CAG Ludovick Uttoh apendekeza nafasi yake iwe ya kuchaguliwa na bunge

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,171
3,346
CAG amependekeza nafasi yake iwe ya kuchaguliwa badala ya ilivyo ya kuteuliwa na Rais.

Akifafanunua zaidi, kuwa taatifa zake haziishii kwa Rais bali bunge la JMT na kusisitiza ni bora awe anachaguliwa toka huko.

Ukiichunguza kauli hii ya CAG kitaalamu ni kama anataka uhuru zaidi katika utendaji wake wa kazi tofauti na ilivyo sasa kwa kuwa mteule wa Rais ni kama kama ina "impair independence" yake.

Wadau nini maoni yenu kuhusiana na kauli hii ya Uttoh??
 
bahati yake katiba inamlinda kidogo namna ya kumuondoa inakuwa ngumu kidogo, yangemkuta ya tiddo muhamdo.
 
Sijakuelewa Mkuu. Unamaanisha CAG achaguliwe na wabunge au achaguliwe toka ndani ya bunge? Mimi siungi mkono hayo mapendekezo yote mawili. Napendekeza nafasi ya CAG iwe inatangazwa kwa uwazi kabisa na watu wenye uwezo waombe kisha wafanyiwe usaili wa wazi na mshindi ateuliwe na rais kisha athibitishwe na bunge.
 
  • Thanks
Reactions: ESI
Napendekeza nafasi ya CAG iwe inatangazwa kwa uwazi kabisa na watu wenye uwezo waombe kisha wafanyiwe usaili wa wazi na mshindi ateuliwe na rais kisha athibitishwe na bunge.
naunga mkono hii hoja, hii kuteuliwa teuliwa ina madhara yake kiutendaji
 
  • Thanks
Reactions: ESI
Sijakuelewa Mkuu. Unamaanisha CAG achaguliwe na wabunge au achaguliwe toka ndani ya bunge? Mimi siungi mkono hayo mapendekezo yote mawili. Napendekeza nafasi ya CAG iwe inatangazwa kwa uwazi kabisa na watu wenye uwezo waombe kisha wafanyiwe usaili wa wazi na mshindi ateuliwe na rais kisha athibitishwe na bunge.

Good idea!
 
  • Thanks
Reactions: ESI
Ni wazo zuri,ingawa wasiswasi wangu ni kuingiza siasa kwenye professional!
 
Hii maana yake ni kuwa ludovic kagundua baadhi ya mambo kuwa hayaendi sawa kutokana na kuingiliwa katika kazi yake pengine na idara ya raisi
 
Hii maana yake ni kuwa ludovic kagundua baadhi ya mambo kuwa hayaendi sawa kutokana na kuingiliwa katika kazi yake pengine na idara ya raisi

Alitakiwa apendekeze kua nafasi itangazwe watu waombe, ipitishwe interview ya nguvu, washindi watatu wapelekwe kwa raisi, raisi ateuwe mmoja kati ya hao, na mwisho ndo asibitishwe na bunge. Kama itaenda kinyume na hapo hakuna chochote zaidi ya siasa.
 
Sikio la kufa halisikii dawa,baada ya sheria mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya ukaguzi ya 2008.CAG amepunguziwa madaraka
 
CAG anatakiwa apendekeze kwa mapana. Kwa kuwa yeye anakagua ofisi za umma anafahamau ofisi nyingine nyingi za umma ambazo zinakosa uhuru wa kiutendaji kwa kufunikwa na uteuzi wa Ikulu.

Ni vema aziainishe kwa kuzitaja na ofisi hizo pia. Asitaje tu Ofisi yake wakati anajua anapata mzigo mkubwa wa kazi kwa sababu ofisi nyingi watendaji wanaboronga kwa sababu ya kufanya kazi kwa uzembe, wizi na ubadhirifu ili kuwafurahisha waliowateua.

Nafasi za watendaji wakiwamo wakuu katika Ofisi hizo zitangazwe, wenye sifa waombe, usaili ufanyike kwa uwazi, wenye kustahili washinde na hatimaye wapate idhini ya Bunge.

Baadhi ya Ofisi hizo ni hizi zifuatazo;-

1. Mwanasheria Mkuu

2. Jaji Mkuu

3. Inspekta wa Jeshi la Polisi, Magereza, Uhamiaji

4. Controller Of Budget

5.CAG

6.Tume ya Taifa ya Uchaguzi,

7. PCCB, etc.

Kwa kuwa ofisi hizi kwa umuhimu wake ni nyingi na nyeti, unahitajika umakini na mchakato wa kutosha kuziainisha.

Nchi nyingine, utaratibu huu ni wa Kikatiba.
 
ateuliwe na Raisi wa JMT. CAG akiboronga utakimbizana na wabunge (wa CCM), wewe tazama jinsi Spika wa Bunge aliechaguliwa na wabunge jinsi anavyoharibu.. ni bora achagulie na Rais, akiboronga Rais hasiwe na ksingizio cha kumbadilisha ....
 
Kama Bunge leneywe ndo la kishabiki, hakuna manaam, ni mpaka hapo bunge halipo biased!
 
Kauli yako ni nzuri ila some editting pls.
Bunge litumike kumpitisha tuu uyo CAG na awajibike kwa bunge na si kwa Raisi wa JMT maana kama madudu ya serikali alafu unaenda mpelekea mkuu wa serikali iyo iyo ambayo mhimili wake umeharibu kuna mambo atakuambia weka kapuni.
 
CAG amependekeza nafasi yake iwe ya kuchaguliwa badala ya ilivyo ya kuteuliwa na Rais.

Akifafanunua zaidi, kuwa taatifa zake haziishii kwa Rais bali bunge la JMT na kusisitiza ni bora awe anachaguliwa toka huko.

Ukiichunguza kauli hii ya CAG kitaalamu ni kama anataka uhuru zaidi katika utendaji wake wa kazi tofauti na ilivyo sasa kwa kuwa mteule wa Rais ni kama kama ina "impair independence" yake.

Wadau nini maoni yenu kuhusiana na kauli hii ya Uttoh??

Ninampongeza Utouh kwa kuliona hilo.Kwa uteuzi wake alionao akikurupushwa na aliyemteua anaweza asiifanye kazi yake kw akiwango kinachotakiwa au akafanya kazi ili kuendelea kupata mshiko wa uteuzi.Lakini ningemuona anasimamia anachokiongea pale ambapo angeamua kujiuzulu baada ya kuliona hilo.
 
CAG amependekeza nafasi yake iwe ya kuchaguliwa badala ya ilivyo ya kuteuliwa na Rais.

Akifafanunua zaidi, kuwa taatifa zake haziishii kwa Rais bali bunge la JMT na kusisitiza ni bora awe anachaguliwa toka huko.

Ukiichunguza kauli hii ya CAG kitaalamu ni kama anataka uhuru zaidi katika utendaji wake wa kazi tofauti na ilivyo sasa kwa kuwa mteule wa Rais ni kama kama ina "impair independence" yake.

Wadau nini maoni yenu kuhusiana na kauli hii ya Uttoh??

Naona ametoa wazo zuri lakini siyo kuchaguliwa kutoka huko bali office ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali inatakiwa iwe chini ya Bunge ili kuongeza uhuru wake lakini pia kuonyesha kwamba inalisaidia bunge katika oversight role. Lakini hapa Utouh aelewe kwamba hii haiiondolei serikali kuwa na auditor general wake ambaye atakuwa anatoa ripoti ya serikali kwa rais kwa sababu rais ndiyo kama CEO. Kwa sababu serikali haina uhakika kama sera zake na fedha zake zinatumika vilivyo basi watahitaji auditor general wa kwao. Ila Bunge halimhitaji huyu. Bunge linamhitaji auditor wa kwao ili aweze kuwasaidia kuonyesha kwamba yale maamuzi yanayopitishwa na bunge (ikiwemo fedha) yanafanyiwa kazi kama ilivyoidhinishwa na bunge. Maana wabunge wanawakilisha wananchi hivyo wanatakiwa wachague auditors kama vile kwenye mashirika ambapo auditors huteuliwa na shareholders

Sasa sijui Utouh anaweza kukubali kwamba yeye awe wa bunge na mwenzie achukue nafasi ya auditor wa serikali au anataka vyovyote?
 
Back
Top Bottom