Has
genious answer ndio maana kubana matumizi vifeUchumi ungedorora vyama vya siasa visingepata ruzuku!
genious answer ndio maana kubana matumizi vifeUchumi ungedorora vyama vya siasa visingepata ruzuku!
Na hapo ndio pananifanya nisiwe na wasiwasi, maana uchumi wetu ni imara mara 7 ya ule wa Marekani.Kuna nchi wana 278% na bado wanakopeshwa kinachoangaliwa ni uimara wa uchumi na rasilimali zilizopo!
CAG.....76% is not just a reason....the reason here is China, hii ndiyo nchi hatari sana duniani kwasababu ya njia ya Urubuni wao juu ya uchumi wa nchi maskini na zenye tawala mbaya barani Africa. Hawa wana-override sheria na taratibu zozote ili mradi waweze kuingia kwenye rasilimali yoyote ilie iwayo hata chumba kimoja anachoweza kuishi Mchina mmoja.
Kwa ufupi
Rais alitoa ufafanuzi huo baada ya awali, Profesa Assad kutahadharisha kwamba kiwango cha deni hilo kilichofikia cha Sh46trilioni kutoka Sh41trilioni kwa mwaka uliopita (2015/16)
Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemtoa wasiwasi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kuhusu Deni la Taifa, akisema nchi inakopa fedha na kuzitumia kutekeleza miradi ya maendeleo.
Akizungumza jana Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akipokea ripoti ya ukaguzi ya CAG mwaka 2016/17, Rais Magufuli alisema uwekezaji katika miradi mikubwa ya miundombinu, ikiwamo ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na mradi wa umeme wa Stieglers Gorge, utasaidia kukuza uwezo wa Serikali kulipa deni hilo.
Rais alitoa ufafanuzi huo baada ya awali, Profesa Assad kutahadharisha kwamba kiwango cha deni hilo kilichofikia cha Sh46trilioni kutoka Sh41trilioni kwa mwaka uliopita (2015/16) sawa na ongezeko la asilimia 12, kinatia wasiwasi na kwamba Serikali inatakiwa kuchukua hatua kupunguza ukubwa wa deni hilo.
“Tulichosema hapa kwa kweli ukuaji wa deni tunasema ni himilivu lakini jinsi linavyoongezeka, tunakaribia maeneo ya wasiwasi. Asilimia 72 ya GDP (Pato la Taifa) si mbaya lakini ikifika asilimia 76 ya nchi nyingine zimepata shida, inabidi tuangalie sasa namna gani tunaweza ku-control (kudhibiti) ukuaji wa deni hilo,” alisema Profesa Assad.
Katika ufafanuzi wake Rais Magufuli alisema miradi hiyo mikubwa imechagiza baadhi ya wahisani kujenga matumaini ya kuendelea kutoa ushirikiano na wameanza kurejea baada ya kuona Serikali ikiitekeleza kwa kutumia fedha za ndani.
Alisema Serikali inazo fedha za kutosha kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa reli ya kisasa na umeme.
Akitoa maoni yake kuhusu deni hilo, Profesa wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Humphrey Moshi alisema wasiwasi wa deni hilo unaweza kuchagizwa na aina ya mkopo, akisema ipo ya riba nafuu ya marejesho ya muda mrefu.
“Tunaita non- concessional, lakini kuna mikopo ya riba kubwa,” alisema.
Alitaja mambo matatu ya kuzingatia katika kudhibiti ukuaji huo wa deni kuwa ni pamoja na kuangalia upya mikataba ya misamaha ya kodi kwa kampuni za kigeni nchini.
Alisema tafiti kadhaa zinaonyesha misamaha hiyo inatengeneza mazingira ya Taifa kuibiwa kodi.
“Pili, Serikali inatakiwa kuongeza kasi ya udhibiti ukwepaji kodi na kasi ya ukusanyaji kodi, lakini (tatu) Serikali inatakiwa kutekeleza miradi haraka inayotokana na mikopo ili kuepuka mazingira ya ufisadi.”
Chanzo: Mwananchi
Thank you. This is a wonderful piece of observation and advice. Kitu cha kujiuliza je hizo pesa tunazokopa zinaenda kwenye miradi ipi? Serikali inatuchanganya maana kila siku miradi ya SGR na Stieglers Gorge tunaambiwa inajengwa kwa fedha zetu za ndani; wakati huo huo utetezi wa kukopa ni kutekeleza miradi hii hii mikubwa. Na deni linaendelea kupanda! Je tunakopa kwa ajili ya miradi ipi?CAG nimemuelewa, kwasababu by defacto ni "mchumi". JPM pia nimemuelewa, kwasababu si "mchumi" kama mwenyewe anavyosema. Ila huyu profesa wa UD ndio sijamuelewa kabisa. Sidhani kama kwa sasa nchi hii tuna tatizo la kukwepa kodi. Nadhani kwa sasa tuna tatizo la kutotengeneza vyanzo vingi vya kutoza kodi.
Kimsingi kodi haipaswi kutozwa katika any economic activity bali kodi yapaswa kutozwa kwenye "profitable" economic activities. Profesa anaposema miradi itekelezwe haraka kuepuka ufisadi sijui anamasnisha nini hapa. Jambo la msingi katika mikopo ni "sensible" predictable returns kule hizo pesa zinakoelekezwa. Reli, Stiglers Gorge ni miradi mizuri lakini lazima tukubali yote ni derived demand nature. Return kutoka katika miradi hiyo inategemea na other government policies, siyo yenyewe kama ilivyo.
Fine, tunataka tuwe na umeme mwingi ili utumike kwenye viwanda vyetu. Tunataka SG ili tusafirishe bidhaa zetu za kilimo na viwanda. Lakini cause-impact siyo "having enough electricity implies many industries". Kuna factor nyingine nyingi zinazotakiwa kuchochea uanzishwaji wa viwanda.
Government should avoid single direction policy! Inclusive government policy is needed ili kufikia kile tunachokipata. Inclusive government policy lazima ijumuishe hard policy and soft policy.
Hata wewe usingeenjoy mb za Ufipa!!...... Hahahaa natania Ova!Akili zenu finyu mko radhi mtete ujinga wowote ule
Ova
Ina maana CAG hajaona viwanda kila mahali,hajaona watu walivyouawa Kibiti.
Haaaa haaaa nawaza kama Pascal Mayalla
c.c BAK
Rais Magufuli kapewa adhabu ya kuwa na ndimi mbili.Mbona sielewi elewi!! Watuambie vizuri upandaji wa hili deni!
SI walishatuambia miradi mikubwa nchini kama vile ujenzi wa reli; tunatumia mapato yetu wenyewe?!
Kwa muda mrefu niliamini Mzee wa Msoga ni bonge la msanii lakini mbele ya Jecha Palamagamba Muhongo; Mzee wa Msoga tupa kule!Rais Magufuli kapewa adhabu ya kuwa na ndimi mbili.
Tuendelee kumlilia Mungu ampe mapigo zaidi