Cameroon: Watu 22 wapoteza maisha katika shambulio la kijiji

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Watu takribani 22 wameuawa katika shambulio la kijiji kimoja kaskazini-magharibi mwa Cameroon, Umoja wa Mataifa (UN) umesema.

Zaidi ya nusu ya waliouawa katika kijiji cha Ntumbo walikuwa ni watoto.

Vyombo vya habari vya nchini humo vinadai kuwa baadhi walichomwa moto mpaka kufikwa na umauti.

Hakuna kundi lolote ambalo mpaka sasa limethibitisha kutekeleza mauaji hayo yaliyotokea Ijumaa iliyopita.

Serikali ya Cameroon pia mpaka sasa haijatoa tamko lolote juu ya shambulio hilo.

Kumekuwa na mapambano katika eneo hilo baina ya serikali na waasi wanaotaka kujitenga na nchi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu sasa.

Afisa wa wa UN James Nunan, kutoka taasisi ya UN ya kukabiliana na majanga ya kibinaadamu ameiambia BBC kuwa mama mjamzito alikuwa ni mmoja wa waliouawa.

"Bila kujali kundi gani limefanya hivi, wametishia kuwa machafuko yataendelea," amesema na kuongeza: "Watu tuliozungumza nao wameumizwa na kushtushwa sana."

Chama kimoja cha upinzani kimetoa tamko nna kulaumu "utawala wa kidikteta" na mkuu wa majeshi ya Cameroon kwa shambulio hilo.

Watoto 14 wakiwemo tisa wa chini ya miaka mitano, pia ni miongoni mwa waliouawa, amesema bwana Nunan.

Afisa huyo anadai kuwa tukio hilo limewaogopesha wenyeji wa eneo hilo.

Moja ya viongozi wa juu wa vuguvugu la kujitenga Agbor Mballa, pia amelaumu "majeshi ya serikali kuhusika."

Afisa mmoja wa jeshi, ambaye amehojiwa na shirika la habari la AFP amekanusha madai hayo.
 
Africa kweli bara la Giza....! Sasa badala ya kupambana na askari wenye silaha ambao ni pinzani kwake, mtu anaua watoto na wanawake ambao hata kujitetea hawawezi.
 
Back
Top Bottom