Kichuchunge
JF-Expert Member
- Dec 2, 2020
- 425
- 1,027
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeeleza sababu za kuupeleka mchezo wa marudiano wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Simba SC na RS Berkane ya Morocco, kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, mjini Zanzibar.
Wakati vigogo hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa tayari wameanza kujipanga kuandaa mechi ya marudiano ya marudiano itakayochezwa Mei 25, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, CAF ikaja na wazo tofauti: Mechi ipigwe kwenye uwanja dogo unaobeba mashabiki wasiozidi 15,000 tu, visiwani Zanzibar.
Tayari uongozi wa Simba ulikuwa umeshawahamasisha mashabiki wake kununua tiketi kwa ajili ya mchezo huo kwenye Uwanja wa Mkapa wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 60,000.
Bei za tiketi za fainali zilikuwa kama ifuatavyo: Jukwaa la kawaida: TSh 7,000 VIP C: TSh 20,000, VIP B: TSh 30,000, Platinum: TSh 250,000 ambazo tayari zilikuwa zimeuzwa.
Hata hivyo, taarifa ya CAF iliyosainiwa na Katibu Mkuu wake Veron Mosengo-Omba, na kusomwa na mwandishi wa ukurasa huu, inaweza kuathiri mipango ya Simba.
Katika taarifa hiyo, CAF wamelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kufanya maandalizi yote ya mchezo kisiwani Zanzibar kufuatia mfululizo wa tathmini za kina za kiufundi zilizofanywa na washauri wa kimataifa wa shirikisho hilo la Afrika, huku pia wakizingatia athari za msimu wa mvua zinazoendelea nchini Tanzania.
Kwa tafsiri ya kiswahili, taarifa kamili insomeka:
"CAF inatoa shukurani zake za dhati kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Serikali ya Tanzania, na wadau wote, kwa ushirikiano mkubwa na jinsi walivyojitolea kwa ajili ya maandalizi ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika Mei 25.
Tunatambua na kupongeza kwa dhati uongozi na moyo wa kujitolea ulioonyeshwa na Rais wa TFF Wallace Karia, katika kipindi chote cha mchakato huo.
"Kufuatia mfululizo wa tathmini za kina za kiufundi zilizofanywa na washauri wa kimataifa wa CAF, na kwa kuzingatia msimu wa mvua unaoendelea Tanzania, imependekezwa - kwa mtazamo wa kiufundi - kwamba fainali ifanyike katika Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar.
"Uamuzi huu umechukuliwa baada ya mashauriano ya kina, kwa lengo moja tu la kuhakikisha hali bora ya michezo na uzoefu kwa wachezaji na mashabiki. Kwa vyovyote vile tunatafakari juhudi kubwa zilizofanywa na TFF na uongozi wake, jambo ambalo tunashukuru sana. Tunatarajia kufanya kazi kwa karibu na timu yako ili kuhakikisha mpangilio mzuri na wa mafanikio wa fainali ya Zanzibar."
Simba iliutumia Uwanja wa Amaan katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza dhidi ya Stellenbosch ya Afrika Kusini, mchezo ambao ilishinda 1-0, kabla ya kutoka sare ya 0-0 ugenini na kutinga fainali kwa jumla ya bao 1-0.