Can Samwel Sitta Walk the Talk? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Can Samwel Sitta Walk the Talk?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ibange, Jun 26, 2011.

 1. i

  ibange JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nimeguswa sana na hoja za Sitta huko mzumbe jana kuwa tz ni nchi ya pili africa kuwa na potentials za umeme baada ya drc. alisema tz ingetakiwa inauza umeme nje si kuwa na mgao. alimaanisha tatizo ni uongozi mbovu unashindwa kulinda na kuendeleza rasilimali zetu. najiuliza anaweza kutekeleza anayozungumza akiwa ndani ya magamba? nampenda anaonekana mzalendo isipokuwa yupo kwenye a wrong party
   
 2. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Namfananisha sitta na mwanafufunzi aliyefumaniwa na mwalimu akivuta sigara.Yule mwanafunzi alilazimika aifiche sigara kwenye mfuko wake huku bado inawaka.Dogo akawa anaungua na kwa sababu mwl alimwona anaiweka mfukoni ikiwa haijazimwa akaendelea kumpisha stori huku dent anakipata kitu cha moto.Sita naye hivyo ataendelea kuumia lakn afanyeje! hawezi kujivua gamba.Angekuwa anaweza siku nyingi angetoka kwa sababu ameshawahi kutishiwa kunyang'anya kadi lakn yumo tu.
   
 3. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Alichosema Sita kiaendelea kutia chumvi kwenye kidonda...umeme hatuna halafu Waziri wa serikali anasema ungeweza kupatikana tena kwa wingi hadi tuuze nje. Hivi ndio anatuambia kwakua hakuweza kuongea hayo kwenye baraza la mawaziri? Hivi JK anashindwa hata kudhibiti baraza la watu sitini aliowachagua mwenyewe?
   
 4. T

  Technology JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 733
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  If what Sitta says is true; then the information we have about electricity problems that we now know is even worse, can Mr. President come out and tell us.
   
 5. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Tatizo la siita ni kwamba anachosema ni kweli lakini anakisema sababu yupo kwenye postion ambayo labda haipendi. Sijui kama angekuw awaziri wa nishati angezumza hayo . Na sijui kama angekuwa ni PM na hali ika kama ilivy leo angesema hivi.

  Sitta hafai hana colective resposibility. Anatakiwa ajiuzulu ili tuamini anammisha anachosema , Kwangu naona he sj want political gain and publicty. Anachosema Sitta ikanatkiwa kuongelewa na CDM na CUF yeye kama wairi anatakiwa anasema hivyo kisha anajiuzulu.

  Tumuulize wakiwa kwenye viakao vyao vya baraza la mawairi anawaambia wenzake hayo???!!!!!!
   
 6. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #6
  Jun 26, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,130
  Trophy Points: 280
  mimi napingana na wewe kwa aslimia 500%, samweli 6 ni moja kati ya viongozi wanafiki sana nchi hii. Tujiulize akiwa kama spika aliwezaje kusaidia kupunguza tatizo la umeme hapa nchini?
  Six tatizo lake anapenda sana madaraka na tambua kwamba katika nchi hii spika wa bunge ni kama mtu wa tatu au wa nne kwa mamulaka ya nchi.

  Kitendo cha 6 kukubari uwaziri wa wa africa mashariki kumemushushia hazi sana. Ni sawa na raisi arudi kuwa waziri mkuu. Yeye anaganga njaa tu na hakuna lolote. Kwa sasa hivi kila kiongozi anaibuka na kudai hili na lile
  na kitendo cha 6 kutumia mamilioni ya walipa kodi kujenga ofisi ya usipika jimboni kwakwe na hiyo ofisi haitumiki kwa sasa ni hakufai. Angekuwa na uchungu na nchi hii asinge jenga ofisi ya uspika kule urambo.
   
 7. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 133
  But fighting within is also good and can yield better results!
   
 8. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Why Mr. Sitta speaks out of the government? What we have here is a collective govt, he have to innitiate within the govt and come out with the solution not with a problem of load shading which is killing Tanzanian
   
 9. p

  plawala JF-Expert Member

  #9
  Jun 26, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Obviously Mr Sitta cant walk the talk,since he cannot walk the talk he better stop to talk!
   
 10. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #10
  Jun 26, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Yes it can yield btter result na mimi nafurahi sababu anaidhoofisha CCM . Kwa wanapenda mabadiliko tunapenda wawepo kina SIX kama kumi hivi ndani ya CCM . lakini ukweli ni kuwa Kama Sitta angekuwa PM au waziri wa Nishati asingeongea hayo...........

  Wizara aliyopewa sitta haina publicty anayotaka na mbaya nadhani na yeye sio creative wa new idea zinazoweza kuleta mjadala wa kitaifa.

  Mfano ningekuwa sita ningeaza kutoa hoja Bunge la Tanzania na mabunge ya afrika mashariki yapige marfuku usafirishi wa wanyama nje ya nchi. hii issue hatuwezi kufanikiwa peke yetu lakini kusafirisha wanyama nje ku uhaini wa uchumi wetu wenyewe.

  Anyway mi natahamin kazi ya sita lakini naitahmini sababu anaidoofisha CCM.

  Otherwise aseme fighting within hiyo ametoa mapendekezo gani hasa yenye tofauti au yaliyokataliwa
   
 11. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,163
  Trophy Points: 280
  Mr. President, the only President who declared that all elctricity production problems will end within his tenure and more than that he has even shown us how he is going to do that, where are you?
   
 12. h

  housta Senior Member

  #12
  Jun 26, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kuwa Spika sio kwamba unaweza kuleta a direct impact kwenye suala hili.Kumbuka kuna mamlaka zaidi juu yako hivyo kila kitu kinategemea hao waliopo juu na mawaziri wake.Sitaki kumtetea na kauli zake lakini penye ukweli tuache hisia binafsi na tuseme ukweli.Aliyepewa wizara ni kilaza na aliyempa ni kilaza vile vile.Ndio kuna viongozi wazuri tu ndani ya serikali,tukubali hilo!Ila nchi yetu inahitaji 'overhauling' ya hali ya juu sana kuweza angalau kufika robo ya matarajio ya wengi.
   
 13. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #13
  Jun 26, 2011
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mzee Six,

  Nakusoma sana kauli zako na nafuatilia sana kila usemalo... lakini mpaka sasa kwa kweli umeonyesha dhahiri kwamba wewe madaraka kwako ni kitu kikubwa sana. Naomba nikukumbushe machache.
  • Uliwapa wabunge mafao mengi kuhakikisha wanakurudisha muhula wa pili ukidhani yafuatayo
   1. Wabunge wengi wangerudi kwenye bunge kipindi cha awamu ya pili ya JK
   2. Kwamba wewe ungepitishwa na chama chako kugombea tena.
  • Ulijenga ofisi ya Bunge kali kuliko zote kwa sababu ati ofisi hiyo ni ya mbunge na pia Spika... as if wewe ungeweza kuwa Spika wa Maisha au Urambo ingetoa Spika kwenye vipindi vyote vya Uchaguzi
  • Ukiwa Spika ulikuwa unatamani Muhimili wa Bunge ndio uwe juu ya mihimili yote... hivyo kuipeleka mchakamchaka serikali ya Kikwete na wakati mwingine kuingilia mahakama.
  • Wakati ukiwa Spika kuna wakati ulikuwa hata unawasaidia Mawaziri kujibu Maswali. Aidha kuwa-influence wakubali jambo... au waahidi kitu kwa mbunge muuliza swali.
  • Inajulikana wazi kwamba issue ya Richmond ilikuzwa sana kwa sababu tu ya kuwa ungedhani mitambo ya Dowans ingenunuliwa na TANESCO wapinzani wako wangekuwa na uwezo zaidi ya kukushinda wewe kwenye mbio za Urais 2015... hata hivyo tunakuomba uendelee kupigania hiyo mitambo ilivyonunuliwa na Symbion kama wewe mzee wa Viwango.
  • Mengine mengi nakubaliana na wewe isipokuwa kuna mambo yaliyojificha kwenye kauli zako nyingi sana mzee.
   
Loading...