Okay,
Acha tupitie namba zako kidogo!
Mapato yako: 1,500,000 TZS kwa mwezi
Matumizi mawili uliyoeleza tayari ni makubwa:
Mafuta: 450,000
Pombe (bia 14 za Serengeti kwa siku)
Gharama za bia husema ni kiasi gani lakini maneo ya Dar es salam kwenye bar kubwa inaweza kuwa 2000 hadi 4000 tufanye Kama bia moja ni takribani 3,000–3,500, maana yake kwa siku unatumia karibu 40,000 – 50,000 kwenye beer.
Kwa mwezi hiyo inaweza kufika karibu 1,200,000 – 1,400,000.
Kwa lugha rahisi, pombe pekee inaweza kuwa inakaribia au hata kuzidi kipato chako cha mwezi. Ikiwa namba ulizotoa ni sahihi. Hapo bado hatujahesabu chakula, nyumba, au mahitaji mengine.
Hivyo tatizo lako si kukosa pesa. Tatizo ni matumizi mawili makubwa sana: pombe na matumizi ya hisia (kuhonga sana).
Kitaalamu kuna hatua chache za kuanza nazo:
1.
Punguza pombe hatua kwa hatua
Kama unakamua bia 14 kwa siku, usijilazimishe kuacha ghafla kama haiwezekani. Anza kupunguza polepole:
wiki ya kwanza: bia 10
wiki ya pili: bia 7
wiki ya tatu: bia 4–5
Ukifanya hivyo unaweza kuokoa maelfu ya shilingi kila siku.
Njia ya pili, Jaribu kuruka siku moja moja bila kunywa pombe Mf. Kunywa jumatatu, jumanne jizuie usinywe, jitahidi kadri ya uwezo wako Kupunguza kunywa kila siku.
Njia ya nyingine ngumu kidogo ni Gym, fanya mazoezi magumu saa moja ikifika umechoka, hutowaza kwenda kulewa.
Njia nyingine, ambayo inahitaji muda na utaalam ni "dopamine detoxing" hii nitaichambua siku nyingine au weka namba yako PM nitakupigia.
2. Weka “daily spending limit”
Kwa kipato cha 1.5M, matumizi yako ya kawaida ya siku yasizidi takribani 25000-3000 isipokuwa kwa gharama maalum kama mafuta.
3. Tenganisha pesa ya mafuta mapema
Hiyo 450k iwe budget yake maalum. Ukishaitenga usichanganye na pesa nyingine, unaweza Kupunguza safari zisizo za lazima ili kuokoa mafuta. Weka sheria binafsi, kisha jiadhibu.
Mfano: Sheria: Mafuta ya 400k yamalize mwezi.
Adhabu: Yakiisha kabla , nitatumia usafiri wa uma ( mwendokasi, daladala) hakuna nidhamu bila sheria. Kuwa mkweli weka sheria na adhabu kisha zifate.
4. Acha au Punguza kuhonga kihisia
Hii ni moja ya money leaks kubwa kwa wanaume wengi. Kama pesa yako haina mfumo, kila mtu anakuwa na access nayo.
Solution: vile huna mke: Tafuta mwanamke mmoja kisha weka kiwango cha pesa utakazompa. Ukizidisha jiwekee adhabu. Weka sheria, kuwa mkali, kuwa mbinafsi, kuwa bahili! Wewe sio mlezi wa wanawake!
5. Anza mfumo wa akiba ya lazima
Siku unayopokea pesa, weka pembeni angalau 300k – 400k kabla hujaanza matumizi. Hii inaitwa pay yourself first.
Jilipe kwanza, weka kwenye account ambayo huwezi kutoa kirahisi mfano "fixed account" "bonds" au weka kwenye account ambayo hauna kadi yake na hujawezesha sim baking, mchakato wa kuitoa hela ukiwa mrefu, unafanya ubongo wako kuignore!
Tips:
- Punguza safari kwa 50% ili kuokoa gharama za mafuta.
- kunywa pombe weekend tu.
- Kuwa na mwanamke mmoja na mpe kiwango cha pesa ambacho umekipanga si vinginevyo. Acha kutaka kuonekana mwamba.
- Record kila shilingi moja iliyotoka na iliyoingia
- Weka laki tano kwenye akiba, bila shaka hata ungekuwa unalipwa milioni ungeendelea kuishi!
Ninaamini una nafasi ya kufanya mabadiliko chanya.
Haraka Haraka na kwa ufupi sana. Ikiwa utahitaji Ushauri na msaada zaidi, na ninaamini nitakusaidia kwa kiwango kikubwa na hautajutia.
Tuma message kwa WATSAPP +255 737 450 640
Au nitumie namba yako PM nitakupigia!