Carina wa NSSF, tunaomba NSSF Taarifa App

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,176
huku nikimpongeza Mama Wangwe kwa kuteuliwa kuwa Mkubwa wa Kazi wa shirika la NSSF, ninamshauri pia katika mambo ya msingi anaweza kutufanyia, japo kwa kuanzia ni kutengeneza application la simu la NSSF kama ilivyo kwa PPF ambao wana PPF Taarifa app.

sisi kama wanachama wa NSSF tunataka taarifa zetu tuzipate viganjani siyo kuja kupanga panga foleni huko mambo ya kizamani au kuenda internet cafe kufungua website ya NSSF ambapo kuna mlolongo mreeefu wa kupata ukurasa sahihi wa kujuwa taarifa za michango.

Mwisho naomba wewe na wenzio wa mashirika mengine ya Hifadhi ya Jamii muangalie uwezekano wa kuishauri serikali makato ya NSSF yawe makubwa kuliko makato ya PAYE maana PAYE inawahusu mafisadi, NSSF inahusu maisha yetu ya baadae. Haileti sense kuwachangia mafisadi pakubwa afu mi mwenyewe najichangia kiduchu.
 
Back
Top Bottom