Shondola
Member
- Apr 2, 2014
- 95
- 58
Kila kunapokucha Taifa letu linaendelea kuingia katika giza tororo hasa kutokana na baadhi wa wale walioaminiwa na Raisi kuhakikisha kuwa wanaendelea kuziacha Wizara zikiwa hoi kutokana na Ufisaidi wa kutisha.
Kabla hata swala la Escrow halija futika katika mioyo na fikra za Watanzania jambo ambalo limepelekea baadhi ya Mawaziri kuwajibishwa sasa limeibuka lingine kubwa na la aibu.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali amependekeza hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya Dkt. John Pombe Magufuli (Waziri wa Ujenzi) na Dkt. Harrison Mwakyembe (aliyekuwa Naibu Waziri) kutokana na Ufisaidi unaofikia kiasi cha Shilingi Bilioni 256.
Hoja hii ilishawahi kuibuliwa Bungeni ila kama kawaida yake Magufuli aliizima kiujanja ujanja jambo ambalo sasa limeibuka upya na CAG kujiridhisha kuwa majibu waliyoyatoa Waziri hayakiwa na usahihi wowote hivyo alilidanganya Bunge na fedha hizo hazijulikani zilikopelekwa kwa kuwa hakukuwa na barabara mpya zilizojengwa na kama haitoshi madeni ambayo Magufuli alisema yamelipwa hayaendani ama kulingana na kiasi hicho cha zaidi ya Bilioni 256.
Akizungumza na Gazeti la Mwananchi Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya PAC Mhe. Zitto Zuberi Kabwe amesema huwa ana mashaka sana na majibu ya Magufuli manake kujiamini kwake hupelekea watu wengi kumwani hivyo hata anapofanya mambo ya hovyo watu hucheka na kumpigia magofi.... Hivyo yale majibu aliyoyatoa Bungeni kipindi kile hakuyaamini na kuamua kuendelea kulifuatilia jambo ambalo sasa limeibua ukweli kwamba Magufuli alilidanganya Bunge na hili halivumiliki hata kidogo lazma hawa mabwana sasa wakatujibu Bungeni na wajiandae kuwafuata wenzao kwa kuwajibika.
Itakumbukwa kuwa Magufuli amekuwa akitunukiwa jina la "The Chosen" kwamba ndiye anayetakiwa kumrithi JK baadhi ya watu wakisema kwamba huyu bwana ni msafi kumbe ndo yale yale waliwahi kuyasema wahenga Usilolijua ni kama usiku wa kiza........
Kama ilivyokuwa kwa Escrow sasa hili nalo Watanzania wanalisubiri kwa hamu kubwa.
Chanzo: Mwananchi