Ujue uchaguzi wa Marekani (USA) na jinsi rais wake anavyochaguliwa

Boi Manda

JF-Expert Member
Oct 26, 2023
388
506
Uchaguzi wa rais wa nchini Marekani ni tofauti sana na chaguzi za nchi nyingine duniani

Kura wanazopiga wananchi hata mgombea wa urais akishindi kwa wingi wa kura hizo hazimuingizi moja kwa moja mshindi huyo madarakani

Kwa kawaida nchini Marekani (USA) uchaguzi wa kumchagua rais wa nchi hiyo na makamu wake hufanyika kila baada ya miaka minne na ni lazima iwe wiki ya kwanza ya mwezi Novemba ni lazima pia iwe Jumanne ya kwanza baada ya Jumatatu

Hivyo kwa kanuni yao hiyo uchaguzi wa mwaka huu 2024 itafanyika Novemba 5 Jumanne ya kwanza ya baada ya Jumatatu

Katika uchaguzi wa mwaka huu mpambano mkali ni kati ya Makamu wa rais wa chama cha Democratic BI. Kamala Harris (60) na mwamba Bw. Donald Trump (78) wa chama cha Republican

Baada ya muda wa kampeni kwisha wananchi wote wa United States of America (USA) hupiga kura hata waliopo nje ya nchi hiyo wenyewe wanaita "Popular Votes or Simple Majority"

Lakini matokeo ya kura hizi za wananchi (Popular Votes) haziwezi kumuingiza rais na makamu wake Ikulu ya kifahari yenye jengo lenye shepu ya yai la white house

Baadala yake Rais wa Marekani na makamu wake wanaingizwa madarakani na wajumbe wapatao 538 kutoka kwenye majimbo 50 yanayounda nchi hiyo tajiri kiuchumi na yenye nguvu kubwa za kijeshi duniani

Iko hivi baada ya wananchi wote kupiga kura (Popular Votes) na kura hizo kuhesabiwa matokeo ya kura hizo yanasaidia kuonyesha jimbo lipi linamuunga mkono mgombea wa chama kipi na kila jimbo kati ya majimbo hayo hutoa mgombea mmoja au zaidi ya mmoja kwa baadhi ya majimbo makubwa na kupatikani wajumbe hao 538

Wajumbe hao 538 ndio watakao piga kura ya "electoral college votes" kuchagua rais wa Marekani na mgombea atakayepata kura 270+ ndiye atakuwa mshindi wa urai wa nchi hiyo ambapo ni zaidi ya nusu ya kura kutoka kwa wajumbe hao 538 kutoka kwenye majimbo 50 ya USA

Baada ya kura hizo za electoral Votes kupigwa na kutoa mshindi zitahesabiwa na kuidhinishwa na bunge la Congress la nchi hiyo ambalo ni bunge la "Mabwanyeye" (Majiri)

Bunge hilo la Congress likishamuidhinisha matokeo hayo rais mpya wa nchi hiyo ataapishwa Januari mwakani tayari kwa kuanza kazi ya kutumikia wanachi wa Marekani

Katiba ya nchi hiyo inatoa muda huo mrefu wa rais aliyechaguliwa kuanza kazi ili kupisha kama kuna mapingamizi ya mgombea mmoja kutoridhika na matokeo hayo kwenda mahakamini kupinga matokeo hayo

Hivyo ndivyo rais wa Marekani na makamu wake wanavopakina

Comasava.
 
Nadhani mleta mada kuna nanna haufahamu uchaguzi wa USA kiuhalisia, ni kama umekaririshwa fulani au ameandika kinadharia mnoo hata kama alichokiandika kuna chembechembe za ukweli.

Kwa kifupi sana, mfumo wa uchaguzi wa USA kumpata raisi wake huamuliwa na wamerekani wenyewe kwa wingi wao na wala sio kweli kuwa mshindi huamuliwa na wajumbe wa Electoral college! Ukishinda Popular votes katika majimbo mengi na muhimu zaidi basi wewe tayari ni mshindi. Kura za wajumbe wa Electoral college ni hitimisho la mchakato wa kura za Popular vote za kila jimbo. Kwanini nasema hivyo, waza haya.

1. Uchaguzi wa USA rasmi (ambapo Popular votes hupigwa) utafanyika siku ya jumanne (5/November) na katika hali ya kawaida kufikia jioni ya siku ya jumatano (6/November) tayari mshindi wa kiti cha urais wa USA atakuwa tayari amejulikana kwa kila mtu dunia nzima, wakati upigaji wa kura za wajumbe wa Electoral college zitakuja kufanyika wiki kadhaa huko baadaye. Kama wajumbe wa Electoral college (independently) huamia mshindi wa urais wa USA, kwanini mshindi ajulikane kabla ya kura zao kupigwa?

2. Hakuna mgombea yoyote wala chama chochote katika USA kinachoweza kupoteza hata dakika moja kuwafuata hao wajumbe wa Electoral college kikiomba kura zao. Yaani hakunaga kampeni za kuwashawishi hao wajumbe wa electoral college. Sio kwamba inakatazwa bali kimsingi hakuna mantiki ya kufanya hivyo.
Sasa Kama hao wajumbe ndio huamua nani awe rais, kwanini wagombea na vyama vyao wasitumie kila resource kuwashawishi hao wajumbe kuliko kutumia hizo resource kusaka popular votes ambazo 'haziamui' nani awe rais?

HITIMISHO LANGU.
Mchakato wa uchaguzi wa USA kumpata mshindi hauna tofauti yoyote ya kimsingi na chaguzi zingine za nchi nyingi za kidemokrasia ya moja kwa moja, tofauti chache zinazoelezwa zipo katika sayansi ya kutafsiri walio wengi ni kina nani au wamepatikanaje. Kwa mfano, katika uchaguzi wa Tz, mshindi wa kiti cha urais ni lazima apate zaidi ya 50% ya kura zote halali, na mshindi wa kiti cha ubunge au udiwani ni yule mwenye kura nyingi zaidi ya wagombea wengine (hata kama mshindi amepata chini ya 9% ya kura zote).
 
Lakini Electoral College imeshatoa Marais watano walioshindwa Popular vote wa karibuni wakiwa George Bush na Trump.
 
Ndio maana yake nimeeleza hapo kuwa popular votes hazimuingizi rais madarakani hata akishida rais anaingizwa madarakani kwa kushinda electoral college votes

Kwa hiyo mgombea anaweza kupata kura chache za wananchi akaja kupata kura nyingi za electoral college votes na kushinda urais
 
Electoral college votes zinapatikanaje?

Kwa nini, kwa mfano, electoral college votes za Florida ni nyingi kuliko za South Carolina?

Nani huamua kwamba hizi electoral college votes za Florida apewe Dr. Cornell West na si Dr. Jill Stein wala Donald Trump?
 
Back
Top Bottom