CAG aikana ripoti feki ya NSSF, asema ripoti itatolewa na Bunge Aprili 25

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
51,145
40,092
OFISI ya Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imekana taarifa inayosambazwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya jamii kuonyesha kuna ufisadi mkubwa kwenye miradi mbalimbali ya Shirika la Taifa la Hifadhi za Jamii (NSSF).

Taarifa ya kuaminika iliyopatikana ndani ya ofisi hiyo na mmoja wa viongozi wa ofisi hiyo, wameeleza kuwa taarifa kamili kuhusiana na NSSF itatolewa na bunge April 25, mwaka huu na wanashangazwa na mambo yanayoenezwa kwenye vyombo vya habari.

Kiongozi huyo mwandamizi huku akikataa kutajwa jina lake alisema hata magazeti hayo yanayoandika uvumi huo, hakuna hata moja linaloeleza kwa ufasaha kuhusiana na ripoti ya CAG.

Ilisema watanzania wanapaswa kutulia na kusubiri taarifa rasmi itakayopelekwa bungeni, kwa kuwa imeeleza kila kitu na sio hicho ambacho kinaonekana kama kinakolezwa na watu wenye maslahi nayo.

"Hata sisi tunashangazwa kumekuwa na msukumo mkubwa na hatujui dhamira yake ni nini, ila tunachoamini tusubiri tu taarifa rasmi ya ripoti itakayopelekwa bungeni,''alisema mtoa taarifa wetu.

Akizungumza na Wabunge wajumbe wa Kamati za Bunge za usimamizi wa fedha, LAAC na PAC, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Profesa Mussa Assad kwenye semina ya mafunzo aliwaeleza wabunge kuwa Ripoti ya CAG anayo yeye na Rais Magufuli tu na anashangazwa na wanaosambaza kinachoitwa taarifa ya CAG wanapata wapi nguvu ya kufanya hivyo.

Profesa Assad alikuwa anajibu maswali ya wabunge ambapo mmoja wa Wabunge kutoka Kambi ya Upinzani alitaka maelezo ya CAG kuhusu kinachoitwa ufisadi katika NSSF.

“taratibu za ukaguzi zinajulikana. Baada ya mkaguzi kuandaa taarifa ya awali hutoa kwa mkaguliwa kujibu hoja za ukaguzi. Kisha Mkaguzi huweza kuziondoa hoja zenye majibu aliyoridhika nayo na baada ya hapo huitwa kikao kinachoitwa ‘exit meeting’ na kukubaliana masuala ya ukaguzi”, alifafanua.

Profesa Assad kwa wabunge wajumbe wa PAC,LAAC na Kamati ya Bajeti. Aliwaeleza wabunge kuwa inawezekana kinachosambazwa ni taarifa ya awali kwa malengo mahususi ambayo yeye kama CAG hawezi kuyajua na kuwataka wabunge wasubiri taarifa yake rasmi itakayowasilishwa Bungeni kabla ya tarehe 25 Aprili 2016.

Kumekuwepo na taarifa mbalimbali, ambazo nyingi zinaonekana zinamtuhumu aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau aliyeliendesha shirika hilo kwa mafanikio makubwa kuhusishwa na vitendo vya ufisadi wa miradi mbalimbali.

Baadhi ya wachunguzi wa mambo wanasema nguvu inayosukumwa kuichafua NSSF ina lengo la kufifisha nyota ya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo kabla ya uzinduzi wa daraja la Kigamboni mnamo tarehe 16 Aprili 2016.


Chanzo: Michuzi
 
Eti NSSF imenunua Hekta moja kwa Tshs.800 Million!!!
Kuna Vichwa Panzi hata ukiwaulize tofauti ya Management letter na Auditors Report ni zipi japo zote zinatolewa na CAG hawaijui, lakin wakajifanya Mafundi wakujadili Auditors Opinion.
 
Nasubiri wazee wa chuki na husda watakavyokuja na kimuhemuhe cha kudai uongo, uzushi na maneno kibao. Dr Dau we will continue to respect and value your contribution to this country. Few visionaries leaders tulionao nchini wewe, Mchechu na Dr Rashidi Taifa iko siku watajuta mmungu atuweke hai tutakuja kuyasema humu humu
 
Hakuna namna ya kuutenganisha ufisadi wa Nssf na Assad,Assad alikuwa board members wa Nssf na sikuwahi nununa jengo LA Nssf tanga,hawezi kuleta taarifa sahihi za Nssf,hutaki poa
 
Hivi kwanini DAU anatumia nguvu kubwa hivi kujisafisha na rundo la ufisadi wa NSSF???
 
hiyo habari ingetoka kwa mara ya kwanza humu JF ningeliweza kuamini,ila sio hicho kiblog uchwara kinachopitiwa na wakuda na mapashkuna kama wewe,ngoja tuone huyu mwizi anavyotaka kutakatishwa
 
Hakuna namna ya kuutenganisha ufisadi wa Nssf na Assad,Assad alikuwa board members wa Nssf na sikuwahi nununa jengo LA Nssf tanga,hawezi kuleta taarifa sahihi za Nssf,hutaki poa

Conspiracy vp mnaogopa kivuli chenu na subiri wasambaza sumu wote tunajua nia zenu. Mnaelekea ukingoni zitajulikana mbivu karibuni tulia.
 
hiyo habari ingetoka kwa mara ya kwanza humu JF ningeliweza kuamini,ila sio hicho kiblog uchwara kinachopitiwa na wakuda na mapashkuna kama wewe,ngoja tuone huyu mwizi anavyotaka kutakatishwa
Usiwe punguani kwa hiyo wewe unaamini ile ripoti ya mara ya kwanza ndiyo ya CAG?
 
Back
Top Bottom