Salamu wana JF wote,
Ukiiangalia Tanzania ya leo kwa umakini inaonekana kana kwamba mtu hawezi kuendelea bila kumrudisha mwenzie nyuma kwa namna fulani. Angalia nyanja zote unazozijua wewe, anzia kwa masikini wa chini kabisa mpaka tajiri mkubwa kabisa. Tunaumizana kwa namna nyingi kabisa lakini kinachosaidia ni kwamba ukiumizwa hamna kupiga kelele kwa maana na wewe unayo sehemu ya kumuumiza mtu. Hii ndio vicious circle tuliyomo, ndio mfumo wa maisha viongozi wetu wa kisiasa wameamua tuishi nao. Mwalimu wa shule ya msingi hawezi kuishi kwa 160,000 kwa mwezi, Trafiki hawezi kuishi kwa mshahara anaopata, mkulima hawezi kuishi kwa kilimo anachojihusisha nacho, wahudumu wa afya hawawezi kuishi kwa kipato wanachopata, wasafirishaji nao hawawezi kuishi, LAKINI WANAISHI . Hili ndio chimbuko la Rushwa na Ufisadi unaoitesa nchi hii. Karibia kila mtu anaishi kwenye Rushwa ijapokuwa wengi hawawezi kukubali, ndio maana nimeamua kuuliza 'Can we make someone better off without making someone worst off? Tunaweza kumuendeleza mtu bila kumrudisha mwingine nyuma? :nono:
Pax