CCJ: Msajili kabadili namba za wanachama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCJ: Msajili kabadili namba za wanachama

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Jun 6, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  CCJ: Msajili kabadili namba za wanachama

  Na Moshi Lusonzo

  Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa
  Uongozi wa Chama Cha Jamii (CCJ), umeibuka na kutoa madai ya kufanyiwa hujuma baada ya kugundua namba za wanachama wake zilizokuwa ndani ya fomu za Msajili wa Vyama vya Siasa nchini zimebadilishwa.

  Akizungumza na Nipashe jana, Katibu Mkuu wa CCJ, Renatus Muabhi, alisema kutokana na kubainika kwa kasoro hiyo, wamepanga kumfikisha Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa mahakamani Jumatatu (kesho) ili asiendelee na zoezi la kuhakiki wanachama wao hadi hapo hali hiyo itakaporekebishwa.

  Muabhi alisema, baada ya kuvunjika kwa uhakiki wa wanachama wa Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na watu wengi kuonekana sio halali, uongozi umegundua fomu alizokuwa nazo Tendwa nyingi zimebadilishwa namba pamoja na majina ili kuhakikisha kinashindwa kupata wanachama wa kutosha na kunyimwa usajili ya kudumu.

  "Kwa kweli tumebaini kuna njama zimefanyika kwa kubadilisha namba kwenye fomu alizokuwa nazo Msajili, lakini hilo litamalizwa kisheria kwa sababu tunatarajia kwenda mahakamani kupinga mchakato wote wa kuhakiki wanachama hadi hapo totakapokaa na kumaliza tatizo hili," alisema Muabhi.

  Katika zoezi hilo lililofanyika Jumatano iliyopita katika Viwanja vya Mwembeyanga, wanachama 40 waliofanikiwa kuhakikiwa kabla ya zoezi hilo kusitishwa, 27 walishindwa kutambuliwa na Msajili baada ya kuonekana sio halali na 13 pekee ndio waliotambuliwa.

  "Kitu hiki bado kinatuumiza kichwa sisi kama viongozi wa CCJ, haiingii akilini tuwe na wanachama 13 tu ikiwa tulikuwa na maandalizi ya kutosha kabisa, hili jambo lazima tutakwenda mahakamani ikiwa ni pamoja na kumzuia Tendwa asiendelee kuhakiki wanachama wetu bila ridhaa yetu," alisisitiza.

  Aidha, alisema ametoa agizo kwa viongozi wa mikoa yote itakayotembelewa na Msajili kutotoa ushirikiano wowote kwa sababu wao wamejitoa.

  Aliwataka wanachama wa chama hicho kutulia kwa kuwa ana matumaini makubwa suala hilo litatatuliwa haraka ili uhakiki huo urudiwe kwa mara ya pili.

  Hata hivyo, Tendwa alipozungumza wakati akiendelea na zoezi la uhakiki wa chama hicho Ifakara mkoani Morogoro, alisema fomu alizokuwa nazo ni halali kitu ambacho hata viongozi wa CCJ wanakitambua, bali kinachofanyika sasa ni kulidanganya taifa.

  Alisema, anachoendelea kukiona katika ziara yake hiyo ni kitu ambacho hakukitarajia, kwani kuanzia uhakiki wa Mkoa wa Pwani hadi alipofika Ifakara jana hakuweza kumpata hata mwanachama mmoja.

  "Nadhani CCJ wanaliongopea Taifa, hawa watu hawana wanachama kama wanavyodai, jambo hilo ndilo nakumbana nalo kwenye ziara yangu kuanzia jana (juzi) Kibaha na sasa Ifakara hali ni hiyo hiyo, japokuwa huku nimeona ofisi yao," alisema
  .
  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 2. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  CCJ wasitake kutuchanganya akili hapa,wana haraka gani hio ya uchaguzi au mda wote walikuwa wapi kujiandaa kuanzisha chama mpaka ghafla tu na matokeo yake ndio haya kutojiandaa.


  kama kweli wana nia tutawaona 2015 sasa hivi wamekuja kuvurga akili za watanzania tu.
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Me hata hizi siasa nashindwa kuzielewa!
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Siasa zetu hizi zinatufikisha pabaya sana. Sikuamini kuwa wangeshindwa kujipanga kukabiliana na mambo kama haya
   
 5. K

  Keil JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Siasa za Bongo ni aibu tupu ... sasa sijui ni nani anasema ukweli.
   
 6. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,836
  Likes Received: 1,091
  Trophy Points: 280
  endapo itajulikana dhahiri kuwa Tendwa kapika mizengwe atakuwa amepoteza heshma yake kwa jamii, ataondoka katika ofisi kwa aibu kubwa. Kwa upande mwingine kama CCJ wanasema uongo watakuwa wamejiharibia kabisa, ni vema wakasema ukweli na kuomba msamaha kama kuna makosa katika upande wao.
   
 7. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2010
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mbona hii lilikuwa rahisi.

  Mlalamikaji angekusanya hao wanachama halisi 40 na kadi zao, akaita press conference na kwa video akaruhusu angalau wawakilishi watatu au zaidi toka media tofauti tofauti kuita majina kwa mujibu wa orodha yake na waliopo wajitokeze na kuonyesha kadi zao hadharani.

  Hakika nawambieni mkanda huo ungerushwa hewani kusingekuwa na ubishi.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Jun 6, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  watch and learn.. waandishi waliokuwepo hawakutaka kuangalia kinacholalamikiwa wao wakakimbia kuripoti tu? Of course "serikali imesema"..
   
 9. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,927
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Sijui kwa nini nashindwa kumwamini Tendwa!

  Inawezekana kweli CCJ 'wamechemka'...lakini kwa mwenendo wa msajili siku karibuni kweli inatia mashaka. Mtu huyu alituambia CCJ nni 'hoax' lakini baada ya muda akakipa usajili wa muda, baadae akasema hana pesa za kuhakiki...lakini haukupita muda na bila kusema pesa hiyo ghafla imetoka wapi...ameanza kuhakiki! Achilia mbali kauli zake mara kadhaa kwamba CCJ haiwezi kushiriki uchaguzi wa mwaka huu! Ni kama vile kuna mtu anampa directives!
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Jun 6, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  unatumia kile kiungo kilichoko kwenye kichwa chako vizuri sana.. unachofanya ni "thinking".. unahusisha mambo badala ya kuangalia in isolation.. unayaweka katika maudhui yake.
   
 11. B

  Bibi Ntilie JF-Expert Member

  #11
  Jun 6, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 245
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kinachoshangaza ni kuona jinsi ambavyo watu wanashindwa kuketi chini na kutafakari. Chama cha Mapinduzi katika chaguzi hususan Zanzibar na sehemu ambazo kimekuwa kikizidiwa nguvu na vyama vingine kimekuwa kikishutumiwa kwa wizi wa kura. Tumewahi kuelezwa na vyombo vya habari kwamba wakati mwingine kura zinapohesabiwa ghafla taa huzimika na kinachoendelea wakati wa giza hakijulikani. Hatimaye CCM huibuka kidedea! Waswahili wanasema "lisemwalo lipo" na kama CCM wanaweza kufanya madhambi kama hayo, je watashindwa kufanya mikakati ya kikidhalilisha CCJ makusudi kwa kukifanyia mchezo mchafu?
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  Jun 7, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Jamani,
  Rejeeni kauli za Marmo. Na ofisi ya Tendwa iko chini ya Marmo.
   
Loading...