Card yangu ya CRDB imemezwa hata sijui nifanyeje

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,631
Nilienda kutoa pesa kwenye moja ya Atm zao nikakuta hakuna salio nikawa nangoja card itoke lakini cha ajabu ikamezwa!ilikua jana hiyo

Cha kushangaza ni kuwa wananiambia card yangu imekwisha muda wake wakati nimejiunga nao mwaka jana tu hapo mwezi December!
Ni issue ni kwamba account namba sikukariri chochote zaidi ya password yangu tu hata sijui nafanyaje

Nimeambiwa niende tawi lao nikaenda nilipofungulia nashangaa naambiwa umeme hakuna! ikabidi niondoke tu wakanambia niende tawi jingine

Wakuu nisaidieni jee nifanyeje? Nifanyeje maana pesa ndo huwa zinatumwa kupitia huko na ndo iko registered kwenye mishahara yangu kwamba ndo pesa inatakiwa iingie huko na jana tu na kuna hela nyingi tu inatakiwa itumwe huko
Na itachukua muda gan kuipata?

Kingine naomba kujuzwa nikienda kama nitatozwa gharama yoyote!,Maana nahisi nimevurugwa

Asanteni
 
Kadi yangu ishawahi kumezwa, ukienda kwenye tawi lao unapatiwa form unajaza, unasubiria siku 7 mpaka 10 unapata kadi yako mpya.

Kuhusu account namba unaeza muomba mhasibu wa mahali unapofanyia kazi akupe namba hiyo, au kama ulikua umejiunga na Simbanking pia unaweza endelea kutoa hela kupitia simu yako mmoja kwa mmoja bila kadi.
 
Haujui namba yako?? Duh!!
Mwombe mhasibu au wanokuigizia hela akupe namba yako!
Nenda tawi lolote na ID yako na namba ya Ac jaza form watakupa hela!
Ni lazima uweze kuijua namba yako kwanza!
 
Kadi yangu ishawahi kumezwa, ukienda kwenye tawi lao unapatiwa form unajaza, unasubiria siku 7 mpaka 10 unapata kadi yako mpya.

Kuhusu account namba unaeza muomba mhasibu wa mahali unapofanyia kazi akupe namba hiyo, au kama ulikua umejiunga na Simbanking pia unaweza endelea kutoa hela kupitia simu yako mmoja kwa mmoja bila kadi.
Basi hizi benk ziko tofauti mbona mimi siku hio hio nilipata
 
Bank ulipoenda ungepewa maelezo yote ,

Kadi sio lazima UE nayo ili utoe pesa ya kusurvive.

Bank hata km huna account number utapata huko ..

Kadi sio yako umekosea namba ya siri???.

Kadi ya mwaka Jana time expire Leo?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom