Canada na Ufaransa zawalilia wawekezaji wa Kichina kuwekeza kwenye mataifa yao

Canada na Ufaransa zawalilia wawekezaji wa Kichina kuwekeza kwenye mataifa yao

Xi Jinping

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2023
Posts
8,102
Reaction score
23,690
Mwaka 2024 Canada ikishinikizwa na Marekani iliweka ushuru wa 100% kwa magari ya umeme ya China kama ilivyofanya Marekani.

The table has turned, hivi karibuni Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney alikuwa na ziara nchini China. Katika ziara hiyo alifungua milango ya kibiashara kati ya mataifa hayo.

Baada ya mambo kuwa magumu kwa Canada katika auto industry hatimaye Carney ameondoa ushuru kwa Chinese EVs.

"Ili kuifanya Kanada kuwa kiongozi katika utengenezaji wa magari ya umeme, tunajitahidi kuvutia uwekezaji mpya wa ubia na China. Na kadri sekta yetu ya ndani inavyoongezeka, tutaruhusu EVs kutoka China kwenye soko la Kanada."
Mark Carney

Wakati hayo yakiendelea upande wa Canada, barani Ulaya Raisi wa Ufaransa Macron akiwa Davos katika mkutano wa World Economic Forum naye kilio chake kilikuwa:

"Tunahitaji uwekezaji zaidi wa Wachina barani Ulaya katika sekta muhimu."
Emmanuel Macron
Hili ni pigo kubwa kwa Trump ambaye mara zote amekuwa akilitumia bara la Ulaya na Canada kuidhoofisha China bila mafanikio.

Ni wakati wa Marekani kuiga mfano wa Canada, Ufaransa na Ulaya, ni ngumu sana kwa sasa kumkimbia Mchina kwenye manufacturing na technology plus kibunda wanacho.
 
Trump ubabe umezidi. Ni kama waambiwa na tajiri jirani usiende duka la fulani ama sivyo tajiri hatakusaidia siku ya shida? Na pia tajiri atatumia mbinu za kukudhalilisha! Mawazo ya trump ni ya kitoto, kijinga na kufedhehesha!
Uongozi wa trump utawaangusha kiuchumi sana USA, hata kama watashupalia kuteka rasilimali na maliasili za nchi zingine...
 
Back
Top Bottom