Camfed ni nini? Anae wafahamu Camfed vizuri afunguke

Camfed ni nini? Anae wafahamu Camfed vizuri afunguke

Kuna mtu namfahamu ni mwana CAMA kwa maana aliwahi kusaidiwa na hao Camfed. Kwa sasa anajifanyia shuguli zake za kipato na ana pesa nzuri tu. Camfed huwapa hadi mikopo isiyo na riba. Can you imagine unakopa milioni 4 ulipe mwaka mzima/miezi 6 bila riba?
Bidada huchukua na kurejesha haraka kisha hukopa tena.

Sema watu wanapiga hela sana huko kwa namna wanayojua wao.

CAMFED (Campaign for Female Education)
Duh
 
CAMFED (Campaign for Female Education) ni shirika lisilo la kiserikali (NGO) linalojikita katika kuwezesha wasichana kutoka familia maskini kupata elimu bora na endelevu hasa vijijini katika nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Lengo kuu ni kuvunja mzunguko wa umasikini kupitia elimu ya mtoto wa kike.

CAMFED ni nani?

Ilianzishwa mwaka 1993 nchini Uingereza, na imekuwa ikifanya kazi katika nchi kama Tanzania, Ghana, Zambia, Zimbabwe, na Malawi.

Ilianzishwa kutokana na uhitaji mkubwa wa kuelimisha watoto wa kike waliokuwa wakiachwa nyuma kwa sababu ya umasikini, mimba za utotoni, kazi za nyumbani, na ukosefu wa vifaa vya shule.

---

Wanafanya kazi kwa utaratibu gani?

1. Kutoa msaada wa moja kwa moja kwa wasichana

Wanalipia ada za shule, sare, vitabu, taulo za kike, na gharama nyingine muhimu za elimu.

Wanaunga mkono elimu ya sekondari hadi chuo kikuu au elimu ya ufundi.

2. Kushirikiana na jamii

Wanatengeneza mitandao ya wanawake na jamii kama vile:

Teacher Mentors (walimu wa kuwaelekeza wasichana).

Community Champions (wanajamii wanaosaidia kufuatilia na kusaidia wanafunzi).

Parent Support Groups (vikundi vya wazazi kusaidia watoto wa shule).

3. CAMFED Alumnae Network (CAMA)

Huu ni mtandao wa wasichana waliowahi kusaidiwa na CAMFED.

Wanawake hawa huendelea kusaidia wengine kijamii, kuwa waalimu, wakufunzi, au hata viongozi wa jamii.

Hutoa mafunzo ya ujasiriamali na uongozi.

4. Kuwezesha kiuchumi

Wanatoa mafunzo ya stadi za maisha, ujasiriamali, na kusaidia kuanzisha biashara ndogo kwa wale waliomaliza shule.

Wanatoa mikopo midogo kwa wasichana na wanawake kujiendeleza.

5. Kufuatilia maendeleo

Wanatumia mifumo ya kidigitali kufuatilia mafanikio ya kila msichana na kutoa msaada unaoendana na mahitaji.

---

Faida kubwa ya CAMFED:

Wanazingatia muktadha wa jamii husika.

Wanaongeza uongozi wa wanawake katika jamii.

Wamefadhili zaidi ya milioni moja ya wasichana kwenda shule hadi sasa.

---

Kama uko Tanzania na ungetaka kufaidika au kushirikiana nao:

Wana ofisi ya CAMFED Tanzania.

Mara nyingi wanashirikiana na wizara ya elimu, halmashauri, na mashule ya kata.

Wanaweza kuwa na wawakilishi wa mikoa wanaoshirikiana na shule moja kwa moja.
 
Camfed ni watu gani hawa? Wana fanya kazi kwa utaratibu gani?

Anae wafahamu vizuri ni nani?

How comes mnamuandikisha mtoto kwenye mpango wa kumsomesha kwamba anaishi kwenye mazingira magumu bila kuwashirikisha wazazi wake?

Mimi baba Nina uwezo wa kumsomesha mtoto wangu. Ghafla naambiwa mtoto wako eti yupo chini ya Camfed?

Mlikuja saa ngapi nyumbani kwangu kuthibitisha kwamba mimi Sina uwezo hadi mumuandikishe mwanangu kwenye programs zenu?

Yani kweli Mimi kabisa nishindwe kumsomesha mwanangu shule ya Kayumba? kweli?

Matusi makubwa sana haya
Sasa tumekuta mtoto shuleni ana viraka matakoni tukaona tumwandikishe. Sasa baba mwenye uwezo unashindwaje kumnunulia mtoto uniform aisee?
 
Camfed ni watu gani hawa? Wana fanya kazi kwa utaratibu gani?

Anae wafahamu vizuri ni nani?

How comes mnamuandikisha mtoto kwenye mpango wa kumsomesha kwamba anaishi kwenye mazingira magumu bila kuwashirikisha wazazi wake?

Mimi baba Nina uwezo wa kumsomesha mtoto wangu. Ghafla naambiwa mtoto wako eti yupo chini ya Camfed?

Mlikuja saa ngapi nyumbani kwangu kuthibitisha kwamba mimi Sina uwezo hadi mumuandikishe mwanangu kwenye programs zenu?

Yani kweli Mimi kabisa nishindwe kumsomesha mwanangu shule ya Kayumba? kweli?

Matusi makubwa sana haya
Hilo lipo kwa ajili ya watu kujipigia misaada kwa migongo ya watoto wenu unakuta bajet inasoma full package wao wanamletea midoli ya viatu na Miche ya sabuni

All in all wako vizuri kuna rafiki zangu ni manesi sasa hivi kwa ajili ya hao camfed wana connection ya uhakika wakikusomesha
 
Pole mkuu - Ila kuna swali la kijinga linanijia.
 
God forbid!

Sina vitu vyote hivyo. Mimi mzima wa afya na Nina uwezo wa kumsomesha mwanangu. Kwanini mwanangu aingizwe Camfed bila ridhaa yangu?

Huo si udhalilishaji?
Unazingua kutoa hela ya pencil au unatoa kwa kelele sana. Mwanao kaona ajiandikishe huko asipate tabu
 
Camfed ni watu gani hawa? Wana fanya kazi kwa utaratibu gani?

Anae wafahamu vizuri ni nani?

How comes mnamuandikisha mtoto kwenye mpango wa kumsomesha kwamba anaishi kwenye mazingira magumu bila kuwashirikisha wazazi wake?

Mimi baba Nina uwezo wa kumsomesha mtoto wangu. Ghafla naambiwa mtoto wako eti yupo chini ya Camfed?

Mlikuja saa ngapi nyumbani kwangu kuthibitisha kwamba mimi Sina uwezo hadi mumuandikishe mwanangu kwenye programs zenu?

Yani kweli Mimi kabisa nishindwe kumsomesha mwanangu shule ya Kayumba? kweli?

Matusi makubwa sana haya
Watoto wanaishi mazingira magumu wanaonekana hata kuwaangalia tu. Labda humpatii mahitaji ya msingi hadi kuonekana anatokea familia maskini.
 
God forbid!

Sina vitu vyote hivyo. Mimi mzima wa afya na Nina uwezo wa kumsomesha mwanangu. Kwanini mwanangu aingizwe Camfed bila ridhaa yangu?

Huo si udhalilishaji?
Kama unajiweza nenda shuleni ukiwa na barua ya kuomba mwanao atolee kwenye ufadhili huo.

Lakini Walimu walikuka utaratibu.

Maana walipaswa wawaite wazazi kabla a ufadhili kuanza wawape taarifa na Elimu kuhusu Shirika Hilo.

Hivyo andika barua ipeleke shuleni au nenda kwa afsa elimu wilaya kwenye halmashauri yako utapata maelezo zaidi
 
Thank you
 
Hawa ni watu wanao jipiga tu kifua unakuta mtoto sare za shule zote zimejaa viraka soksi hana viatu vinapiga miayo hata ungekuwa wewe mwalimu kwanini usimwandikishe mtoto wako kuwa anatokea mazingira magumu?
 
Camfed ni watu gani hawa? Wana fanya kazi kwa utaratibu gani?

Anae wafahamu vizuri ni nani?

How comes mnamuandikisha mtoto kwenye mpango wa kumsomesha kwamba anaishi kwenye mazingira magumu bila kuwashirikisha wazazi wake?

Mimi baba Nina uwezo wa kumsomesha mtoto wangu. Ghafla naambiwa mtoto wako eti yupo chini ya Camfed?

Mlikuja saa ngapi nyumbani kwangu kuthibitisha kwamba mimi Sina uwezo hadi mumuandikishe mwanangu kwenye programs zenu?

Yani kweli Mimi kabisa nishindwe kumsomesha mwanangu shule ya Kayumba? kweli?

Matusi makubwa sana haya
Camfed hawana tatizo tatzo lipo kwa wale wanaopokea misaada kukuletea ww hawo mara nyingi Huwa wanaandika watu wenye uwezo ili wakwepe kukuletea misaada waipige
 
Hiyo ni nuksi mkuu. Nuksi kubwa sana. Kataa kabisa hiyo nuksi
Kuilaumu CAMFED unakosea.....wa kumlaumu ni mwanao.

Camfed haisajili watoto, bali hutoa matangazo shuleni kisha mchakato wa kuwapata watoto unaanza, na watoto huwa hadi wanahojiwa hali za nyumbani

Inawezekana mwanao kasema umedanja 😂😂😂
 
Back
Top Bottom