Calexit- Jimbo la California laanza (jitihada) kujiondoa USA!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Siyo bure, huyu Donald Trump kuna jambo kubwa sana liko nyuma ya pazia ambalo hatulifahamu, sasa Jimbo kubwa na tajiri kabisa klk yote USA limeanza mchakato ya kujitenga na USA, sasa hivi wanakusanya saini za wakazi wa Jimbo hilo kama idaidi inayokubalika kisheria ikifikia basi kura ya maoni ya wana California itaitishwa ili kuamua kama wanataka kubaki USA au kujitenga, kisa na mkasa ni Donald Trump!

Tunaambiwa kwamba Raisi wa USA hana nguvu na madaraka makubwa, iweje mpaka wafikie hatua ya kufikiria kulitenganisha Jimbo kubwa na muhimu kama California kama waliweza tu kuzuia maamuzi yake?


1427862_3_californiarepublic.jpg



'Calexit' can start collecting signatures
 
Hii inanikumbusha akina Chief Mareale na wenzake walipoiomba serekali ya Mkoloni muingereza kuigwa Moshi ili iwe nchi tofauti na Tanganyika.

Jee nao leo wanaweza kusanya maoni ya wana Kilimanjaro na wakaamua kujitenga
 
Tatizo la Trump baadhi ya Sera zake anaingizwa mkenge na Russia ili tutakuja kuliona baadae kabisa.......

Lakini yeye anajifanya mjuaji wa kila kitu.............

Kila kitu anachokifanya toka amekuwa Rais kinakuwa na negative impact kwa marekani na wamarekani sana kuliko positive impact..........

Mfano swala la migrants anajua kabisa kuwaondoa watu 11 milioni ambao ni immigrant itasababisha kuyumba kwa uchumi maana Matajiri wa marekani waliwatumia kuwafanyia kazi kwa malipo kidogo au wastani ukilinganisha na wazawa...........

Mfano kwenye mashamba ya mahindi kule kuna sehemu wakati wa mavuno mpaka wapatikane hawa watu walipwe ujira kidogo ndio wavune mazao.......

Anasahau pia kuwa wazawa sio wachapa kazi kama walivyo wageni wazawa siku zote uwa wanachagua kazi za kufanya na wengi usimamia mali za wazazi wao kama ilivyokuwa kwake......

Hawana exposure kama wageni wanavyo fight maisha tuwe wakweli hata huko Tanzania Dar es salaam ukiona walioijenga sio wazawa wa hapo either ni Wapemba,Wachaga au wahaya lakini wazawa kama Wazaramo wapo wapo tu kupigania Urithi na kufunga ndoa na viduku kila siku hawana exposure...........

Kichekesho ni kuwa hata yeye makampuni Yake yalikuwa yanaajiri immigrant kutoka hasa ulaya .......

Jamaa anachekesha kweli huyu

Sizani kama vyombo vya usalama vitakubali upuuzi huu.....
 
Tatizo la Trump anatumika na Russia.....

Lakini yeye anajifanya hatumiki........

Kila kitu anachokifanya toka amekuwa Rais ni negative impact kwa marekani na wamarekani.......

Mfano swala la migrants anajua kabisa kuwaondoa watu 11 milioni ambao ni immigrant itasababisha kuyumba kwa uchumi maana Matajiri wa marekani waliwatumia kuwafanyia kazi kwa malipo kidogo au wastani ukilinganisha na wazawa...........

Mfano kwenye mashamba ya mahindi kule kuna sehemu wakati wa mavuno mpaka wapatikane hawa watu walipwe ujira kidogo ndio wavune mazao..

Kichekesho ni kuwa hata yeye makampuni Yake yalikuwa yanaajiri immigrant kutoka hasa ulaya .......

Jamaa anachekesha kweli huyu

Sizani kama vyombo vya usalama vitakubali upuuzi huu.....


Hata wewe pia ni victim wa upotoshaji mkubwa unaofanywa na Mass media, hakuna mahali Donald Trump aliposema anataka kuwaondoa immigrants, bali amesema illegal immigrants with criminal records au Wahamiaji haramu, kuna tofauti hapo!
 
Basi hauielewi vizuri USA, moja kati ya upekee wa USA tofauti na nchi nyingine, USA Jimbo linaweza kujiondoa kwenye Muungano imeandikwa kabisa Kikatiba! Nchi nyingi Duniani kama siyo zote zenye federal system huwezi kujitenga lkn USA inaruhusiwa maadamu mmefwata utaratibu, kwa maana Kihistoria kabla ya USA haya Majimbo yalikuwa ni nchi zilizojitegemea hivyo waliiingia makubaliano na USA kabla ya kujiunga na hiyo ndiyo tofauti kubwa!

Kaka hakuna kitu kama hicho, Muungano wa kuipata USA ulifanyika kwa hiyari kwa baadhi ya state na damu ilimwagika kwa baadhi ya states Ili kuipata hiyo USA,
Baada ya hapo hakuna states inayoweza kujitenga tena, seal ya USA imeshawekwa
 
Basi hauielewi vizuri USA, moja kati ya upekee wa USA tofauti na nchi nyingine, USA Jimbo linaweza kujiondoa kwenye Muungano imeandikwa kabisa Kikatiba! Nchi nyingi Duniani kama siyo zote zenye federal system huwezi kujitenga lkn USA inaruhusiwa maadamu mmefwata utaratibu, kwa maana Kihistoria kabla ya USA haya Majimbo yalikuwa ni nchi zilizojitegemea hivyo waliiingia makubaliano na USA kabla ya kujiunga na hiyo ndiyo tofauti kubwa!
Haiwezekani kisheria, only through revolution.
 
Ingekuwa rahisi kama barbarosa anavyotaka kutuaminisha hiyo nchi isingekuwepo leo hii, miaka mingi state nyingi zilikuwa zinapigania kujitenga ikiwemo hiyo hiyo stare ya Calfonia ambayo inaamini kuwa inanyonywa kutokana na utajiri iliyonayo na pia inaona kana inabinywa wakati yenyewe ina kila kitu..
 
Hauelewi USA, nimekwambia kujitenga USA inawezekana na inaruhusiwa Kikatiba, na ni rahisi tu kama Jimbo likipiga kura ya maoni na sehemu kubwa ikasema ndiyo tunataka kujitenga ni moja kwa moja, hiyo ndiyo tofauti kubwa na fedaral system nyingine, ndiyo maana kila Jimbo USA lina Sheria zake!

Kaka uwe mwelewa basi, hicho kitu cha state kujitenga hakipo na hakitakaa kutokea ndani ya USA, kweli kila state zina sheria zake, lakini kun Sheria na Katiba mama ya USA, hilo la kujitenga Halipo na Sheria hairuhusu kwa states kujitenga
 
Alafu huo mwisho wa Vote wengi wakitaka Cal Ijitenge ndio watajitenga?
Soma taarifa kutoka kwenye source niliyokupatia. Soma maelezo acha ubishi. State inaweza kujitenga.
Soma hapo maelezo ya kujitenga.
 
Me naona kaja kuisambaratisha marekani na sera zake za mikazo kujifanya anajua kila kitu na aaminicho ndo sahihi, kumbe ajui mrusi sasa ni zake yake kumsarambatisha mmarekani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom