Kamundu,
..wako wa-Tz wengi tu ambao ni competent wangeweza kuteuliwa kutumikia wizara ya fedha.
..nadhani JK mwenyewe haamini kama wizara ya fedha ni muhimu kiasi hicho kulazimisha kuteua watu wenye solid track record kutumikia pale.
NB:
..halafu kitendo cha waandishi wa habari kucheka na kuguna kuhusu baadhi ya teuzi za Raisi, kinaleta taswira isiyo nzuri kwa mteuliwa, washauri wa Raisi, pamoja na Raisi mwenyewe.
cc Mchambuzi, Mdondoaji, NasDaz
Ndugu zanguni huyu mwigulu mie sijui kama hii wizara nyeti namma hii ataitendea haki. Au ndo tunajipanga kwa ajili ya 2015
Wakuu,
Hivi hakuna marais WAKUKODISHA?pengine tunaweza tukamkodi OBAMA,au CLINTON wakatusogeza kimaendeleo,maana hawa wenzetu naona kama hawana VISION hivi!wanaongoza nchi kwa mazoea tu!
Naona kama wanajali maslahi Yao zaidi ya maslahi ya nchi!
UCHAMBUZI WA HARAKA:
Yaelekea matatizo ya uchumi wetu si miongoni mwa mambo yanayomnyima usingizi Rais Jakaya Kikwete, ndio maana amefanya kituko cha mwaka kumteua Mwigulu Nchemba kuwa Naibu Waziri katika Wizara hiyo nyeti. Ila mzaha huo ni wa kimkakati zaidi. CCM inahitaji fedha kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu mwaka 2015. Hadi hapo si tatizo, lakini tatizo lipo kwenye kupata fedha hizo kwa njia halali. Ninatafsiri uteuzi wa Mwigulu kwenda Wizara ya fedha kuwa ni sehemu ya mkakati wa kuiwezesha CCM kupata fedha za uchaguzi mkuu ujao. Tutegemea EPA nyingine? Time will tell.
Adam Malima kupelekwa Wizara nyeti ya fedha si jambo la kushangaza, ikizingatiwa yyeye na JK wanatoka mkoa wa Pwani na ukaribu wao. Sijui nini kilichopeleka Juma Nkamia kupewa uwaziri wa Michezo, lakini majibu anayo JK mwenyewe.
BOTTOM LINE: Tatizo sio mawaziri bali Kikwete mwenyewe. Mbunge wa Ubungo aliwahi kuingia matatani alitamka bayana kuwa JK NI DHAIFU lakini ukweli unabaki kuwa ukweli, na alichosema Mnyika ndo ukweli wenyewe. Mawaziri wanaweza kubadilishwa kila wiki, lakini as long as kiongozi wao ni dhaifu, basi tuendelee kutarajia yaleyale yanayopelekea kabineti kubadilishwa mfululizo kama safari za JK nje ya nchi.
Na kwa waliodhani Pinda angeng'oka walikuwa wanaota ndoto za mchana. Pinda ni nyenzo muhimu kwa JK, ni mtu anayebeba lawama za bosi wake. Madudu yakifanywa na JK,lawama zinaelekezwa kwa Pinda.
Tuombe Mungu 2015 ifike mapema, JK amalize majaribio yake ya urais, labda nchi yetu itapata mwelekeo mpya.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
http://www.chahali.com/2014/01/baraza-jipya-la-mawaziri-jk-afanya.html
Mkuu hapa watu hawachezi viduku, hapa kinachoangaliwa ni maendeleo ya Taifa letu. Hilo jembe lako Mwigulu records zake ndizo zinazomhukumu.Pamoja na usomi wake bado hao akina Sugu,Lema na Mbowe wanaona mbali kuliko huyo Mwigulu wako.Unasema watu hawajafika form four, je, wewe mwenye phD umesaidia nini Taifa hili??!!Ona mbali, siyo mbele tu!!Watu mlio wengi humu mnaongea utumbo mtupu hivi mwigulu mnaweza kumfananisha na mavilaza wenu kama wakina Sugu , Lema, Mbowe nk Mwigulu ni jeshi la mtu mmoja na nikiongozi supavu na mwelevu acheni kuongea utumbo humu ndani wakati elimu zenu hata form 4 hamjafika
Hii nchi inaendeshwa kihuni sana..