Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Watu wanne wameuawa kwenye ufyatulianaji wa risasi katika msikiti mmoja mjini Quebec, Canada
Ufyatulianaji wa risasi ulitokea katika kituo cha Kitamaduni cha Kiislaam cha Quebec Jumapili usiku, polisi wamesema
Kituo hicho kimepakia kwenye ukurasa wake wa Facebook video inayoonesha polisi wakiwa nje ya kituo hicho. Video hiyo imeambatana na ujumbe kwamba "baadhi wamefariki"
Polisi wamesema watu wawili wamekamatwa, lakini hawajatangaza idadi kamili ya waliofariki au kujeruhiwa
Mtu aliyeshuhudia ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba watu hadi watatu walikuwa na silaha wamehusika
Shirika hilo la habari pia limesema maafisa wa usalama waliokuwa na silaha kali wameonekana wakiingia kwenye msikiti huo
Gazeti la Le Soleil linasema limepata taarifa kwamba mmoja wa washukiwa ni Kijana wa miaka 27 mwenye "jina la asili ya Quebec" na alikuwa na bunduki aina ya AK - 47
Ufyatulianaji huo wa risasi umetokea katika msikiti ulio kwenye barabara ya Sainte - Foy, moja ya misikiti miwili inayoendeshwa na kituo hicho cha Utamaduni wa Kiislaam
Shambulio lilitekelezwa wakati wa Sala ya jioni
Rais wa msikiti huo Mohamed Yangui, ambaye hakuwa ndani ya msikiti wakati wa shambulio, ameliambia Reuters kwamba hajafahamu kufikia sasa idadi ya waliojeruhiwa ingawa wamepelekwa hospitali mbalimbali Quebec
"Nini kinatendeka hapa? Huu ni unyama ", alisema
Juni mwaka jana, kulipatikana karibu na mlango wa msikiti huo kichwa cha nguruwe kilichokuwa kimefungwa vizuri kama zawadi na kuandika" bonne appetit ". waislamu hawali nguruwe
Waziri Mkuu wa Justin Trudeau ameandika kwenye Twitter kwa Kiingereza na Kifaransa na kusema," Usiku huu, raia wa Canada wanaomboleza waliouawa kwenye shambulio hili la woga katika msikiti mmoja Quebec. Fikira zangu ni kwa waathiriwa na jamaa zao.
Chanzo: BBC