CBE seminary | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CBE seminary

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by SI unit, Mar 29, 2012.

 1. S

  SI unit JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 1,938
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Ni kama unaenda kanisani au masjid. Hakuna kuvaa nguo zinazoonesha maungo ya ndan mathalan vimin, vipedo, tait, vitop, kuvaa mlegezo, pensi n.k. Hii nimeipenda!
  WELCOME CBE SEMINARY!
   
 2. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2012
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwanini unaiita Seminary?
   
 3. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  wote tumelipenda hilo,ila tatizo lako kwa nini uite SEMINARY?
   
 4. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ingekuwa safi sana kama hili la CBE lingetumiwa kama mwongozo kwa vyuo vyote hapa nchini. Wakati unakutana na mtu unaogopa hata kumwangalia usoni kutokana na mwonekano wa mavazi aliyotinga!
   
 5. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,052
  Likes Received: 3,082
  Trophy Points: 280
  Seminary??kwani wewe unazichukuliaje Seminary mpaka uamue kuhusanisha sehemu hizi mbili kiongozi?

  Nadhani pamebaki IFM ili tuishi kwa raha mustarehe huku heshima ikisoma 100% kwenye mizani


  Big up sana CBE.
   
 6. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Heko CBE kwa uamuzi wenu makini.Bado IFM na Ustawi wa jamaa,yaani wanawake viumbe wa ajabu sana.Jua kali la saa 6 mchana kweupee yupo na kichupi eti anakwenda chuoni!
   
 7. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Uh,
  wengne tunaona wamechelewa xana
   
 8. S

  SI unit JF-Expert Member

  #8
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 1,938
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  .
  Wewe ulishawahi kuona seminary wanavaa hovyohovyo?
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  y hauish kwa RAHA
   
 10. S

  SI unit JF-Expert Member

  #10
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 1,938
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  .
  Seminary wanavaa kwa adabu, thatz why
   
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  Mar 29, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Wabongo bana dah, hivi mngekuwa serious na vitu vya msingi si tungekua mbali sana? unafiki na kudili na vitu trivial ndio jadi ya mdanganyika.
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wanaogopa majotro bana... lol
   
 13. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #13
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Nampa big up huyo mtu aliotoa wazo
   
 14. m

  mariavictima Senior Member

  #14
  Mar 29, 2012
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tuwapongeze sana CBE na SAUT (St. Augustine) kwa kuonyesha mfano mzuri. Tunaomba Vyuo vingine vyote viige mfano huo.
   
 15. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #15
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ongo vilaza sana ..wanashindwa kufanya mambo ya msingi
   
 16. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #16
  Mar 29, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Majotro ndo nini?...Uzee huu!
   
 17. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #17
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 99%, align: left"]
  [TR]
  [TD="class: kaziBody, align: left"]Vimini, milegezo marufuku CBE
  KAMPENI ya kupinga mavazi yasiyo na heshima imeingia katika sura mpya baada ya uongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kampasi ya Dar es Salaam, kubuni sera inayopiga marufuku mavazi yanayokiuka mila na utamaduni wa Mtanzania, vikiwamo vimini, mlegezo na wanaume kusuka nywele.

  Katika sera hiyo iliyoingizwa katika kanuni za maisha ya mwanafunzi shuleni, mwanafunzi atakayekiuka ataadhibiwa ikiwamo kusimamishwa chuo kwa miezi mitatu.

  Adhabu nyingine ni pamoja na kuzuiwa kuingia getini kwa wanaotoka nje ya hosteli na wanaoishi ndani ya eneo la chuo hawatapewa huduma yoyote kama vile kuingia darasani, kantini, maktaba au ofisi yoyote ya chuo.

  Akitangaza uamuzi huo jana Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Athman Ally Ahmed, alisema chuo kimefikia uamuzi huo baada ya kukithiri kwa uvaaji mavazi yasiyo na staha unaofanywa na wanafunzi chuoni hapo hali inayosababisha udhalilishaji wa utu wa wanafunzi ndani na nje ya chuo.

  Mavazi yanayopigwa marufuku kwa wanaume ni pamoja na uvaaji wa suruali au kaptula na kuacha sehemu ya makalio nje, maarufu kama mlegezo, suruali za kiume zilizopasuliwa kama zilizochakaa (jeans), kusuka nywele, kuvaa kofia aina ya kapelo, pama au bosholi darasani na kuvaa hereni.

  Kwa wanawake mavazi yaliyopigwa marufuku ni vimini, suruali hata za jeans zinazobana na blauzi zinazoacha tumbo, kiuno na kifua wazi, na suruali zinazobana bila kitu kingine kinachoziba mapaja.

  CBE pia imepiga marufuku kaptula za kike au suruali fupi za kubana maarufu kama pedopusha na mavazi yanayoonesha mwili wa mwanamke kuanzia kifuani mpaka mapajani.

  Pia imepiga marufuku sketi fupi zinazoacha wazi mapaja wanapokaa na vazi lolote linaloacha sehemu ya nyuma ya kiuno cha mwanamke wazi au linaloacha wazi sehemu ya juu ya nguo ya ndani wakati amekaa.

  Ahmed alionya kuwa, uongozi wa chuo, hautasita kumchukulia hatua mwanafunzi au mfanyakazi yeyote atakayefika chuoni hapo amevaa mavazi yasiyo ya heshima huku ukitoa mwito kwa wananchi kuunga mkono kampeni hiyo yenye manufaa katika kujenga Taifa lenye maadili mazuri.

  Alisema wanafunzi ambao wengi wao ni vijana chuoni hapo wamekuwa mstari wa mbele kuiga kila aina ya vazi kutoka utamaduni wa watu wa Magharibi hali ambayo
  aliielezea kuwa ni ukiukaji wa mila, desturi na utamaduni wa Mtanzania.

  "Mtindo huu wa kuiga utamaduni wa Magharibi bila kuangalia wapi tunakwenda haukubaliki hata kidogo, ukiangalia katika vyuo vingi vya elimu nchini, wanafunzi wamekuwa wakivaa mavazi ya ajabu na yasiyofaa katika maeneo ya chuo," alisema.

  Makamu Mkuu wa Chuo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mafunzo, Bertha Kipillimba, alisisitiza kuwa sera hiyo itahusu pia wafanyakazi wote wa kampasi ya Dar es Salaam na wanafunzi zaidi ya 6,000 wa chuo.

  Mlezi wa Wanafunzi, Faustin China, alifafanua kuwa umefika wakati wanafunzi hao kujitambua huku akisisitiza kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakinyoshewa vidole na jamii kuhusu suala la uvaaji na mienendo ya wanafunzi chuoni hapo.

  "Tumesemwa vibaya kwa muda mrefu, hatuwezi kuachia suala hili likaendelea, tunataka wanafunzi wetu wavae vizuri kwa mujibu wa kanuni tulizojiwekea, ili kujenga heshima ya chuo," alisema.

  Kampeni dhidi ya uvaaji wa mavazi yasiyo na staha, hivi karibuni ilishika kasi katika madhehebu ya dini hasa Kanisa Katoliki ambako walianzisha matumizi ya kaniki maalumu kuvisha wanaovaa vibaya.
  source: habari leo

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: Text, align: left"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 18. Boniface Evarist

  Boniface Evarist JF-Expert Member

  #18
  Mar 29, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Nataman sana kuandika sheria za St. Joseph university ili ujue hawa jamaa CBE na SAUT wanaiga hili.
  Ila ninapenda sana vyuo vikuu vyote nchini viweke sheria za mavaz itakuwa safi sana.
  Ntarud badae kuweka dress code ya St. Joseph College of Engineering & Technology na St. Joseph Institute of Information Technology ambapo kwa umoja wake ndo St. Joseph University in Tanzania.

  NIMERUDI

  Policy on Dressing

  St. Joseph college emphasize of the total formation of its students. As highlighted in the mission of the college, the management focus on the Discipline and building Values. Keeping this in mind and also the fact that we are in the process of molding the leaders of tomorrow, the safety of the students in Lab and workshops where they work with machinery and chemicals, the college designs its dress code. The college encourages a neat and decent dress along with the uniform and special dress for workshop and labs
  Special Coats Common for both Boys and Girls

  Computer Lab - White Overcoats
  Chemistry Lab - White Overcoats
  Physics Lab - White Overcoats
  Workshop - Blue Overcoats
  Dress Code: Girls

  1. Uniform Shirts and Trousers on all days stipulated.
  2. Neat , Decent and well covered formals and semi-formals on specified days.
  a. Skirts which flow well below knees.
  b. Jeans pants without any holes.
  c. T-Shirts- with Collar and round neck ( no V neck are allowed) .
  d. T-shirts, Shirts or tops with full or half Sleeve
  d. Lab coats are compulsory
  3. Shoes on all working days are compulsory .
  4. High heels, stilettos are not allowed in workshops and labs.
  5. Lab coats are compulsory

  Dress Code: Boys

  1. Uniform Shirts and Trousers on all days stipulated.
  2. Neat , Decent and well covered formals and semi-formals on specified days.
  a. No shorts or Half Trousers of any form are permitted .
  b. Jeans pants without any holes.
  c. T-Shirts- with Collar and round neck .
  d. T-shirts or Shirts with full or half Sleeve
  e.Unwanted, Political, Religious Inviting, Provocation, Obscure, Captions and photos or designs on the dress are not allowed .
  3. Shoes on all working days are compulsory .
  4. Clean shave and well groomed hair is a must. .
  5. T-shirts and Shirts should tuck in their pants
   
 19. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #19
  Mar 29, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  safi cbe......vitoto vilikuwa vinakaa uchi navyo sana....na maukimwi yalikuwa mengi..
  [​IMG]
   
 20. m

  mhondo JF-Expert Member

  #20
  Mar 29, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Ni heri kuchelewa kuliko kutokufanya kabisa.
   
Loading...