Card designing- tuelimishane | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Card designing- tuelimishane

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Mtazamaji, Dec 19, 2011.

 1. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #1
  Dec 19, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wakuuwa wa mambo ya ghraphics na card design

  • Napena kujua ni application gani au software gani zinazotumika kutengenza card nzuri za harusi na shere nyinginezo ama Mwaka mpya , siku ya kuzaliwa na hata na nyinginezo?
  Pamoja na kuwepo watu wanaotengeza kadi nzuri zaharusi na sherehe nyinginezo kwa nini kwenye maduka mengi hakuna kadi (Nzuri) za kitanzania au za kiswahili za sherere kama X-mas, Mwaka mpya , bitrhday, Idd, etc

  Karibuni tuelimishane na
  ikwezekana tutengeneze custom JF technology forum card ya mwaka mpya amabayo tunaweza kuiprint kwenye hard Copy. I mean sio zile za kutengeza online
   
 2. matwi

  matwi JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2011
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 276
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wazo zuri mkuu yani wengine tunaletewa card zimendikwa kizungu tunafurahia picha tu ya card ila ujumbe ulioandikwa mayolooo..!!!
   
 3. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Good idea. Tunasubiri wataalamu watueleze namna ya ku-design hizo kadi.
   
 4. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Bila bila . Haya feeback niliyopata kupitia google kuna application kibao za kusaidi kufanya mambo haya moja wapo inatwa HALLMARK CARD STUDIO. . Unaweza kucheki Greeting Card Software Review 2012 - TopTenREVIEWS

  Nategemea wataaaam wa graphics watakuja na mambo mazuri zaidi kutuelimisha.
   
 5. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #5
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Inategemea na level yako katika graphics design. Waweza tumia software za card moja kwa moja. Ila nadhani Adobe Illustrator itakuwa ni bora zaidi kama wewe ni advanced user.
   
 6. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Simple and straight foward.. M.S PUBLISHER.
   
 7. Buggy

  Buggy JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 239
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  yes, kuna software kibao za ku-design cards! mie napenda kutumia Adobe Illustrator, Photoshop na Indesign (zote zikiwa katika level ya CS5), huwa naweza kutumia zote kwa wakati mmoja kama na-design a certain card. Photoshop CS5 inanisaidia kuweka manjonjo kama effects na kadhalika....., then Illustrator au indesign inanisaidia kuweka layout etc....
   
 8. K

  Kizzy Member

  #8
  Dec 21, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nafikiri Ku design ni swala moja na kuchapisha swala jingine maana unaweza kuwa na top of the software kama wadau wengine walivyokushauri lakini kama uchapishaji sio mzuri basi ni bure maana utakuwa na goog design lakini printing ikakulet down
   
 9. Bosi Michembe

  Bosi Michembe JF-Expert Member

  #9
  Dec 21, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 273
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mkuu! Buggy hapo juu ametoa list ya most used software za design katika industry. Ila kuna Corel Draw nayo nzuri (it is one of the most used software kwenye textile design). But kama hutaki kuumiza kichwa in the sense wateja ni harusi,birthday na kipaimara na they won't be willing to pay you 250 usd for a design basi Microsoft publisher is the best. Ina templates kibao za kila publications from brochures to magazines.
   
 10. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #10
  Dec 21, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Asanteni wadau. Binafsi sio advanced user ila nimepata mwamko na mambo haya ya graphiccs mwaka huu. Nilichoona ni rahisi Kwangu amabcho ingawa sio proffesional sana kama mdau mmoja alivysoema zaidi ni kutumia application kama hallmark card studio au Print shop.
  Hizi zinakuja na sample projects kibao lakini kali kuliko hata za Ms publihser. Kwa wale wenye internet cafe ni something wacheki. Wasridhie na MS publihser.

  Sasa kwenye hizi hallmark na Printshop msaada wa program za adobe kama photoshop na ilustrator unaweza pia kutumika kuichakachua sample project au kutenegza project nyingine mpya kirahisi zaidi.

  Uzuri wa Hallmark studio(Amabayo nimejaribu na uthibitisha ) na Printshop( sina uhaika ila kwenye review wanasema hivyo) zinuruhusu vile vile kuifanya import ya picha kutoka sehemunyigine kama adbe na kuchakachua hizo sample project. Hallmark

  GHARAMA
  inauzwa $29 na Printshp inauzwa $49. But as usual zinapatikana pia kwa bei chee ile mitaa yetu teh teh teh .Gharama ni uvumilivu na banwidth ya kupakua 6 GB ( hallmark) na 8GB Printshop.

  TRADE OFF BTN DESIGN PRINTING QUALITY
  Kuhusu kuchapisha ni kweli ni issue lakini si unaweza kutengenenza kadi yako safi ghetto then ukatafuta sehemu yenye printing facility nzuri tu? Je Bs mchembe , Kizzy na wengineo tukiacha Kudesgn kadi wapi naweza kwenda na kazi yangu tayari kweye flash wao wakanitoza huduma ya kuprint tu na karatasi .Au. ni Ni karatasi aina gani ngumu zinafaa kwa printing ya kadi ili nininue nikajarbu hata kwneye ka printer k ka deskjet au laser uswazi


  Mkuu sasa wee kama mtaalama kwa nini soko la kadi za bongo za siku uu zimejaa kadi ya kuimport.
  • Tufanye nini taifa liokoe $$$$$$ wa ajili ya kuimport kadi ya X mas birthday, motherdays day fathers day, Idd-el-fitr, etc ?
  • Kwa nini kuna kadi za harusi , send off za kiswahili nzuri lakini sio za sikukuu na sherere nyingine? nini kikwazo
   
 11. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #11
  Dec 21, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hii ni moja ya kadi amabayo nimejaribu kuyachakachua maneno ya kingereza na kuyatafsiri kwenye kiswahili. Hapa kilichobaki ni kupata karatasi sahihi na printer sahihi
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Bosi Michembe

  Bosi Michembe JF-Expert Member

  #12
  Dec 23, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 273
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mkuu idea yako ni nzuri sana.. but unahitaji kujipanga na kuja na marketing strategies za maana ili uweze kuteka soko. Lets say unaweza kufanya custom made cards ambapo mtu akija kununua inakuwa blank kwenye meseji anakupa maneno yake au anaandika mwenyewe. (note: kadi nyingi za nje ni maneno ya mzungu mmoja huko ulaya anaejaribu kufikisha ujumbe kwa niaba yetu na mara nyingi ujumbe unakuwa haujitosheleza ndo maana tunaishia kuongeza maneno yetu kwa peni kwa pembeni). Au unaweka email adress ambayo mtu anKucontact anakutumia anachohitaji , iweje ni ya nini then lets say anaipitia after some time.. (Just an idea)

  Kuhusu printers wako wengi but ushauri wangu epuka printers wakubwa(from my experience wanakuwa na wateja wakubwa ambao mara nyingi niPriority na wewe kama startup utapigwa delays za hapa na pale hata kama uliwahi ili waweze kuwamalizia kazi wanaoleta pesa nyingi..

  Hints nyingine usiprint kwa laser printers maana ni expensive (wino, karatasi , muda) na quality yake inakuwa siyo zaidi ya office standard, Offset printing ndiyo yenyewe ingawa inahitaji uprint large quantity kidogo its far less cheap na wateja watapenda.. Posters, maboksi ya biskuti na magazines karibu zote ni Offset..

  Mpigie huyu jamaa anaSmall scale facility na bei zake ni za kawaida sana yuko Mikocheni (mimi hupeleka kazi kwake). Atakushauri kuhusu karatasi ya kutumia pia..

  0713 555 369 anaitwa Steve


  Am sure ukikomaa u will make its business venture ambayo haijawa explored kivile. . (local made cards work vibaya mno mi nilikuwa nachora shule hivyo nilikuwa siongei sana nikiwaangushia kitu nimechora mwenyewe na jina lake ndani.. Kitu na Boksi)
   
 13. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #13
  Dec 23, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Kwa upande wangu mimi ninazifahamu software nyingi ambazo hutumika katika kudesign graphics like business cards, wedding cards, ID's etc. But tukiachana na hizo software ndogo ndogo, the best software for graphics designing in this world kwa matumizi ambayo wewe unayahitaji ni Adobe Photoshop and Adobe Indesign
   
 14. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #14
  Dec 24, 2011
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Suala la software za kutumia inategemea na ujuzi wa designer kama walivyosema wadau hapo juu. Software zilizopendekezwa kama Ms Publisher na zingine zenye templates kibao mara nyingi huwa intended kwa beginners, professionals hutumia templates kidogo sana, usually kama guidelines. Well, binafsi kwa graphic design hutumia Adobe Photoshop, Adobe Illustrator na Adobe Indesign aghalabu kwa wakati mmoja kutegemeana na kazi nayofanya.

  KADI
  Miaka kama 5 iliyopita nilipata kuongea na watu fulani (Actualy mtu mmoja-muuza cards) juu ya uwezekano wa kuuza cards zilizoandikwa kwa kiswahili. Aliniambia kuwa kuna wakati watu fulani walitengeneza kadi za kiswahili lakini zilipata taabu sana sokoni kwa kuwa wanunuzi wengi hawapendi lugha ya kiswahili kwa sababu inaonekana haina mzuka na anayenunua anaonekana kama maamuma (illiterate) wa Kiingereza jambo ambalo kwa kizazi chetu inaonekana kama aibu fulani.

  MAONI YANGU
  Ukitaka kutengeneza kadi za kiswahili ni muhimu ufanye haya:
  1. Hakikisha quality ya both design na printing inaendana na international standards. Tatizo la Wa-TZ ni ku-politicise kila kitu. Huwezi kudesign kadi mbaya halafu unitake niinunue ili kuonesha uzalendo kwa U-Tanzania na lugha ya Kiswahili. Mbaya ni mbaya tu!! Turn yourself into a professional designer. Achana na Ms Publisher (Naruhusu mjadala hapa). Jifunze kudesign from concept to finish. Tumia template kama guidelines tu. Tazama kadi za wengine kama inspiration. Madhara ya templates ni kazi kuwa similar hasa kwa watu ambao si creative.
  2. Wanunuaji wakubwa wa kadi ni Wanawake. Fahamu hisia zao kuhusu rangi, maneno na aina ya matukio wayapendayo. Hakikisha lugha unayotumia ina flavour/rhyme zinazoendana na hisia zao. Design sample halafu waoneshe wanawake ila usiwaambie kuwa umedesign wewe wasije wakasifia kwa kukuonea huruma. Wasipopenda design zako waulize kwanini na fanyia kazi mapendekezo yao.
  3. Kiswahili ni lugha inayodharauliwa kiasi fulani na wazungumzaji wake kwa kuwa inaonekana haina ladha ya mahaba na pia huonekana kama kali sana kwa baadhi ya maneno. Kwa mfano maneno "I want to hug and kiss you" hayana uzito kama "Ninataka kukukumbatia na kukubusu" japo maana ni ile ile (kwa tafsiri yangu). Angalia majina ya sinema za akina Kanumba ni ya Kiingereza hata kama kuna Kiswahili chake rahisi. Hivyo inahitaji weledi mkubwa wa kuchagua maneno sahihi ili yalete hisia sahihi. Jifunze kufikiri kama professional.
  4. Kumbuka kuwa gharama ya kutengeneza cards inaweza kuwa kubwa ama ndogo tegemeana na teknolojia unayotumia kuprint. Kariakoo (na sehemu zingine) kuna Digital Printers (Konica Minolta Bizhub) ambapo waweza kuprint hata sheet moja tu ya karatasi na quality yake ni nzuri. Huwa wanacharge 1000/= kwa upande mmoja wa karatasi ya A3 bila kujali unene wake. Karatasi ifaayo card ni Glossy paper (inang'aa na kutereza) ya gramu 300. Kwa mfano ukitaka kutengeneza card ya size ya A5 inabidi udesign katika A4 then uikunje katikati. Generally, gharama ya kuprint kadi nzima itakuwa kama 1000/= hivi. Je, utaiuza sh ngapi? Discount za Digital printers ni very minimal. Njia ya pili ni kuprint kwa mashine kubwa (Offset Printer) ambazo quality yake ni excellent lakini hawako tayari kuprint kadi chache. Huenda wakataka kuanzia 500 (na hii ni kwa wachapishaji wadogo, wakubwa kama Jamana wanaweza kusema kuanzia 2000 copies). Kwa nakala 500 huenda ikakugharimu kati ya sh 400 na 600 kwa kadi moja (I may be wrong). Kadiri unavyoprint nyingi ndivyo gharama inapungua kwa kila kadi. Je, uko tayari kuprint kadi 1000 za Kiswahili kwa soko lenye mashaka? Unahitaji kufanya utafiti.
  5. Ubora wa kadi si printing na designing pekee bali hata finishing zingine kama cutting na kuweka tones ama nyimbo kadi ikifunguliwa. Najua mmeshaona kadi zilizokatwa vizuri kweli; je, mashine za kufanya hivyo tunazo? Je, tunaweza weka bongo flavour katika kadi? Kama ndiyo, basi inaweza kuwa biashara nzuri sana. Wanaoweza kujaribu wafanye hivyo na watuletee majibu.
  MWISHO
  Usitengeneze kitu kibaya halafu utegemee tununue kwa sababu wewe ni Mtanzania mwenzetu. Kila biashara inahitaji research. Ni vizuri kujaribu.
   
 15. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #15
  Dec 24, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkuu thanks Analysis yako imekaa njema sana. Kuhusu kiswahili naomba nijibu si ama mtalamaau mzoefu ila ninavyohani. Kiswahili kina radha ni ni lugha tajiri sema tu kiswahili ninachojuaimi na wewe kinaweza kisiwe kizuri kwa mahaba. Nia hakia kuna walee wazee shaban , Goga, Kahmis Akida (Sijui ama bado wako hai) wakitumiwa wanaweza kutoa misemo maneno na fulani ambayo ninahaikmtu akisoma anaweza kuvutika zaidi. Lakini Ukweli uko wazi watanzani wengi perception yetu kwenye kiswahili = Ilitierete. Lakini hii weakness mtu unaweza kuitumia kuwa opprtunity ili upate suport na promo ya vyombo Husika kama BAKITA, Idara ya Utamaduni nahata serikali. May be naota lol

  Kuhsu kinakanumba nahani ni udhaifu wa fani yetu kutotaka auutopend autuia ushauri wa wataalm niliotaja hapo juu. Sidhani kama anuba nawenzake mvie wanazotenegza huwa wanapata muda wa kuwapata watalam wa sanaa wa Chuo kuu au hata bagamoyo ili wawape japo kaushauri. Tati

  Cha mwisho card ni unpreishable. So sidhani kama inaweza kuwa na hasaraa kama imepromotiwa na na ni i nuzir kama. Kikwazo kikubwa kinaweza kuwa kwenye maduka mengi ya kadi sio waswahili wengi ni wahindi. Sasa kadi za X mas zinaonyesha barafu lakini kwa desinger wetu nadhani wanaweza kunyesha image nyingine nzuri tu hata ya nyumba ya msonge...........

  But thanks kwa uchambuzi wako makini

  Powa mkuu. Aksante sana Nimeona kua software ya Hallmark ambayo pia unaweza kuimport hata graphics za Phothoshop . wa kuwa si mtaalama nitaanza na hii hallmark na baaay nitatitumia kusaidianana na Photoshop.

  Ngoja nile zoezi iwe ni project ya 2012
   
 16. matwi

  matwi JF-Expert Member

  #16
  Dec 25, 2011
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 276
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wakati tuna jadili haya mie leo katika pita yangu kwenye maduka ya kadi nimezikuta za kiswahili
  DSCF0019.JPG DSCF0018.JPG DSCF0027.JPG
   
Loading...