commonmwananchi
JF-Expert Member
- Mar 12, 2011
- 3,377
- 1,952
kwa mujibu wa taarifa ya habari ya BBC swahili,asubuhi hii.wamefikia uamuzi huo baada ya kumtuhumu kukigawa chama kwa hatua yake ya kuwatuhumu baadhi ya vigogo ndani ya chama kwa mambo mbalimbali,pia ikiwemo kutoa matamshi ambayo yamekuwa yakipingana na viongozi wa chama chake katika siasa za ndani na kimataifa.
Kwa ujumla suala hili limeshabihiana na kwa kiwango cha juu na yanayoendelea hapa kwetu hususan ndani ya CCM. kati ya Nape nnauye na baadhi ya vigogo ndani ya chama chake kuhusiana na suala la ufisadi.
My take.
Niliwahi kumueleza Nape Nnauye humu ndani ya JF kuhusiana na suala hili hili na nilimpa mfano wa Julius Malema huyuhuyu, nikimshauri kwamba kama ana nia thabiti ya kupambana na ufisadi ndani ya chama chake basi achukuwe hatua thabiti na uamuzi muhimu na mgumu kwa kuhamia chama kingine cha upinzani na kuendeleza mapambano ya kweli.
Katika majibu yake kwangu Nape, hakugusia swali hili bali alinijibu maswali mengine tu ambayo nilikuwa nimemuuliza,pamoja na hili. Sasa imekuwa hivi kwa Julius Malema, kwa vile misimamo yao ilikuwa inashabihiana (ingawa sina uhakika kama kweli Nape ana nia thabiti kama Malema) ndio maana narudia kumuuliza tena.
Je anasemaje kuhusiana na hili?