawazo hayo, lakini jiulize ni wapi vyama vya upinzani vilivyopo vilipojikwaa?na kwanini havijirekebishi ili kubeba matarajio ya watu hawa?...labda ndio sikio la kufa.
WanaJF mna maoni yeyote kuhusu hili?
Najaribu kujenga conclusion kuwa CCJ ni mradi wa CCM.
Najua kuwa CCM inafanya kila jitihada kuhakikisha haiondoki madarakani. Mojawapo wa mbinu wanazotumia ni 'wagawe uwatawale'. CCM wanajua kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la wananchi wanaokipinga chama chao hali inayohatarisha future yao katika siasa. yapo maeneo yanayoibukia kwa kasi katika kustawi kwa siasa za upinzani, moja wapo ikiwa kanda ya ziwa victoria. Kwa kuona na kutambua hatari hii inaonekana kundi moja la CCM (huwa naamini CCM ina makundi ma3) limeamua kuanzisha chama kitakachogawa nguvu ya upinzani nchini (hasa ya CHADEMA) kuhakikisha kuwa hakutakuwa na chama kitakachojenga nguvu ya kutisha.
Kama ni mfuatiliaji wa mambo ya CCJ utagundua kuwa chama hiki kimejijengea umaarufu mkubwa maeneo ya kada ya ziwa. Na pia utagundua kuwa huku ndiko CHADEMA kwa miaka ya karibuni imeanza kujizolea umaarufu na ukubaliwaji mkubwa.
Naamini CCJ kinaanzishwa katika mazingira ya ku-confuse akili za watanzania wapenda mabadiliko ambao wengi walishaanza kukifikiria CHADEMA kama chama muafaka ambacho kikiendelea kujipanga vizuri kitakuwa na uwezo wa kuchukua madaraka.
Nisiandike sana lakini pamoja na ushahidi mwangine wa kimazingira kama muda kilipoanzishwa, watu waliokianzisha na maeneo kinapojizatiti inatoa alarm kabisa kuwa CCJ ni chama mradi cha CCM...
Unauhakika kuwa havijirekebishi?umefuatlia trend yao au unasema tu?hivi unafikiri changes huwa zinatokea ndani ya siku moja?hata Roma haikujengwa kwa siku moja,reformation ndani ya taasisi yeyote ile huwa hafanyikikwa haraka kama unavyotaka,hata ndani ya familia huchukua muda...Mabadiliko ni mchakato Mkuu,sio rahisi kihivyo,kumbuka hizi ni taassisi za kisiasa sio MONGOs (My own NGOs)ambapo unaweza ukafanya mabadiliko ndani ya masaa 24 na mambo ya kawa sawa tu...Siasa ni ngumu inahitaji maandalizi na uchambuzi wa kina..
vimekuwa na karibu miaka 15 kujirekebisha...[/QUOTE
Una maanisha nini Mzee Mwanakijiji;?
vimekuwa na karibu miaka 15 kujirekebisha...[/QUOTE
Una maanisha nini Mzee Mwanakijiji;?
kama wangetaka kuungana wangeungana miaka hiyo 15.. kama wangetaka sera mpya wangeweza kuzisahihisha in the past 15 years..
hakuwaandalia maisha unayoyategemeaMbona watoto wa baba wa taifa ni wachovu tu!
.....Kama muda sio limit, yes kila kitu kinawezekana, sio kwa CHADEMA tu bali pia kwa CCM, lakini je tuendelee kusubiri kwa sababu kuna possibilty ya marekebisho kufanyika in the future,...la hasha.
...Wakati ni huu, yawezayo kutendwa na yatendwe haraka kabla treni mpya haijaanza safari, historia ni mwalimu mzuri sana, TADEA/DP/NCCR/TLP wanalijua hili.
Mabadiliko katika siasa yanahitaji kujitolea na uvumilivu wa hali ya juu kwa sababu una dili na mawazo mbali mbali ya watu, mtaji wa siasa ni watu si kama NGO's ambazo mtaji wake ni pesa unazoweza kopa benki. Mtaji watu hauna grantee kuwa utakopa benki na baada ya miaka 15 utarudisha na faida juu kama mnavyotaka kulazimisha.kama wangetaka kuungana wangeungana miaka hiyo 15.. kama wangetaka sera mpya wangeweza kuzisahihisha in the past 15 years..