Kwa jicho pana Rais yupo nyuma ya Spika.
Mwaka jana alipokea Live ripoti ya CAG na kuichambua madudu kadhaa yaliyoainishwa.
Mwaka huu ni kama hajui kuna ripoti ipo, aliipokea kimya kimya na sekeseke linaloendelea ni kama hasikii.
Siku zote Rais tulie nae kitu anachopinga huwa hanyamazi maana hana kariba ya kujizuia. Ila kwa hili kanyamaza. Ipo sababu.
Hapa ndipo tunasema kwa jicho pana magufuli anamsapoti ndugai, maana madudu yote ni ya uongozi wake, 1.5 trilion, zisizofahamika matumizi ni awamu yake.
Manunuzi yasiofata sheria, zabuni na kadhalika, magufuli apendi kusemwa, anaamini yeye anajua kila kitu. Na ana uwezo wa kila kitu ilimradi tu yeye ni Rais. Kauli zake nyingi huthibitisha hilo.
Sasa anasaka kichwa cha CAG na uwezo wa kukipata hana. Sasa anamtumia yule dhaifu bungeni kufikia lengo.
Rudia kauli ya dhaifu jana. "Eti" CAG akajisalimishe kwa Rais. Na ajiuzuru. Hii ndio nia ya Dhati ya Magufuli, Assad aondoke maana ni kikwazo kwake
Magufuli hapendi kukosolewa wote mnajua ya Lissu, wote mnajua ya Wapinzani leo, wote mnajua kilichompata msajili wa hazina alipotoa maoni ya wazi clouds 360 kuwa kuweka fedha za umma bank kuu kutapunguza mzunguko wa fedha na si kosa kisheria kuweka katika mabenki ya kawaida, aliliwa kichwa.
Dumelang