Sitaki kuamini kwamba kila jambo na wakati wake ila kuanzia LEO itabidi nisaliti amri japo kwa majonzi makuu. Siku kama tano hivi nimekua nanyi humu ndani kwa furaha isiyoelezeka na wakati pia umefika kuwaacha kwa huzuni. Ni huzuni yenye furaha kwani kuwa nanyi kumenifunza na kunielimisha mengi. Kuwa nanyi umekuwa muda mfupi wa burudani. Ninaondoka jamvini ila kabla sijaondoka ninaomba kama kuna yeyote niliyemkwanza aniwie radhi kwani vikombe kwenye sinia havikosi kugongana. Ninawapenda wote na kwa namna ya kipekee natoa shukrani zangu kwa wafuatayo: dume la mende mzee wa tigo, Lizz, Mentor, The boss, Aisha adam,mzee wa kijiji,gambalanyoka,kisasangwe,igwe sr,manyanza,yatima,sangara,dena amsi,mrembo,nyani ngabu,mchillo,shantel,muinjilisti,Russian roulette,afrodenzi,mwanajamiionline,ballerina,sokomoko,nyenyenkuru,mito, miss parliament,sabry001 na wengine wote mlioshirikiana katika kuchangia hoja mbalimbali. MUNGU AWABARIKI SANA TUTAKUTANA TENA INSHALLA.