CAG amkalia kooni Msekwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CAG amkalia kooni Msekwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jozzb, Apr 16, 2012.

 1. j

  jozzb Member

  #1
  Apr 16, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  RIPOTI ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imeisonda kidole Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa kwa kuingilia utendaji wa Bodi ya Hifadhi hivyo kuipunguzia uhuru menejimenti ya hifadhi hiyo.

  Bodi hiyo ni moja ya mifano aliyoitoa CAG Ludovick Utouh, kuwa baadhi ya Bodi za Wakurugenzi kuingilia kazi za Menejimenti na wajumbe wa Bodi katika baadhi ya mashirika mbalimbali ya umma wamekuwa wakijihusisha katika utendaji wa kazi za menejimenti.

  “Kitendo hiki ni kasoro kubwa na inapunguza uhuru wa menejimenti kutoka kwa Bodi na inaleta migongano ya kimaslahi kati ya pande hizi mbili,” inasema ripoti hiyo ya CAG. CAG alitoa mfano wa kasoro kama hii ilionekana katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ambapo Bodi ya Wakurugenzi ilijihusisha mara kadhaa katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii katika kipindi kati ya Julai, 2010 na Juni, 2011.
  Ripoti inasema hali hiyo ni kinyume cha utawala bora na waraka wa Ikulu namba SHC/B.40/6/21 wa tarehe 28/03/1994 aya ya 3 na 5. “Utaratibu huu huathiri kazi za bodi za usimamizi kwa kuwa zitakuwa zimegawanyika kimtazamo,” alieleza Utouh katika ripoti zake alizowasilisha bungeni wiki iliyopita.”
  AG anadai kuwa inapotokea kutotekelezwa majukumu ya kiutendaji yaliyotolewa kwa wajumbe wa Bodi, wajumbe wa Bodi hawatakuwa na nguvu ya kufuatilia na kudai maelezo juu ya kushindwa kufikiwa kwa malengo hayo, na hivyo Bodi itabaki kufanya maamuzi yanayolinda maslahi yao katika utendaji wa mamlaka husika.
  Pia ripoti hiyo imesema baadhi ya viongozi wamekuwa wanavunja sheria za nchi katika uteuzi wanaoufanya kutokana na kuteua wajumbe wengi katika baadhi ya bodi za wakurugenzi kinyume cha sheria za uanzishwaji wa mashirika husika.

  SOURCE: HABARI LEO
  CREDIT: MPEKUZI << CAG amkalia kooni Msekwa.>>


   
Loading...