CAG: Ndege yenye miaka 47 ilikarabatiwa kwa 278.42m ikatumika masaa 18

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,244
103,932
CAG: NGORONGORO ILITUMIA TSH. MILIONI 278.42 KUKARABATI NDEGE YENYE MIAKA 47

Kupitia Daftari la Mali za Kudumu za Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, CAG alibaini kuwa Mamlaka inamiliki ndege aina ya CESSNA 182P yenye Namba za Usajili 5H-MPZ

Ndege hii kufikia Juni 30, 2021 ilikuwa na miaka 47 na ambayo ilikusudiwa kuwezesha doria za usalama ndani na karibu ya Eneo la Hifadhi

Amesema kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2018/2019 hadi 2020/21, Mamlaka ilipanga ndege hiyo ifanye safari kwa saa 900 kwa ajili ya doria za ulinzi lakini iliweza kufanya safari kwa saa 18 tu (asilimia 2) wakati gharama za matengenezo zilizotumika zilikuwa Tsh. 278,420,000
 
Bado kuna watu wanaridhika kutembea na kadi za CCM mifukoni mwao!
Hata Mimi ninayo na vikao vya chama nahudhuria na michango ya hapa na pale natoa.
Mimi ni chadema damu Ila nikifanya matukio ma CCM wanajua ni mwenzao hivyo nahamishiwa idara nyingine.
 
mwe haka hapa kandege kenyewe
images (2) - 2022-04-21T190500.974.jpeg
 
Legacy haitaachwa hata inchi moja bila doa
Mama anahakikisha kalifukia jiwe kwa zege
 
CAG: NGORONGORO ILITUMIA TSH. MILIONI 278.42 KUKARABATI NDEGE YENYE MIAKA 47

Kupitia Daftari la Mali za Kudumu za Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, CAG alibaini kuwa Mamlaka inamiliki ndege aina ya CESSNA 182P yenye Namba za Usajili 5H-MPZ

Ndege hii kufikia Juni 30, 2021 ilikuwa na miaka 47 na ambayo ilikusudiwa kuwezesha doria za usalama ndani na karibu ya Eneo la Hifadhi

Amesema kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2018/2019 hadi 2020/21, Mamlaka ilipanga ndege hiyo ifanye safari kwa saa 900 kwa ajili ya doria za ulinzi lakini iliweza kufanya safari kwa saa 18 tu (asilimia 2) wakati gharama za matengenezo zilizotumika zilikuwa Tsh. 278,420,000
Hela ya kununua dash 8 mbili na chenji inabaki
 
Hela ya kawaida kwa matengenezo ya ndege!

Unalosema ni kweli. Je unajua kwanini ilifanya masaa 18 tu?? Vipi kama ilikuwa de-commissioned baada ya matengenezo ya gharama hiyo?

Pamoja na kuwa taarifa ya bandiko sio kamili lakini huwezi kusema gharama ya matengenezo ni sahihi bila kuangalia nini kimefuata baada tu ya matengenezo hayo.
 
CAG anaimba kwaya Hakuna hatua zozote zitakazochukuliwa anachofanya ni uchonganishi wa serikali na wananchi
 
Mjomba Magu hakujua hesabu ya uhasibu,wakatumia nafasi hiyo wakanufaika.
Always utilize government assigned assistance, not ONE MAN SHOW.
 
Back
Top Bottom