Cake ya Taifa yazua balaa

Miunda

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
530
180
Wanasiasa Tanzania wazua balaa, kwa kutumia neno cake 🎂 ya taifa. Matukio yaanza kujitokeza.

Mwananchi mmoja kutoka mkowa mmoja jina (********) alikuja dar es salaam kuuza mazao yake, baada ya kumaliza shughuli zake za kujipatia kipato amejikuta akihangaika huku na kule mjini dar es salaam kutafuta cake 🎂 ya taifa.

Mtu huyo kwa jina la Joseph alikutana na mjanja mmoja katika jiji kumuelekeza wapi atapata cake 🎂 ya taifa ili akale na familia yake, mtu huyo alimueleza mwenyeji kuwa amei promised familia yake kuwa akirudi kijijini anarudi na cake 🎂 kwa bei yoyote ili nao wafaidi kama viongozi wa nchi.

Mwenyeji nae hakusita na kumchukua mwananchi huyo hadi katika duka la cake 🎂.
Walipofika mwenyeji alimuomba yule Joseph amsubiri nje ili aweze kumbembeleza mwenye duka wapate 🎂 cake kwani cake ni expensive nani special kwa viongozi.

Baada ya muda mwenyeji kutoka dukani alimuomba Joseph kutoa laki tano, baada ya kutoa laki tano Joseph alipatiwa cake yake ilio andikwa cake ya Taifa na jina lake Joseph.

Joseph aliondoka mjini dar es salaam akiwa na furaha huku akisema nae amekula cake ya taifa.

Tunawaomba wanasiasa nchini, kueleza vizuri kwa wananchi, nini maana ya cake ya taifa, wengi wanafahamu kuwa ni cake 🎂 ya kawaida lakini ni maalumu kwa viongozi. 😀😀😀
 
Back
Top Bottom