CAG amgusa Sirro mfuko wa maafa

CAG amgusa Sirro mfuko wa maafa

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG Charles Kichere ameendelea kuibuka madudu na safari hii ametuarifu kuwa aliyekuwa IGP Sirro ambaye sasa ni Balozi wa Tanzania Nchini Zimbabwe anahusishwa na upotevu wa Tsh bilioni 4.8 ambazo ni fedha za Mfuko wa Maafa.

CAG Kichere ameeleza kuwa IGP Sirro ndiye alikuwa mwangalizi wa mfuko huo, uongozi ukiwa chini ya Mwenyekiti na Meneja.

Miaka mitano ilipita bila kuwa Sekretarieti ya mfuko wala kufanya vikao na mikutano mikuu ya mwaka ya wanachama na fedha za mfuko kutoweka katika mazingira ya kutatanisha.

“Usimamizi huu mbovu ulisababisha ubadhirifu wa Sh2.44 bilioni kutoka kwenye Mfuko. Napendekeza hatua za kinidhamu na kisheria zichukuliwe chidi ya watu wote waliohusika na uba dhirifu huo wakiwemo wale waliotoroka” CAG Charles Kichere
 
Back
Top Bottom